Michezo

Michuano ya Mpira wa Rede Zenj.

michezo
Monday, December 2, 2013
Michuano ya Mpira wa Rede Zenj.

Na Mwanajuma Juma.

MICHUANO ya mpira wa rede yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa UVCCM jimbo la Rahaleo ilianza juzi rasmi kwa miamba mine kushuka katika kiwanja cha Komba Wapya mjini Unguja.

Miamba hiyo ambayo ilishuka kwa nyakati tofauti ilitanguliwa na mchezo kati ya timu ya Jimbo la Rahaleo A na Kwamtipura mchezo ambao ulimalizika kwa timu ya jimbo la Rahaleo A kushinda mabao 11-6.

Mchezo mwengine uliochezwa kwa siku hiyo ulikuwa ni kati ya timu ya Jimbo la Kikwajuni na Mpendae na kushuhudiwa Kikwajuni kushinda kwa mabao 30-16.
Katika mchezo huo ambao ulivuta hisia za watazamaji wengi Kikwajuni iliyokuwa ikimtumia mchezaji wake Tauhida Abdalla ‘Kirukuu’ ambae aliingiza magoli tisa pekee kati ya 30.

Jumla ya timu 11 zinashiriki michuano hiyo ambayo ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Michuano ya Mpira wa Rede Zenj.

Share: