Habari

MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAWAIDA CHA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA

MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAWAIDA CHA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI)
P.O. BOX 3637, Zanzibar, Tanzania

MAAZIMIO YA KIKAO CHA KAWAIDA CHA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-CHAMA CHA WANANCHI) LILILOFANYIKA TAREHE 19 MACHI, 2017 KATIKA UKUMBI WA OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CHAMA ILIYOPO VUGA, MJINI UNGUJA-ZANZIBAR.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) limekutana jana Jumapili tarehe 19 Machi, 2017 katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya chama iliyopo Vuga, Mjini Unguja-Zanzibar, kikao ambacho kiliitishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 80 (1).

Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa Mheshimiwa Julius Mtatiro na kilihudhuriwa na Wajumbe halali 43 kati ya wajumbe wote Halali 53 wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa waliopaswa kuhudhuria kikao hicho.Wajumbe wanne kati ya hao hawakuweza kuhudhuria kwa kutoa udhuru kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwa nje ya nchi. Wajumbe hao ni Ismail Jussa, Ahmed Marshed, Juma Mkumbi na Hashimu Mziray.

Kikao hicho kilipokea, kuzijadili na kufanyia maamuzi mbalimbali Ajenda Kuu Nane 8 zilizotayarishwa na kuwasilishwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kama ifuatavyo:
1. Kupitia na kuthibitisha Mihutasari na Yatokanayo na vikao vya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa vilivyofanyika Tarehe 20/8/2016, 28/8/2016 na Tarehe 27/9/2016
2. Hali ya Kisiasa na Kiuchumi nchini.
3. Taarifa za Kesi mbalimbali zinazoendelea Mahakamani pamoja na Kesi ya wizi wa fedha za Ruzuku ya Chama kiasi cha shilingi 369 milioni uliofanywa na Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi, Ibrahim Lipumba na washirika wao.
4. Taarifa ya Hujuma zinazofanywa na Lipumba na kundi lake dhidi ya Chama, wanachama na Viongozi wa Chama na Taarifa ya hatua za kinidhamu zilizochukuliwa na Matawi ya Chama dhidi ya wanachama waliokiuka Maadili, Katiba ya Chama na kuwa na mwenendo usiofaa kwa Chama.
5. Taarifa ya Ushindi wa Chama katika Uchaguzi Mdogo wa mitaa uliofanyika Manispaa ya Lindi tarehe 12/3/2017.
6. Taarifa ya Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Maalim Seif Sharif Hamad, kisiwani Pemba, Zanzibar. Programu ya Kuimarisha Chama nchini na Muongozo wa kazi za Waratibu wa Chama.
7. Taarifa ya michango ya fedha kutoka kwa Viongozi na Wanachama wa CUF Tanzania Bara na Zanzibar.
8. Mapendekezo ya Uteuzi wa Wagombea wa Chama katika Ubunge wa Afrika Mashariki.

Baraza kuu la uongozi Taifa baada ya kupokea na kujadili ajenda hizo kimepitisha na kuazimia yafuatayo:-

1. Kuhusu utekelezaji wa Maagizo kwa Kupitia na kuthibitisha Mihutasari na Yatokanayo ya vikao vya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa vilivyofanyika Tarehe 20/8/2016, 28/8/2016 na Tarehe 27/9/2016:
Baraza Kuu limeipongeza Kamati ya Utendaji ya Taifa kwa kusimamia utekelezaji wa Maazimio yote muhimu yaliyoagizwa katika kipindi chote ambacho kwa makusudi

Share: