NAKUAGA RAMADHANI
1. Sina budi kukuaga Karimu wetu mgeni
Nyoyo wazitoa woga Hata khofu hatuoni
Kwa madhambi kujitenga Heshima yako Fulani
2. Unakuja na mapenzi Mjo wako una kheri
Thalathini siku hizi Zino neema kathiri
Na nyoyo huwa ziwazi Na roho zina nawiri
3. Wewe bwana wa baraka Wewe kinga ya maasi
Wewe Mola kakuweka Utukinge sisi nasi
Wewe kesho kiondoka Mambo hayawi mepesi
4. Ewe bwana Ramadhani Kutuaga budi huna
Kwa amri ya Rahmani Si haba tumekutana
Jee ? ifikapo mwakani Habiby tutaonana ?
5. Wakati ukiwadiya Karibu na kuondoka
Nyoyo giza huingiya Na nuru inatoweka
Hukumbuka mazoweya Na pendo unotuvika
6. Hatuna budi kuliya Machozi kutumwaika
Kwa vile utapoteya Kwa miezi kadhalika
Hapo utaporejeya Mpaka mwaka ukifika
7. Kwa kheri wetu azizi Kwa kheri ya kuonana
Wewe bora ya mlezi Mfano wako hakuna
Yako matamu mpenzi Yajayo machungu sana
8. Kesho siku ya hesabu Ubavuni utasimama
Jawabu wewe tajibu Ya haki utayasema
Tukifanya ya wajibu Aloyataka Karima
9. Mmoja wa waokozi Nasi twakutegemeya
Tuliziona upuuzi Anasa za hii duniya
Kuwa wetu muelezi Mola anakusikiya
10. Buriyani Ramadhani Inshaalla tutaonana
Iwapo si duniyani Akhera tutakutana
Wallahi una imani Na baraka nyingi sana.
Nakutakieni kila la kheri Eid hii naa aila zenu.na jamaa zenu
Eid Mubarak



