Maalim Seif Salim Akumbukwe

Written by  //  22/07/2010  //  Burudani  //  7 Comments

Wazalendo nachukua nafasi kuwakumbusha mchango wa msanii wetu maarufu Maalim Seif Salim.

Miaka kadhaa katika uhai wake alikuwa mstari wa mbele kuhimiza jamii ya Kizanzibar kujiletea umoja na mshikamano. Hivyo katika wakati huu ambapo Wazanzibar wamo kwenye shamrashamra za kuelekea kwenye kupiga kura ya maoni, nimeonelea ipo haja ya kuyakumbuka maneno ya Maalim Seif aliyoyatoa kwenye nyimbo yake hii.

Endelea na usikilizaji

 

7 Comments on "Maalim Seif Salim Akumbukwe"

  1. Taaban bin Hoi 22/07/2010 kwa 1:53 um ·

    @ashakh

    Hilo jina lako na hayo mambo unayoyaweka hayaendani kabsaa.

  2. Junius 22/07/2010 kwa 2:08 um ·

    @ashakh
    Mimi nakuunga mkono, personally nimekuwa ni mutribu wa taarab na mshabiki wa Naad Ikhwan Safaa bali pia ni mpenzi mno wa nyimbo za Almarhum Saif Salim Saleh,ni mashairi yanayoburudisha,yanayoelimisha na kuhamasisha. Ukiusikiliza wimbo huo utakuta jinsi gani Mzalendo huyu kupitia sanaa anavyoiombea nchi amani, mapenzi na maendeleo. Tukubali kuwa utamaduni ni sehemu ya maisha ya watu ambao hauwezi kutengwa kwa tofauti za kiimani au mitazamo yake.

    Ndg.ashakh, kama una wimbo mwengine unaofanana na huo tuletee hapa tuburidike, binafi nikisikiliza nyimbo za tarab asil, zinanikumbusha mengi ya nchi yetu.
    J

  3. Heart 22/07/2010 kwa 6:28 um ·

    Hii nyimbo ndio wakati wake haswa inafaa kuenziwa

  4. misali 23/07/2010 kwa 3:31 mu ·

    vijana kila aliye fanya mambo mazuri hukumbukwa kwa alichokifanywa ikiwa kizuri humsaidiya huko alipo na ikiwa kibaya hatutakiwi kumtangazia ubaya aliyoufanya samahanini sijafahamu namna ya kumkumbuka tufanyeni nini tuimbe njibo zake ,tufanye rusha roho,tumuombe dua,tuchangishane pesa zitakazo patikana tumjengee chuo,au tumchimbiye kisima ili nayey afarijike huko alipo hamjafafanua nasema hivi kwasababu mzee wangu ameacha nyimbo nyigi kwenye ulimwengu huu ambapo yeye kishatanguliya mbele ya haki hazitomsaidiya wazee wanasikitika huwa na majonzi

  5. swaglish 23/07/2010 kwa 8:19 mu ·

    @misali we unajijuwa wa wapi peponi au motoni?
    usimuhukumu mtu hayo ni mambo ya mungu yeye ndio anaee juwa sawa,,,sio lazima mtu kupenda nyimbo kuna wengine wanapenda mashairi yaloimbwa, mashairi hayakukatazwa ikiwa ni mazuri sawa
    maasalam

  6. mrfroasty 23/07/2010 kwa 8:43 mu ·

    Info:
    Jinsi ya kueka muziki katika MZALENDO.

    [podcast]http://kiungo_cha_mp3[/podcast]

    Kwa maana replace “http://kiungo_cha_mp3″ na kiungo cha kweli cha mp3 unayotaka kuichapa kwenye chapisho.

    Maasalaam,
    mrfroasty

  7. misali 23/07/2010 kwa 8:02 um ·

    kijana swaglish yaelekeya hujanifahamu mimi sijakwambiya masuala ya peponi na motoni isitoshe huyo unayemtaja mimi ni mzee wangu kwahiyo mimi naona uchungu wala sioni fahari laiti agelikuwa anasoma quran au athana ndizo zigelimsaidiya huko aliku kijana hayo unayosema yaelekeya umepitiliwa utotoni unaupungufu wa iman na ukosefu wa kuijuwa dini yako na kama una mapenzi naye ya kweli siyo unafik na kutaka sifa muuombee dua mtolee sadaka SWAGLISH Tafadhali isome dini yako uodokewe na ujinda kwani itakusaidiya kuishi kwenye aman na uwache kurukiya mambo usiyoyajuwa uzito wake yatakuweka pabaya MUUGU ATAUHIFADHI KWA SOTE TUSIFANYE MZAHA KWENYE IMAN JAMANI KWAKILA NILIYEMUUDHI NAOMBA KUMRADHI

Comments are now closed for this article.