Gordon Brown atubu kwa niaba ya Uingereza
Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown anatarajiwa kuomba msamaha rasmi kwa namna Uingereza ilivyo warejesha watoto zaidi ya laki moja katika koloni zao za zamani.
Hatua hiyo ya Uingereza ilichukuliwa chini ya mpango wenye utata wa kuwarejesha makwao wahamiaji miaka arobaini iliyopita.
Watoto wengi walichukuliwa kutoka kwa familia zao kwa nguvu na kupelekwa nchini Australia, Canada na nchi nyingine za Jumuiya ya madola.
Inasemekana badala ya watoto hao kupata maisha bora, waliteswa kwenye makao ya kuwatunza na walilazimishwa kufanya kazi ngumu kwenye mashamba.
Waathiriwa sitini wamerejea mjini London kushuhudia Waziri Mkuu Brown akiomba msamaha huo.
Mwezi Novemba mwaka jana, Waziri Mkuu wa Australia, Kevin Rudd, pia aliomba msamaha kwa waathiriwa hao waliojulikana kama raia wa Australia waliosahaulika.




