Uzuri wa kitu kwa nje si usalama wa ndani
Written by nnyamwakaleli // 17/03/2010 // Mashairi // 2 Comments
Papai jama papai, lanipendeza machoni,
Kwa yake rangi papai, halinitoki usoni,
Hata nikifunga tai, nalisogeza mdomoni.
Nikilikata papai, kumbe lishaaoza ndani
Ukiliona ni zuri, machoni linavutia,
Ni kwa yake rangi nzuri, mikononi ukilitia,
Njano na kijani nzuri, na umbole vyavutia,
Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani
Yapo mapapai mengi, kwa zake rangi tofauti,
Na mitaani kwa wingi, na hayahitaji suti,
Pia sokoni ni mengi, tena hayana masharti,
Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani.
Ni mazuri sana kwa nje, shida yake kule ndani,
Ukiyaona yalivyo nje, huna swali na ndani,
Yanavutia sana nje, yanachefua kwa ndani,
Nikilikata papai, kumbe lishaoza ndani




2 Comments on "Uzuri wa kitu kwa nje si usalama wa ndani"
shukrun kwa utenzi wako wa papai . kwavile mimi siomzuri wakuleta au kufahamu haraka kwenye huu utenzi wa papai . lakini najuwa umelenda kitu lakini hata hivyo papai kweli lavutiya machoni .hahahaha hongera mr papai
ahsante sana ndugu yangu, tuko pamoja, lengo ni kuelimishana juu ya mambo yetu ya kitanzania katika ligha yetu hii adhimu ya kiswahili, na misemo yetu ile ya … si kila king’aacho ni dhahabu