Eid Mubarak kwa Waislam Wote.
Na. B.OLE,
Assallam Alleikum,
Nawatakia Wanamzalendo Eid Mubarak na Waislam wote popote pale mulipo. Leo ni siku tukufu na adhimu ni wajibu wetu kusameheana na kuombeana Maafra kwa M/Mungu ili atutakabalie funga zetu na sadaka zetu zote.
Mwezi huu mtukufu umeshapita licha ya kufurahia lakini hatuna budi kuwa na masikitiko kwani hatuna uhakika kwamba tutafika Ramadhani nyengine . Tumuomba Mola atufikishe ili tuweze kuifunga tena hapo mwakani tukiwa wazima na buheri wa Afya.
Tumejifunza mengi katika mwezi huu mtukufu ni vyema kwa yote tuliojifunza kuyaendeleza ili iwe ndio dira yetu katika maisha yetu ya kila siku.
Mola atujaze mapenzi miongoni mwetu, tuishi kwa kupendana, kuhurumiana na kushirikiana katika mambo mema ili iwe njia ya kheri kesho mbele ya haki.
Kwani mwisho wa yote tunayofanya tutarejea kwake hatuna budi kujitayarisha kwa safari hii ndefu yenye mikiki ndani yake ikiwa tutapuuza yale tulioamrishwa na subbuhanah Wataala.
Inshallah Mola wetu tujaalie tuwe ni wasikivu, utujaze mapenzi juu yako na tufuate yale yote ambayo umetuamrisha kwa utukufu wako uliotukuka, sisi niwaja wako dhaifu, tunanyenyekea juu ya ufalme wako.
Kwa uwezo wako tujaalie hatma njema, utusamehe madhambi yetu pamoja na vizazi vyetu kwani sisi ni wenye kukosea na wewe ndie tunae kuomba toba.
AMEEN AMEEN AMEEN
EID MUBARAK.





