Habari

BAADA YA ZANZIBAR KUPATA UANACHAMA WA CAF

BAADA YA ZANZIBAR KUPATA UANACHAMA WA CAF

Rashid bin Mwinyi

Awali ya yote nichukue fursa hii kuwapongeza wale wate waliofanikisha Zanzibar kupatiwa uwanachama wa CAF kwa namna moja au nyengine. Lakini pili tuwashukuru wanachama wote wa CAF waliopitisha adhimio la Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF. Pili nitoe maoni yangu juu ya Zanzibar kuwa mwanachama wa CAF kama ifuatavyo:-

1) Tuanze na ZFA, Kuwa mwanachama wa CAF maana yake tumeingia katika ulimwengu wa Soccar, hivyo basi watendaji wa ZFA waache kufanya kazi kimazoeya na wafanye kazi kwa misingi ya uwazibikaji na uwazi ili kufikia lengo la kuwa wanachama wa CAF.

2) Kwa serikali, Serikali yetu ya Mapinduzi Zanzibar ni lazima ichukue jitihada za makusudi kuimarisha miundombini ya mpira wa miguu ili kuhakikisha kuwa mpira wetu unaimarika na kuweza kuingia katika ushindani wa kimataifa. Pia ipige jitihada ya hali ya juu kuweza kuandaa timu ambayo itaweza kushindana katika mashindano ya kimataifa. Sasa timu ya taifa iwepo muda wote na sio sio kuundwa ma kuvunjwa kwa kuwepo mashindano fulani au kumalizika mashindano fulani.

3) Kwa vyombo vya habari, ikumbukwe kuwa vyombo vya habari vinamchango mkubwa katika kukuza kiwango cha mpira kutokana na utendaji wao kazi. Kwa mfano Mpira wa Uengereza hauwezi kuulinganisha na Mpira wa Uhispania lakini mpira wa uhispania unaonekana kuwa juu kutokana na jitihada za vyombo vya hari kuutangaza mpira wao. Hivyo basi vyombo vya habari vya Zanzibar navyo vichukue jitihada za ziada kuutangaza mpira wetu ili kuutia thamani ndani na nje ya nchi.

4) Kwa wachezaji, Sasa Zanzibar imekuwa kwenye ulimwengu wa soka, mambo ya kitoto na yasiyoleta tija katika soccer yaachwe na wachezaji na wawe na ari ya kuletea mafanikio katika timu yetu ya taifa ili tuweze kufika mbali.

Kwa kumalizia napenda kuwashauri Wazanzibar wote wafurahie kitendo cha Zanzibar kupatiwa uwanachama wa CAF na kuungana kwa pamoja kwa lengo la kuleta mafanikio ya timu yetu ya taifa.

FB

Share: