Serikali ya Muungano yateka nyara mzozo wa WASHIRIKA

Written by  //  27/10/2009  //  DIRA  //  Zima maoni

jeshi
Rais wa Finland, Tarja Kaarina Halonen akikagua gwaride la heshima la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Zanzibar juzi kwa ziara ya siku moja. (Picha na Mpiga Picha Wetu).

Na Ali Nabwa

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepeleka Bungeni katika kikao kilichoanza wiki hii, mswada ambao unapingana na Tume iliyoundwa kujaribu kutatua mzozo wa miaka mingi kati ya Umoja wa Ushirika wa Tanzania (TFC) na vyama vitano vya ushirika Zanzibar.

Mswada huo unaojulikana kama The Financial Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2003 unahusu Marekebisho ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya 1991,Marekebisho ya Sheria ya Benki ya Tanzania ya 1995 na Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Ushirika

ya 1991.

Marekebisho ya Sheria ya Ushirika yanahusu mikopo midogo midogo (regulations pertaining to micro-finance companies).

Kinachowashangaza wachunguzi wa mambo ya siasa na fedha,hasa katika sekta ya Muungano wa Tanzania, ni kwamba imeundwa Tume kushughulikia mgogoro mpevu na wa muda mrefu kati ya Zanzibar na Bara kuhusu masuala ya fedha za Washirika (Cooperative Union of Tanzania, CUT). Tume hiyo inatazamiwa kuwasilisha ripoti yake mwisho wa mwezi huu wa Februari.

Inaendelea katika Uchambuzi wa siasa

Top

Watoto wa Karume waingia mitini

Na Mwandishi Wetu

WATOTO wa Rais Amani Karume ambao wamelishitaki gazeti la Dira hawakuonekana Mahkamani siku ya Jumatano, Febuari 5 ambapo kesi hiyo ilikuwa isikilizwe; si wao wala wakili wao.

Watoto hao, Abeid Amani Karume na Amina Amani Karume, wamefungua kesi ya madai Na. 4/2003 dhidi ya Zanzibar International Media Company Ltd (ZIMCO), wachapishaji wa gazeti la Dira na Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo kwa madai kwamba wamevunjiwa heshima katika toleo la Dira Na. 007 la Januari 17 – 23, 2003.

Kesi hiyo ilikuwa ianze kusikilizwa Jumatano Febuari 5 katika Mahkama Kuu ya Zanzibar, Vuga, mbele ya Jaji Bakari Mshibe. Hata hivyo, Jaji Mshibe ilielezwa kuwa

amekwenda Pemba kikazi na kesi hiyo ikapelekwa kwa Jaji Saleh Dahoma kwa ajili ya kutajwa.

Wadaiwa, Ismail Jussa Ladhu, Mwenyekiti wa ZIMCO, na Ali Mohammed Ali (Nabwa), Mhariri

Mtendaji wa Dira, walifika mahkamani, lakini wadai hawakuonekana licha ya kutafutwa sehemu zote na karani wa mahkama.

Hata wakili wao, Fatma Amani Karume, ambaye anawakilisha Kampuni ya

Mawakili ya Mkono & Co. (Advocates) ya Dar es Salaam naye hakuonekana.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Dahoma aliakhirisha kesi hiyo hadi Febuari 27 kwa kutajwa.

Alipoulizwa kwa nini

Inaendelea katika Habari za Kitaifa

Top

Wazanzibari waja juu kuhusu uchimbaji mafuta

Na Mwandishi Mkuu wa Dira

Habari zilizochapishwa katika toleo lililopita la Dira chini ya kichwa cha maneno “Awamu ya Sita yaridhia Serikali ya Muungano kuchimba mafuta Zanzibar” zimepokewa kwa hasira kubwa na wananchi wengi wa visiwa hivi.

Katika mazungumzo na Mwandishi Mkuu wa Dira, Amour Said, maarufu kwa jina la ‘Milo’, mkaazi wa Weles, Zanzibar, alisema haoni sababu yoyote ya msingi ya mafuta kuchimbwa na Serikali ya Muungano wa Tanzania.

“Mbona madini yanayopatikana Bara hayakuingizwa katika masuala

ya Muungano?” aliuliza. “Sasa wanataka wavamie mali yetu, iwe ya Muungano.”

Aliendelea kusema, “Tunasikitika sana kumuona Mheshimiwa Burhan Saadat ambaye ni Mwakilishi wetu akikubali kudhalilishwa wakati wizara yake ndiyo ilipaswa kushughulika na

Comments are closed.