Habari

Francis Mutungi ndio mtatuzi wa mgogoro wa CUF

Leo nimeangaza njia za kutatua mgogoro ndani ya Chama cha Wananchi CUF. Kawaida huwezi kutatua tatizo bila ya kujuwa chanzo chake.

Asili ya mgogoro wa CUF ilianzia pale aliyekuwa Mwenyekiti wake Ibrahim Lipumba kutaka kurudi kwenye uongozi baada ya kujiuzulu nafasi yake. Ilichukuwa takriban miezi 8 akiwa nje ya utendaji wa chama alipokuja na wazo la kubadili uamuzi wake. Hadi hapo hapana kosa wala ubaya.

Ubaya ulianzia pale alipovamia mkutano mkuu ambacho ndio kikao kikuu cha chama, na wakati yeye hakuwa Mjumbe wala hahusiki nanacho. Hili ndio kosa la kwanza, kuwazuwia wanachama kufanya maamuzi na muelekeo wa chama chao kisha kuwajengea khofu, kuleta vurugu, uharibifu nk. Hapa ilistahiki vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

Muda wote huo Lipumba alikuwa anajitambua kuwa sio Mwenyekiti wa CUF. Msumari wa mgogoro uligongomewa na Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, kwa sababu anazozijuwa, alipompa Lipumba mamlaka. Akitupilia mbali hoja kwamba Lipumba amejiuzulu, mkutano mkuu umeridhia kujiuzulu kwake, na Baraza Kuu lishafuta uwanachama wake.

Lakushangaza kwenye website ya Ofisi ya Msajili wanamtambua Lipumba kama Kaimu Mwenyekiti. Cheo hicho kimeanza lini, kwa katiba gani na lini kitasita. Haya ni baadhi tu ya maswali niliyojiuliza. Wewe msomaji unaweza kuongeza.

Hapo ndio nilopohukumu kuwa utatuzi wa mgogoro huu uko chini ya mamlaka Msajili wa Vyama. Ingawa katika majukumu yao hawakulisema hili, lakini ni kwa vile Msajili ndio chapuo yake.

Ofisi ya Msajili inasema inashughulika na kazi za: kusajili vyama vya siasa, kugawa ruzuku kwa vyama, kufuatilia mapato na matumizi ya vyama, kusimamia utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa pamoja na kuwa secretariats ya Baraza la vyama vya siasa. Hivyo utatuzi wa mgogoro umo mikononi mwao.

Naomba kwa pamoja tushirikiane tumtake Jaji Francis Mutungi kuweka sawa pale alipokosea/alipokusudia juu ya mgogoro wa CUF. Laiti ingekuwa si kujichomeka yasinge fikia haya. Hivyo tumtake ajichomoe kwa kufuta yale maelekezo yake yaliyochochea.

Kwa mujibu ya website Lipumba na Kaimu Mwenyekiti, kukamatwa nafasi kuna muda wake, Lipumba hana viongozi kutoka Zanzibar, wote wamefukuzwa uanachama. Na yoyote atakeyemteuwa atafukuzwa uanachama, hivyo ataishia wapi?

Msajili turudishie nidhamu ya chama chetu

Share: