Chuki kwa wageni yafukuta Afrika Kusini

Written by  //  21/07/2010  //  Kimataifa  //  1 Comment

Jeshi lasaidia kuondoa Xenphobia

Jeshi la Afrika Kusini limeungana na polisi, kulinda doria mjini Johannesburg kutokana na mashambulio ya chuki dhidi ya raia wa kigeni yaliyosababisha watu saba kujeruhiwa vibaya.

Miongoni mwa waliojeruhiwa ni wahamiaji kutoka Zimbabwe na Msumbiji, pamoja na waafrika weusi wa Afrika Kusini waliojikuta katika mashambulio hayo jana usiku.

Katika barua kwa Rais Jacob Zuma, mkuu wa chama cha Democratic Alliance upande wa Western Cape, Hellen Zille alibaisha chimbuko la chuki dhidi ya wahamiaji weusi au Xenophobia. Hata hivyo hofu yake ilipuuzwa na mkuu wa polisi kama iliyokosa msingi.

Lakini sasa hivi imebainika wazi kuwa wageni kutoka Zimbabwe, Msumbiji, Malawi na Nigeria, miongoni mwa nchi nyingine, wanakabiliwa na hatari ya kushambuliwa wakati wowote.

Tangu mashindano ya Kombe la Dunia kumalizika nchini Afrika Kusini, wageni wasiopungua 10 wameuawa na watu weusi wa Afrika Kusini katika sehemu ya Cape Town na hatari hiyo imeanza kuenea katika miji mingine.

Mkuu wa Polisi, Mbeki T’wele, ameahidi kuongeza idadi ya polisi wa kushika doria mitaani, kuimarisha usalama.

BBC.CO.UK/SWAHILI 21st JULY, 2010

One Comment on "Chuki kwa wageni yafukuta Afrika Kusini"

  1. Heart 21/07/2010 kwa 4:19 um ·

    Habari hizi zinatishia amani na maisha ya ndugu zetu walio kule Afrika kusini. lakini pia habari hii sio ngeni miongoni mwetu, ilishatokea miaka mitatu liyopita na nikawaida yao sasa.
    hata hivyo serikali ya Afrika kusini ni wajibu wao kulinda wageni na raia wao waliopo kule Africa kusini ili kutunza amani na ushirikianao miongoni mwa nchi za afrika na kwengine kote duniani pamoja na jumuiya zake.

    Habari hii ni changamoto kwetu wanajamii popote pale ulipo kwani matendo haya hayapo kule afrika kusini tu, bali takriban duniani kote. Haya yanasababishwa na vyanzo mbali mbali vikiwemo ubaguzi ambayo ndio yawezekana ikawa chanzo kikuu,ugonvi wa kawaida wa kutofahamiana tu na manufaa ya maisha. Kwa ujumla ni sababu za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

    wazalendo tuipambe nchi yatu kwa kuimarisha misingi ya kupendana na kuheshimiana ili nasi tujivunie maendelea tutakayoyapata.Ni wajibu wa kila alie mbali ya nchi yake kutambua ukweli huu.Tusijisahau tukafikiri ndio tumefika katika nchi za watu, hata hivyo naamini tutaendelea kujiimarisha nyumbani kwani siasa zetu zina muelekeo mzuri.

    Haya viongozi wetu mmejiandaa vipi katika hili?

    nawasilisha

Comments are now closed for this article.