Mjini Magharibi yafanya kweli Copa Co-Cola
Mohamed Akida
MABINGWA wa tetezi wa michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Copa Coka-Cola, Mjini Magharibi jana imeifunga Kagerza, mabao 5-1 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, ilishuhudiwa Mjini Magharibi ikienda mapunziko ikiwa inaongoza kwa mabao 3-0, yaliofungwa dakika za mwanzoni mwanzoni.
Mchezaji Ally Khalifan aliifungia, Mjini Magharibi bao la kwanza dakika ya 16, kabla ya Rashid Rashid kupachika la pili dakika ya 20 kwa shuti lililomshinda kipa wa Kagera, David Mshukanabo.
Mjini Magharibi waliendelea kuliskama lango la wapinzani wao na dakika ya 28, iliandika bao la tatu kwa penati na Marithi Haji, baada ya Omari Abadalaah kuangushwa ndani ya eneo la hatari na Richard Modesti.
Kipindi cha pili kilianza kwa Mjini Magharibi, kuliskama lango la Kagerza na dakika ya 58, Munasabu Hija alifunga bao la nne na kuongeza la tano dakika ya 62, kupitia kwa Mudathiri Yahya.
Kagera ililazimika kucheza pungufu baada ya winga wake Oscar Amosi, kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 66 lakini ilipata bao la kufutia machozi dakika ya 79 lililofungwa na Abdulrazaki Bakari.
Katika mchezo mwingine uliofanyika Uwanja wa Uhuru timu ya Mkoa wa Mwanza ilitoka sare ya 1-1 na Kigoma wakati katika Uwanja wa TAMCO, Kibaha Mara iliifunga Tabora mabao 3-0 huku Morogoro ikiisambaratisha Shinyanga mabao 3-1.




