Wazalendo hapa kuna matokeo zaidi ya kura ya maoni ambayo tumeyapokea na bado hayajawa rasmi.
UNGUJA
Matokeo ya majimbo
Bububu - Ndio: 4978 Hapana: 1622
M/Kwerekwe - Ndio: 3017 Hapana: 2174
Kiembe Samaki - Ndio: 1768 Hapana: 1086
Dole – Ndio: 2429 Hapana: 2527
Kikwajuni – Ndio: 3326 Hapana: 2131
PEMBA
Sikupata matokeo na nambari kamili bali ni the nearest whole number. Pia ni matokeo ya vituo na sio majimbo.
Jadida – Ndio: 1800 Hapana: 200
Utaani – Ndio: 1200 Hapana: 70
Chake Chake – Ndio: 1000
[...]Endelea hapa “Matokeo zaidi ya kura ya maoni”
Majimbo ya Mji mkongwe na Bububu yasema ndio..
Matokeo zaidi kufuatilia usiku mzima
[...]Endelea hapa “majimbo ya bububu na mji kongwe yesema NDIO”
Unaweza kupata picha zaidi za mchakato wa kura ya maoni katika
[...]Endelea hapa “PICHA ZAIDI ZA KURA YA MAONI”
| 31.07.2010 | 15:00 UTC
Matokeo ya muda ya kura kutangazwa kesho, Zanzibar
Zanzibar
Kura ya maoni nchini Zanzibar imepigwa leo yenye lengo la kuamua ikiwa itakuwa na serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba ili kusitisha uhasama uliokita mizizi na kuvuruga maendeleo katika kisiwa hicho cha Tanzania kwa miongo kadhaa.
Wapiga kura laki nne waliojiandikisha walishiriki katika Uchaguzi huo unaonuia kupitisha pendekezo la kufanywa marekebisho katika katiba yatakayotenga nyadhifa mbili za makamu wa rais zitakazogawanywa kati ya vyama vitakavyoshika nafasi ya kwanza na ya pili katika uchaguzi wa wawakilishi.
Uhasama kati ya chama kikuu cha CCM na CUF katika kisiwa hicho cha watu milioni 1.2, umekuwa ukikithiri na
[...]Endelea hapa “Dw-wold.de Deutsche welle Swahili Germany”
Kura ya maoni yafanyika Zanzibar
Kisiwa cha Zanzibar
Kura ya maoni inafanyika Zanzibar hii leo, ambayo inalenga kubadili katiba na kuruhusu uundwaji wa serikali za kuwagawana madaraka.
Zaidi ya wapiga kura laki nne walioandikishwa rasmi wanatarajiwa kupiga kura zao.
Chama tawala CCM na chama kikubwa cha upinzani CUF, vyote vinaunga mkono kura hiyo, ambayo inanuiwa kumaliza ghasia zilizokumba uchaguzi wa siku za nyuma visiwani Zanzibar.
Zanzibar ina utawala wake wa ndani chini ya serikali kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikiwa kura hiyo ya maoni itapitishwa, Zanzibar kwa mara ya kwanza itashuhudia mfumo mpya wa serikali ambapo kutakuwa na rais na makamu wake wawili.
Makamu
[...]Endelea hapa “Report ya BBC Swahili London(uk)”
Matokeo yasio rasmi kutoka Kituo cha Tumekuja
Matokeo ya tumekuja school waliotakiwa kupiga 350, wamepiga 267, kura ndio 231, hapana 33, zilizoharibika 3.
Tumekuja number, wapiga kura 350. wamepiga kura 250 ndio 219, hapana 26, zilizoharibika 5.
Chumba 3, walitakiwa kupiga kura 350, waliopiga 345, ndio 209, hapana 30, ziliharibika 6.
Kituo number4, waliotakiwa kupiga 356, waliopiga kura 252, ndio 224, hapana 26, zilizoharibika.
Kura zote zilizotakiwa kupigwa 1406
Waliojitokeza 1014
NDIO 883
Hapana
[...]Endelea hapa “Matokeo ya Kituo cha Tumekuja [Maoni]“
BBC TUNAWAHESHIMU SANA LAKINI TUNAWAOMBA HIYO PICHA MULIOIWEKA INATUDHALILISHA WAZANZIBAR. ZANZIBAR YA LEO SIO YA 1964 WALA 2005. LEO WATU WANAPIGA KURA KIISLAM NA SIO KIKAFIRI KAMA ILIVYOKUWA IKITOKEZEA KWENYE UCHAGUZI ZILIZOPITA.
TUNAOMBA KUPITIA ALLY SALEH UWAAMBIE JAMAA ZAKO KAMA HAWANA PICHA BASI WACHUKUE HAPA MZALENDO NA TUMESHAWAIDHINISHIA WALA HAWAHITAJI KUOMBA. KAMA MUNAONA TABU BASI NI BORA MUKATUEKEA JAPO YA BAIT AL AJAIB.
UONGOZI WA MZALENDO NAOMBA RADHI KWA KUEKA HABARI HII LAKINI SIJAONA NJIA NZURI YA KUWASILISHA OMBI LANGU ZAIDI
[...]Endelea hapa “SALAM KWA WEB YA BBC YA KISWAHILI”
Zanzibar haikuhitaji kura ya maoni ili kufanya Serikali ya Umoja wa Kitaifa wala haikuweko ndani ya katiba ya Zanzbiar bali ni utaratibu tu wa kusafiana nia, na kuondoa migogoro Zanzibar. Hofu hapa ilikuwa kama ingefanya Serikali ya Umoja wa Kitaifa bila ya kura ya maoni kungetokea vidudu watu wakasema tulifanyiwa tu kura ya Serikali hii lakini haikuwa ridhaa ya Wa-zanzibari. Kwa maana hiyo kuna mantiki ya kufanya kura ya maoni Zanzibar ili kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Ushawishi wa Serikali yeneywe pamoja na Viongozi wa ngazi za juu akiwemo Rais mwenyewe ni kuonesha nia njema ya kutaka kuleta maendeleo badal;a ya kudumu na malumbano
[...]Endelea hapa “KURA YA MAONI ZANZIBAR SI DEMOCRACY BALI PROTOCAL TU YA KUFIKIA TUANPOTAKA”
RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume amemtimu kazi mkuu wa wilaya ya kati Ali Hassan Khamis akidaiwa kufanya kampeni chafu dhidi ya kura ya maoni ambayo itafanyika leo visiwani Zanzibar itakayoamua muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Taarifa kutoka ikulu zimesema rais karume ametmfukuza kazi mkuu wa wilaya hiyo kwa mujibu wa kifungu namba 53(b) cha sheria ya Zanzibar ya mwaka 1984 kinachompa mamlaka rais kumfukuza mtu yeyote katika serikali yake.
Hadi sasa hakuna sababu zilizotolewa kuhusiana na kufukuzwa kazi kwake lakini kwa mujibu wa tetesi ziliopo ni kwamba hatua ya rais karume imefuatia kauli yake ya juzi aliyoitoa katika hafla ya kuzindua majenereta ya
[...]Endelea hapa “mpinga serikali ya umoja afukuzwa kazi”
Habari maarufu