Zanzibar yatumaini uanachama Fifa

Written by  //  04/09/2010  //  Michezo  //  3 Comments

Mwandishi Wetu
Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), kimesema kuna matumaini makubwa ya kuwa mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutokana na majibu ambayo ujumbe uliofuatilia suala hilo umeyapata.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Katibu Mwenezi wa chama hicho, Maulid Hamas Maulid alisema ujumbe ulioenda Zurich, Uswisi kukutana na Rais wa Fifa, Sepp Blatter umepata majibu mazuri.

“Ile ndoto yetu ya muda mrefu ya kutaka tuwe wanachama wa Fifa sasa inakuwa kweli na muda si mrefu mambo yatakuwa mazuri.

“Nimewasiliana na wenzetu walioenda kukutana na viongozi wa Fifa na kwa kweli kazi imefanyika na tunawashukuru wote kwa hatua waliyofikia,” alisema Maulid.

Akifafanua hilo, Maulid alisema Blatter ameafikiana na ombi la Zanzibar kuwa mwanachama Fifa na kuwa sasa jukumu hilo amemuachia Mkurugenzi wa Uanachama wa Fifa Thierry Regenass ashughulikie jambo hilo.

“Mkurugenzi huyu wa Uanachama kwa sasa ndiye anashughulikia jambo letu kwa maana unaweza kusema tumeanza mchakato wa kuwa mwanachama wa Fifa.

3 Comments on "Zanzibar yatumaini uanachama Fifa"

  1. butiama 04/09/2010 kwa 2:16 um ·

    GOOD NEWS

  2. zamko 04/09/2010 kwa 2:43 um ·

    habari siombaya kabisa, lakini huu utakua ni ukweli? au hao akina Shamuhuna wameondolewa njiani tu. Maana viongozi wengi wa CCM SMZ ni majuha kalulu wapo tuuuuu.

    Kama itakua kweli basi huu utakua mwanzo wa kulitangaza Taifa letu la Zanzibar. Kwani michezo ndio inayotangaza nchi fulani na identity yake. Lakini tusiwasahau hawa vidudu mtu, ambao tunawaganya ndio ndugu zetu (Tanganyika TFA)watawaachia wazanzibari wajitangaazie utaifa wao ?

  3. jamaleyl 04/09/2010 kwa 6:20 um ·

    Sasa kwa mara ya kwanza tunapata kauli rasmi kuwa ZFA imepeleka maombi yake ya uanachama FIFA.Kama nilivyouliza nyuma kuwa jee kile alichosema mwakilishi wa FIFA kanda ya kusini ya Afrika A. Mamelodi ni kauli ya FIFA au ametumiwa na wenzetu ili kutuvunja moyo tusipeleke maombi hayo?Nafikiri majibu nyote mshayapata hakuna haja kuyarejea.Kinachoonekana hapa ni kuwa kimsingi FIFA inaweza kuyafikiria maombi yetu ya uanachama na hiyo ni hatua ya mwanzo ambayo wapenda michezo wote hasa wa mpira wa miguu tunapaswa kuifurahikia.Hata hivyo safari iliyoko mbele yetu ni ndefu kwani siyo Blatter mwenye kutoa uanachama.Yeye alichofanya ni kubariki maombi yetu ambayo yanaweza kukubalika au kukataliwa na vikao vinavyohusika vya FIFA.Kwani maombi hayo lazima yapitie kamati ya utendaji ya FIFA kabla hayajapelekwa kwenye Congress ya FIFA na kote huko kutakuwa na vikwazo vyake ambavyo serikali ya SMZ pamoja na ZFA wajitayarishe kukabiliana navyo, siyo wajibweteke na kufikiri kuwa maombi hayo yatapita kirahisi.Hata yakishindikana huo siyo mwisho wa safari kwani tuna haki ya kupeleka malalamiko yetu Court of Sports Arbitration ambayo inatambulika na FIFA.Kama nilivyosema huko nyuma na narudia hapa kuwa haki ya kuwa wanachama kama nchi tunayo kinachotakiwa ni kujua wapi na nini cha kufanya katika kufikia lengo hilo.

Comments are now closed for this article.