Mjuwe aduwi wako na sifa zake.

Written by  //  26/04/2010  //  Mashairi  //  1 Comment

MJUWE ADUI YAKO

KIFUATACHO NI KITAMBULISHO CHAKE

JINA
Ibilisi

MJI
Ndani ya nyoyo za walioghafilika

KABILA
Mashetani

MWISHO WAKE
Ndani ya moto wa Jahannam

CHEO
Muovu wa hali ya juu

SEHEMU ANAZOZIPENDA
Pasipotamkwa jina la Mwenyezi Mungu

NJIA YAKE
Isiyonyoka

RASILMALI YAKE
Tumaini

BARAZA ZAKE
Masokoni

MAADUI ZAKE
Waislamu

ANACHOPENDA
Unafiki

NGUO ZAKE
Mfano wa kinyonga – kila mahali na rangi yake

WAKE ZAKE DUNIANI
Wanaokwenda uchi huku wakiwa wamevaa

ANAOWAPENDA
Walioghafilika na kumtaja Mwenyezi Mungu

ASOWAPENDA
Wenye kuomba maghfira

NYUMBA YAKE
Vyooni na sehemu chafu

SIFA ZAKE
Hana msimamo maalum

TAREHE YA KUANZA KAZI
Siku aliyokataa kumsujudia baba yetu Adam (AS)

MARAFIKI ZAKE
Wanafiki

MSHAHARA WAKE
Mali ya haramu

OFISI ZAKE
Mwahali anapoasiwa Mwenyezi Mungu

SHUGHULI ZAKE
Anaamrisha maovu na anakataza mema

DINI YAKE
Kafiri

WADHIFA WAKE
Mkurugenzi mkuu wa walioghadhibikiwa na waliopotoka

MUDA WAKE WA KAZI
Mpaka siku na wakati maalum

NJIA YAKE
Inayoelekea motoni

WANAOSAFIRI NAYE
Mashetani miongoni mwa majini na binadamu

MFANZA KAZI ANAYEMPENDA
Mwenye kuinyamazia haki

NJIA ZA KUWASILIANA
Kusengenya – kupelelezana – kufitinisha

CHAKULA ANACHOKIPENDA
Kula nayama za maiti (kusengenya)

ANAWAOGOPA
WachaMungu

ANAWACHUKIA
Wanaomtaja sana Mwenyezi Mungu

MITEGO YAKE
Wanawake, watoto, na mali

MATAMANIO YAKE
Kuwakufurisha watu wote

NENO ANALOLIPENDA
‘Mimi’

SAUTI ANAZOZIPENDA
Za waimbaji wanaume kwa wanawake

WAADI WAKE
Anakuahidini ufakiri

KINACHOMLIZA
Kumsujudia Mwenyezi Mungu

One Comment on "Mjuwe aduwi wako na sifa zake."

  1. al saleh 26/04/2010 kwa 4:15 um ·

    asalam alikum jamani naomba mnisaidie huyu adui ni IBILSI au ninani?

Comments are now closed for this article.