Habari

Bado ni uvumi – lakini, ‘lililoko mkondoni lisubiriwe ufukweni’

Na Nurdin Msati – ukurasa wa ‘facebook’

Alhamisi, May 18, 2017

MAPYA YAFICHUKA MGOGORO NDANI YA CUF.
BAADA PLAN A KUSHINDIKANA SASA MAADUI WAANDAA MBINU MPYA.

Ukiulizwa Nchi gani iliyojaa wasomi wenye kutia hasara mataifa yao Afrika Mashariki jibu lisilo na shaka utaitaja Tanzania.

Kwa utafiti wangu nimebaini mtaala wa maisha hapa Tanzania umetawaliwa na mfumo wa undugu hivyo kama kuna kiongozi katoka kanda fulani basi watu wote kutoka eneo hilo lazima watajiona wameula kwani uzawa ndio itakuwa CV kwao kupata riziki kupitia mtawala huyo.

Tunayaona haya yakijiri ndani ya CUF.
Nimeambiwa Bodi ya LIPUMBA na wafuasi wenzake walioasisi mgogoro huu ina lazimishwa kutambuliwa kwa msaada wa anayelindwa ili yafanyike mambo yafuatayo:-

1. Bodi halali ya CUF ifutike na kukosa watu wa kulinda mali na maslahi ya Chama.

2. Board HIYO ya LIPUMBA itakua na wajibu wa kufuta kesi zote zilizofunguliwa kwani kupitia board ya zamani watuhumiwa wanaweza kutiwa hatihani.

3. Kituko kikubwa baada ya kutabuliwa board hiyo inayoandaliwa na maadui wa CUF anatakiwa LIPUMBA atangaze kuitambua Serekali ya Dr. Sheni na kutangaza CUF kujitoa katika UKAWA!

Maajabu ya Dunia LIPUMBA sio mpiga kura na wala sio Mzanzibari, hata akitangaza kumtambua Sheni ndio wataweza kuzika HAKI ya Wazanzibari?

Baada ya kutekeleza maagizo hayo yanayosukumwa na ukanda na ukabila, CUF itaingizwa kwenye mgogoro mkubwa kuliko huu wa sasa.

Wana CUF tuwe makini kwani hata wale waliokua wanaushabikia mgogoro huu kwa sasa wamekua mateka wanaamuliwa kutekeleza kila kile wenye mgogoro wao wanachokitaka.

Vijana wa BENGHAZI walioasisi vurugu Libya wamekimbia Nchi kama walivyoanza kukimbia vijana wa CUF walioshiriki KUMPELEKA LIPUMBA BUGURUNI.

Kwa sasa maadui wanaivuruga LIBYA watakavyo na ndivyo kwa sasa maadui wanavyo ivuruga CUF watakavyo, huku hawa vijana mamluki wakibaki mateka.

Ndugu zangu, CUF tukijisahau LIPUMBA ataweza kutimiza lengo lake la kukidhoofisha Chama chetu.

MAPYA YAJA MGOGORO WA CUF LIPUMBA KUTOKA BUGURUNI MPAKA ZANZIBAR KUMTAMBUA SHENI.

Share: