Magharibi yaichapa Mara 2-1, TMK, Pemba Kusini leo
Doris Maliyaga
TIMU ya Mjini Magharibi imefanikiwa kusonga mbele kwa nusu fainali ya michuano ya vijana ya U-17 Copa Coca Cola, baada ya kuichapa Mara kwa mabao 2-1 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mabingwa hao watetezi walipata bao la kwanza dakika ya 10, lililofungwa na Ally Mohamed kwa shuti baada ya kupokea pasi nzuri ya Rashidi Rashid kufanya matokeo kuwa 1-0 hadi mapumziko.
Mara waliamka kipindi cha pili na kupata bao la kusawazisha dakika 60, lililofungwa na William Wambura aliyempiga chenga kipa, kabla ya Mohamed kufunga bao lake la pili kwa Mjini Magharibi zikiwa zimebakia dakika tatu kufanya matokeo kuwa 2-1.
Mechi ya mwisho ya robo fainali itachezwa leo kwa kuzikutanisha timu ya Mkoa wa Temeke na Kusini Pemba mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru.
Temeke inakutana na Kusini Pemba katika hatua hiyo baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa kundi D ambapo Kusini Pemba alikuwa mshindi wa pili wa kundi C.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wa kuvutia kutokana na matokeo ya awali ya timu zote ambapo tangu kuanza kwa michuano hiyo Kinondoni ilipoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Kilimanjaro ambapo Kusini Pemba alisuluhu mechi moja tu na Morogoro na hakupoteza kati ya sita waliyocheza kwenye hatua ya makundi.
Ambapo timu za Kinondoni iliyoitoa Mbeya na Kigoma iliyowaondoa Morogoro kabla ya mechi za jana zimeshatinga nusu fainali ambapo Kinondoni atacheza na mshindi wa mechi ya jana, kesho na Kigoma atacheza na mshindi wa mchezo wa leo, keshokutwa.
Akiuzungumzia mchezo huo kocha mkuu wa Kusini Pemba Fatawi Sheha alisema, wamejiandaa vizuri na watafanya vizuri kwenye mchezo wa leo: ”Tumejiandaa vizuri na tunaamini sisi ndiyo tuatakwenda nusu fainali.”





One Comment on "Magharibi yaichapa Mara 2-1, TMK, Pemba Kusini leo"
Wazalendo haya mambo vipi?
Lakini kwanza nawapa hongera vijanawetu kwa kuwatwanga wapinzani wao. Musirudi nyuma wembe ni uleule kulitetea taji kwa mara nyengine.
Nirudi kwenye point yangu, haya mashindano nakumbuka zamani yalikuwa yakiitwa “Mkoa kwa Mkoa” na yalikuwa yakishirikisha jumla ya mikoa 20 ya Tanganyika. Leo naona hata Mjini Magharibi, Kusini Pemba, .. kulikoni. Ilihusu nini kwenda kushiriki mikoa ya Zanzibar kwenye masindani ya mikoa ya Tanganyika.
Sh Tamim Ferej hapa umekwenda mchomo. Ndio yale ya ng’ombe kujipinza kisha akataka kujipinzua. Ikiwa nyinyi munataka mutambuliwe na chama chenu, vipi mushiriki katika mashindano kama haya.
Hebu ZFA kuweni na msimamo, tusiwe legelege. Tunachohitaji ni kuiona Zanzibar inashiriki katika mashindano ya kimataifa kama vile Wales, N. Ireland, nk zinavyoshiriki, na sio kwenye mashindano ya mikoa.
Sh Tamim Ferej, naona bora uwaachie vijana hiyo nafasi kwani tayari kushafikia saturation point. Tunahitaji muelekea na msimamo mpya.