Login



Fotos

Get the Flash Player to see the slideshow.

SHAIRI-NABWA UMETUACHIA KALAMU

NABWA UMETUACHIA KALAMU

Hatua yake ya kwanza
Akifika kaburini
Mimi hilo ndani naliamini
Ni Ali Nabwa kuuliza
Jee huku nilikoletwa
Lipo gazeti niandike?

Hakuna hapa gazeti
Ataambiwa na karipio kupewa
Sharubu za Munkar akikaziwa
Wewe vipi, kwanza hapa zoea
Makazi yako ya kudumu
Ndipo mengine uulize
Tuanze na takadumu?

Nipeni niandike makala zangu
Duniani kule ambazo
Sikuwahi kuzimaliza
Maana uhai nimekatizwa
Nikiwa nina mengi umma kueleza
Uss!! Ataambiwa

Hiyo ndivyo atakavyokuwa
Mwenzetu huyu alotangulia
Alietuachia sisi ukiwa
Ukiwa wa habari na taarifa
Kiza…kiza hata kupapasa hatuwezi
Wengine ndio kwanza maziwa
Ametuachisha…kunyonya uwezo wake

Ghafla taa imezimika
Tukiwa katika meza
Mbele ya kompyuta yetu
Tukiandika habari… kujuvya umma
Na yeye kinara wetu
[...]Endelea hapa “SHAIRI-NABWA UMETUACHIA KALAMU”

Mjuwe aduwi wako na sifa zake.

MJUWE ADUI YAKO

KIFUATACHO NI KITAMBULISHO CHAKE

JINA
Ibilisi

MJI
Ndani ya nyoyo za walioghafilika

KABILA
Mashetani

MWISHO WAKE
Ndani ya moto wa Jahannam

Endelea kusoma Mjuwe aduwi wako na sifa zake.

ZANZIBAR NI YAKO YOTE; URITHI NAKUACHIA

mwanangu nisikilize
leo nitayokwambia
si mengi yakuliwaze
utajiri asilia
Zanzibar ni yako yote
urithi nakuachia

Kiwa nyumbani UK
na Omani Arabia
Canada, Norway, Sweden
Denmark Scandanavia
popote utapojiri
ulimwenguni sikia
Zanzibar ni yako yote
Urithi nakuachia

utapochoshwa baridi
na zahama za dunia
nakuomba kwenu rudi
liwazo lipoanzia
na uje uufaidi
upepo Zanzibaria
wa karafuu, waridi, rehani na pompia
Zanzibar ni yako yote
urithi nakuachia.

urudi kwenu urudi
kwenu ulipotokea
urudi kwenu urudi
wazee mejinamia
urudi kwenu urudi
nduguzo kufurahia
urudi kwenu urudi
rafiki wakufikiria
Zanzibar ni yako yote
urithi nakuachia

mzee wako hakika
nguvu zinaniishia
milele hapana shaka
nawe sitokua pia
nakuachia msewe
sijebadili tabia
Zanzibar ni yako yote
urithi

[...]Endelea hapa “ZANZIBAR NI YAKO YOTE; URITHI NAKUACHIA”

Uzuri wa kitu kwa nje si usalama wa ndani

Papai jama papai, lanipendeza machoni,
Kwa yake rangi papai, halinitoki usoni,
Hata nikifunga tai, nalisogeza mdomoni.
Nikilikata papai, kumbe lishaaoza ndani

Ukiliona ni zuri, machoni linavutia,
Ni kwa yake rangi nzuri, mikononi ukilitia,
Njano na kijani nzuri, na umbole vyavutia,
Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani

Yapo mapapai mengi, kwa zake rangi tofauti,
Na mitaani kwa wingi, na hayahitaji suti,
Pia sokoni ni mengi, tena hayana masharti,
Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani.

Ni mazuri sana kwa nje, shida yake kule ndani,
Ukiyaona yalivyo nje, huna swali na ndani,
Yanavutia sana nje, yanachefua kwa ndani,
Nikilikata papai, kumbe

[...]Endelea hapa “Uzuri wa kitu kwa nje si usalama wa ndani”

Paradise Lost

Paradise Lost
Paradise lost is a poem written by Prof. Yusuf Kassam, formerly of the University of Dar es Salaam and currently living in Toronto, Canada.According Prof. Abdulaziz Lodhi of the Department of Linguistics & Philology, Uppsala University in Sweden, Yusuf Kassam was an outstanding student at the former King George VI Grammar School (Now: Lumumba Secondary School). He was among the first Zanzibaris/Tanzanians to have published poems in English.

PARADISE IS LOST

I left Zanzibar, island of spices,
To emigrate to Canada, land of opportunity.

Forsook the tropical sun
For cold frigid weather.
Left behind the warm ocean breeze
For the windchill of winter.

Abandoned white pristine beaches
[...]Endelea hapa “Paradise Lost”

Umoja wa Zanzibar-shairi

Assalaam Alaykum

kwa wanaoenda mashairi

baada ya dhiki faraja, wakuu wameamua
mambo huenda yakaja, hasama zikapungua
yaliyopita si hoja, udugu waufufua
jana tulihunzunika, leo tunafurahika

Ingawa twajikongoja, kwema twaelekea
mwanzo wa hesabu moja, kuzuri twakaribia
si lazima kwa koroja, mema sasa twasikia
jana tulihunzunika, leo tunafurahika

chuki waziweka nyuma, pamoja washikamana
furaha kubwa adhima, mioyo yatulizana
kamwe hatutosimama, kitete twashikamana
jana tulihunzunika, leo tunafurahika

mzigo wameutuwa, adui anaumia
sasa mambo yatakuwa, ya kale yatarudia
kasheshe zitapungua, jamii itatulia
jana tulihunzunika, leo tunafurahika

wakawa hawazikani, wafu wakiterekezwa
udugu na ujirani, kuyaeleza nashindwa
tafurani mitaani, vyama vikaendkezwa
jana tulihunzunika, leo tunafurahika

serikali ya pampoja, raia wahamasishwe
haki kwa kila mmoja, faraja iwasilishwe
wapemba na waunguja,

[...]Endelea hapa “Umoja wa Zanzibar-shairi”

Methali za kiswahili

1. Adhabu ya kaburi aijua maiti, The touture of the grave is only known by the corpse
2. Akiba haiozi, A reserve will not decay
3. Asifuye mvuwa imemnyea. He who praises rain has been rained on.
4. Akili nyingi huondowa maarifa. Great wit drives away wisdom
5. Asiye kubali kushindwa si mshindani.He who does not admit defeat is not a sportsman
6. Atangaye na jua hujuwa. He wanders around by day a lot, learns a lot
7. Asiye kuwapo na lake halipo.If you

[...]Endelea hapa “Methali za kiswahili”

Wazanzibari wamtaka tena Karume – Utenzi

UTENZI ULIOSOMWA KATIKA MAANDAMANO YA KUUNGA MKONO PENDEKEZO LA KATIBU MKUU LA MABADILIKO YA KATIBA YA ZANZIBAR, 16 Januari 2010
Endelea kusoma Wazanzibari wamtaka tena Karume – Utenzi

Nchi yetu rudisheni, msitupige binduki

Twataka amani, bila risasi…
Tukiwapa nafasi, mwatengeneza bunduki…
Tukiwapa ishirini, mwataka mamilioni…
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki

aliye na akili, hauzi yake nchi

aliye jasiri, hatishiki kirahisi

aliye na kasi, huepuka risasi

Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki

asiye na mali, ni Mola hamumwamini
asiye na kazi, masaa hayampiti
asiye na jirani, ya ulimwengu ni ubishi
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki

shida mitaani, twatafuta riziki

shida nchini, wenzetu wana chuki

Shida serikalini, ubaguzi hamuachi

Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki

Twataka amani, bila risasi…
Mamboleo ukoloni, leo hauna nafasi
Tukiwapa nafasi, mwatengeneza bunduki…
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki

Wenzetu tuliwadhani, kumbe mu-nyoka mioyoni..
Ndugu

[...]Endelea hapa “Nchi yetu rudisheni, msitupige binduki”

KUUKOMBOA WA'TANI

KUUKOMBOA WA’TANI
(Kutoka Katika FZV)

Date:  25 February, 2005

Utenzi huu ulitolewa katika gazeti la Umoja wa Wazanzibari (Free Zanzibar Voice) mnamo 1968 linaonesha hisia za Mzanzibari mwenzetu akitunadia katika ukombozi wa Wattani wetu, juu ya fahamu yake kuwa Wattani ndio mama yetu. Ni miaka thalathini na saba, yaani tangu 1968; lakini yaliosemwa ni madhubuti na ni kama yamesemwa jana au leo. Hapana shaka Wazanzibari ni wenye uwezo wa kuirejesha Dola yao Huru ya Zanzibar kama ilivyokuwa kabla ya mavamizi ya 1964. Penye nia pana njia.

  1. Wat’ani watoja damu, ‘tabibu twapiga hodi
    Hima hima muadhamu, Sinene nenda urudi
    Kukawia ni haramu , na kutoa huna budi
    Kwani hii ni

    [...]Endelea hapa “KUUKOMBOA WA’TANI”

Page 1 of 212