HabariMakala/Tahariri

BARUA YA WAZI KWA MUHESHIMIWA WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR

Muheshimiwa waziri wa elimu Zanzibar natumai kuwa umzima wa afya na unaendelea na majukumu yaliyokutiknga kwanza nikupe pole kwa majukumu yako mazito lakini pia nikupe hongera kwa kuwa waziri kijana kuliko mawaziri wote wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Mheshimiwa waziri wa elimu Zanzibar napenda nikuandikie barua hii nikiwa na wingi wa furaha iliyochanganyika na huzuni nafsini mwangu kwa yanayoendelea kutokea.
Muheshimiwa waziri wa elimu kama unavyojua elimu yetu ya juu ni suala la muungano miongoni mwa mambo ya muungano ya jamuhuri ya muungano wa tanzinia ni suala la elimu ya juu.

Muheshimiwa waziri tumeona mwanzoni mwa mwezi julai mwaka 2016 tume ya vyuo vikuu ilitoa tamko la kubadilisha vigezo vya kujiunga na vyuo vikuu kwa wanafunzi wa F6 na wale tuliopitia diploma sambamba na kukataliwa kwa pasi ya Dini kwa kidato cha nne pasi ambayo ndio kimbilio na kiengeza sifa kwa wanafunzi wa Zanzibar kutokana na uhalisia kuwa kwenye masomo ya sanyasi bado hatuja jiimarisha sawa sawa hivyo kufanya wanafunzi wengi wa kizanzibari kubakia katika masomo ya sanaa kuwa kimbilio lao na pasi ya dini ikiendelea kuwabeba.

Muheshimiwa waziri Sidhani kuwa wizara ya elimu Zanzibar ilishirikishwa katika mabadiliko hayo. Lakini kama hilo halitoshi muheshimiwa waziri wa elimu tumeona pia mambo yanayoenda kutolewa matamko na waziri mwenzako wa elimu wa Tanganyika kuwa nikinyume na Sera ya Elimu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 2014 lakini pia sio sera ya muungano tu pia ni ukiukwaji mkubwa wa sera ya elimu ya Zanzibar ya mwaka 2006.

Muheshimiwa waziri leo tukilala tukiamka tunasikia mama Ndalichako anatoa matamko ya kupiga marufuku kuvaa majoho kwa wanafunzi wa diploma na certificate hatuja kaa vizuri tunatafuta wadaiwa sugu wa mikpo hatujatulia tunasikia kuwa ni marufuku kusomea shahada kwa kigezo cha kupitia diploma hatujatulia tena tunaambiwa nimarufuku kusoma pre university yaani foundation ya kujiunga na chuo kikuu kwa waliopungukiwa na sifa.

Muheshimiwa waziri ni wakati sasa wa kusikia sauti yako juu ya hili hasa hili suala la pasi ya dini, majoho, wanafunzi wa diploma na pre university. Tunataka tusikie kauli yako suala la joho hili naweza kuliita kama kichekesho lakini suala la Wanafunzi wa diploma kujiunga na shahada ya kwanza ni kinyume na sera ya elimu Zanzibar amabayo inazungumzia kuengeza vijana wa kujiunga na vyuo vikuu siku hadi siku na kuengeza idadi ya vyuo vikuu zanziabar suala hili la kuondoa pasi ya dini kuwa pasi ya ufaulu na suala la marufuku ya kujiunga shahada kupitia diploma inalisimamisha lengo hilo muheshimiwa waziri.

Muheshimiwa waziri wakati umefika wa kutuonesha wapi yanaanzia haya mashirikiano yetu kielimu hili pia tuna mashaka nalo ifike wakati tuende na mahitaji yetu je masharikiano hayo yanaaza na F4, F6, certificate na Diploma, Shahada au Master. Mbona sera yetu ya elimu inapingana na matamshi ya kila siku ya waziri huyu mama ndalichako. Muheshimiwa waziri inatupaswa sasa tuwe na msimamo juu ya hili tunakutaka utoke hadharini utuambie wewe kama waziri mwenye jukumu la kusimamia elimu Zanzibar msimamo wako ni upi juu ya mambo haya.

Muheshimiwa waziri vijano wako tulioko vyuoni tumechoka na matamshi haya tunasoma tukiwa na fadhaa kwani kesho yake hatujui mama ndalichako atatwambia nini. Muheshimiwa waziri wewe ndio mwenye dhamana ya elimu wazanzibari 100% tunasubiri utatwambia nini kwa mustakabali wa elimu yetu kumbuka kuwa vijana wengi wapo mtaani wakitafakari hatma yao kwa kukosa vyuo na kukosa mikopo angalau tusikie kauli yako muheshimiwa waziri ili tupate faraja.

Kumbuka maneno ya hayati karume kwamba tunahitji kujitawala tujiamulie mambo yetu wenyewe huo ndio uhuru tunaoutafuta hakusita tena akasema kwamba mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe, lakini pia kumbuka malengo ya mapinduzi kuwa ni mambo matatu kupiga vija adui ujinga, maradhi na umasikini na hili analolifanya ndalichako nikuturejesha ujingani.

Wako.
Mwanafunzi wa ZANZIBAR UNIVERSITY
First Year
SEIF HAMAD SULEIMAN.
Seif0772010217@gmail.com
Simu: 0655180217.

Share: