Nchi yetu rudisheni, msitupige binduki
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 05/01/2010 // Mashairi // 2 Comments
Twataka amani, bila risasi…
Tukiwapa nafasi, mwatengeneza bunduki…
Tukiwapa ishirini, mwataka mamilioni…
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki
aliye na akili, hauzi yake nchi
aliye jasiri, hatishiki kirahisi
aliye na kasi, huepuka risasi
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki
asiye na mali, ni Mola hamumwamini
asiye na kazi, masaa hayampiti
asiye na jirani, ya ulimwengu ni ubishi
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki
shida mitaani, twatafuta riziki
shida nchini, wenzetu wana chuki
Shida serikalini, ubaguzi hamuachi
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki
Twataka amani, bila risasi…
Mamboleo ukoloni, leo hauna nafasi
Tukiwapa nafasi, mwatengeneza bunduki…
Leo twasema:
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki
Wenzetu tuliwadhani, kumbe mu-nyoka mioyoni..
Ndugu zetu tulidhani, kumbe weusi wakoloni…
(Hivi kweli) Bila risasi, haiwezi kuwa amani?
Sasa twasema,
Nchi yetu rudisheni, msitupige bunduki
Chanzo:zanzinet




2 Comments on "Nchi yetu rudisheni, msitupige binduki"
hengera…longa mwanangu longa.
TURUDISHIENI NCHI YETU YENYE MILA NA DESTURI ZAKE NAYO NI ZANZIBAR :MFUMBAVU MMOJA ALIWAHI KUTAMKA YA KWAMBA UZANZIBARI NI UDINI. KWA WALE WAZANZIBARI HII NI FAHARI YETU KWANI NDIO MILA YETU
N:B
Admin ameondosha makala refu-imetokeza hapa