Mipango ya wayahudi dhidi ya uislamu Zanzibar
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 29/10/2009 // DIRA // Zima maoni
Na Ali Nabwa
HIVI sasa ulimwengu unaadhimisha mwaka mmoja wa maafa ya Tsunami, maafa ambayo Chama Cha Mapinduzi,CCM,kiliyafurahia sana kiasi ya kuyafanya kigezo cha ushindi wake katika uchaguzi uliomalizika punde hivi,kwanza Zanzibar na baadae Tanzania nzima.
Chama Cha Mapinduzi kina sifa moja,kikise! ma kitafanya maovu amini kitafanya kweli.Tsunami tumeiona na tunaendelea kuiona.Watu wa Piki,Kaskazini Pemba,na Tumbatu Chwaka,Kaskazini Unguja,bado wamo katika gharika ya Tsunami ya Mkapa na Karume.Hakuna anayejali,kwani huu ni sehemu ya mkakati maalum wa Judeo-Christian axis (mtandao wa Mayahudi na Wakristo,hivyo haishangazi kua Mayahudi ndio makungwi wa vitimbi vya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar) ‘kuumaliza’ Uislam.Zanzibar ni kitovu cha Uislam katika Bara la Afrika na mkakati ulianza zamani kuendesha ‘crusade’ ya nguvu hapa.
Ilianza mwishoni mwa karne ya 19 ambapo mtandao wa utawala wa kiislam (sio Waarabu)ulioenea kutoka Mogadishu hadi Sofala,Bwagamoyo hadi Maziwa Makuu u! lipomegwa megwa,tukaishia na Zanzibar,Mwambao wa Kenya (the ten mile strip) na Comoro.Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitamani angeliweza kuisukuma mbali Zanzibar katika Bahari ya Hindi.Aliiona kama mwimba katika mwili wa Catholic hegemony (utawala wa kanisa katoliki)barani Afrika,na bado ni mwiba.Ndipo juhudi zikaendelea,na zinaendelea kufanywa,sio tu kuvidhibiti Visiwa hivi bali Waislam wa Tanzania kwa jumla.Kuna ushahidi kua Afro-Shirazi Party,chama ambacho Julius Nyerere alishiriki katika kuanzishwa kwake kilidhibitiwa na Wakristo(soma ‘Simulizi za Thabit Kombo’).
Nakumbuka mara tu baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulipolazimishwa baadhi yetu tulilalamika,lakini yule mwanafalsafa mashuhuri Abdulrahman Mohamed Babu akasema kua “Si vibaya.Zanzibar ndogo ni vigumu kuathiri vugu vugu la mageuzi Afrika,lakini Tanganyika inaweza kuwa na ‘impact’(athari)kubwa.”Leo tunashuhudia hayo.Ingawa Babu alimaanisha vugu vugu la Kimarx,lakini leo tunaona vugu vugu la Waislam Tanzania nzima kugombea (sio kuomba) haki yao kama raia halisi na sio ‘Second class citizens’ na hatujui yataishia wapi.Pengine yasingekuja haya,au yangechukua muda mrefu kama si maovu yaliyotendwa Zanzibar,yakianzia na mapinduzi ya 1964 na muungano uliolazimishwa miezi mitatu baadae,yakihitimishwa na chaguzi tatu za kiharamia.
Si azma ya mahala haya kuingia kwa undani katika ukweli wa mapinduzi na muungano huo,wakati wake utakuja panapo uhai na majaliwa.Leo nataka kuzungumzia nafasi ya Waingereza na Marekani katika kadhia hizo mbili na kwamba wana dhima ya kufuta dhambi zao kama si kwa kutenda basi kwa kutotenda.Nitafafanua baadae,lakini kwanza tuangalie kwa ufupi vipi dola mbili hizi zimetufikisha tulipofika kiasi kwamba nchi hii maarufu ulimwenguni kwa ustaarabu leo inanuka kwa ushenzi unaoweza kulinganishwa na tawala za kina Bedel Bokassa wa Afrika ya Kati na Macias Nguema wa Equatorial Guinea.
Nathubutu kusema Waingereza walijua,kama hawakua nyuma ya,mapinduzi ya 1964,mapinduzi ya kupindua utamaduni wa kiislam katika Visiwa hivi.Kwanza polisi ilikuwa mikononi mwao na walikuwa na mtandao mkubwa wa mashushu,akiwemo Abeid Amani Karume.Kuna ushahidi kwamba baada Karume kuwajulisha kua ule mpango uliopangwa utatekelezwa usiku wa Jumamosi ile ya Januari 11 (soma Simulizi za Thabit Kombo),hatua madhubuti zilichukuliwa kuhakikisha kua wakorofi wote wanadhibitiwa ili mpango ufanikiwe.
Jeshi la polisi lilikua chini ya Wazungu wafuatao: Mayer na Sulivan (Makao Makuu),Speight (Special Branch na CID),Durham na Bisset (Po! lice Barracks na PTS) na Warring (Police Mobile Force,PMF).Lakini kulikuwa na wazalendo waliokuwa na vyeo vya juu.Kwa mfano,Ali Said Kharusi akitegemewa kuwa Mkuu (Kamishna) wa jeshi hilo baada ya wazungu kuondoka na Sketty,mzaliwa wa Mombasa,naye alikuwa akitumainiwa sana.Hawa walipangiwa shughuli nje ya mji wa Zanzibar siku hiyo. Sketty alipojaribu kurudi kutekeleza wajibu wake aliuliwa kinyama.
Ni mpango kabambe unaodhihirish siasa chafu walioicheza Waingereza.Leo tutachukua mfano mmoja tu wa Assistant Superintendent(ASP) Warring,aliekuwa na dhamana ya kambi ya Mtoni ya PMF.Kwa mujibu wa habari za kuaminika,Warring alikua anajua mpango wa mapinduzi na alikuwa na jukumu la kuufanikisha.Zanzibar haikuwa na jeshi(army)wakati ule na PMF ndicho kikosi kilichokaribiana na jeshi (para military),hivyo kutekwa kwake ilikua muhimu na Warring ndiye aliyehakikisha hilo.
Usiku ule Supt. Misra (mzalendo)alimuamuru Warring kuwazatiti wapiganaji wake kwa silaha kwa vile walikwisha kua ‘tipped’ (kubonyezwa) na Karume kua jaribio la kuipindua serikali lingefanyika usiku ule.Misra alikua mkubwa kuliko Warring kwa cheo na hivyo kamanda wa kambi ya Mtoni ilibidi atii amri.La kushangaza ni kwamba Warring alikataa,jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kijeshi.
Kambi ya Mtoni ilikuwa na wapiganaji wapatao 300 waliopata mafunzo mazuri.Kila ‘guard’ (zamu ya ulinzi) ilikuwa na watu 10,kila mmoja akiwa na risasi 10.Wangeliweza kukabiliana vizuri na wale wavamizi wa kuokotwa mitaani ambao baadhi yao walijifetulia risasi wenyewe kwa kutojua kuzitumia silaha. Lakini wapi ! Warring aliwanyanganya risasi wakabaki na bunduki tupu.
Misra alirudi tena na wakawa na ubish! i mkali na Warring,lakini Muingereza huyo alisimama kidete kua hapewi mtu risasi.Kwa maneno mengine, “he disarmed the camp,” aliipokonya kambi silaha.Kama hiyo haitoshi,mnamo saa 7.45 usiku aliwaamuru wapiganaji wote waende zao nyumbani.Hata hivyo,kabla hawajaondoka ikapigwa tarumbeta ya kuashiria hatari.Huo huwa ni mwito wa kuwataka askari wakimbile ‘Quarter Guard’.Lakini jinsi ilivyokua inalia ile tarumbeta,iliwatia wasi wasi wale askari na wakaambizana watulie waangalie yanayotendeka.Muda si muda wakaona Land Rover za kambi yao zimewashwa taa ‘full’,ikifuatiliwa na uvunjaji wa Quarter Guard
Wakati wote huu Warring alikua amepoa nyu! mbani kwake pale kambini.Askari mmoja,Aboubakar Ali,alisema “Ni bora kufa kuliko kukimbia.” Hajaonekana hadi leo.Wengine waliojaribu kuonesha ushujaa licha ya kuwa mikono mitupu,kama Ali Ruku,Khamis Habib na Said Nassor waliuliwa papo hapo.Baada kazi kumalizika,Warring alionekana akitoka kambini pole pole bila wasi wasi akiwa ndani ya gari na familia yake huku wavamizi wakimuangalia bila kujali. ‘ Mission accomplished’.
Mchango wa Marekani,hasa kwa kupitia jasusi Frank Caluci,katika kulazimisha muungano(uuaji wa Dola ya Zanzibar )umeelezewa vya kutosha ! na hakuna haja ya kuchukua nafasi hii finyu kurejea yaliyokwisha kusemwa.
Haya,mapinduzi na muungano,ndio yaliyoitia Zanzibar utumwani hadi kufika Benjamin Mkapa kuleta majeshi kupiga,kubaka,kutesa,kunyanyasa na hata kuua wananchi wasio na hatia. Na bado yanaendelea Piki,Tumbatu Chwaka na Nungwi. Ili kuhakikisha uvamizi huu wa kijeshi unabaki daima (permanent)hivi karibuini wamezua kukamatwa silaha Nachingwea eti zilizotaka kuletwa Zanzibar.Hii ina lengo la kuhalalisha kubakia jeshi la uvamizi visiwani.
Uchafuzi uliofanywa Oktoba 30 na Disemba 14 kwa jina la uchaguzi ulikua wazi kwa kila mmoja kuona.Mtu angelidhani hii ilikua fursa kwa wale waliotuletea balaa hili kurekebisha madhambi yao . Hakuna dalili.
Kuna mtu mmoja maarufu ambaye alikuwa na tabia ya kuharibu watoto wa kiume.Wazee wakamnasihi aache,lakni akajibu, “Mbona nilipokua naharibiwa mimi hamkusema ?” Wazanzibari wamekwisha kukat! a tamaa na demokrasia ya Magharibi na wanasema ni bora kuweka wazi kua tuko katika mfumo wa chama kimoja.Ningewashauri hawa waliotuletea mfumo huu,pamoja na madalali wao wa Mlimani Dar es Salaam waweke masikio wazi wasikize Wazanzibari,hasa mashababi ,wanazungmza nini siku hizi.Kama ‘wahisani’ wameshindwa kuwatetea Wazanzibari (na Watanzania wote wanyonge),basi wakae kimya wanyonge hao wakiamua kujitetea wenyewe,vinginevyo ‘wahisani’ hao watajitumbukiza kwenye matope watashindwa kutoka.
@Makala ya Dira, kichwa cha habari hakijulikani kimeongezwa na MZALENDO.NET ADMIN.
Niliwahi kuandika habari ya kikundi cha Jingoists cha Uingereza waliokuwa na msemo, “We don’t want to fight,but by jingo if we do”,wakimaanisha, “Hatu! taki kupigana lakini ikibidi ole wenu.”



