Kampeni za uchaguzi nchini uholanzi (wale makaburu wa afrika

Written by  //  07/06/2010  //  Kimataifa  //  2 Comments

Mchakato mzima wa uchaguzi nchini uholanzi hivi ndio unavyokwenda.Hapo kwa wale wasiofahamu lugha nitajaribu kutoa madondoo mawili matatu ya sera za mwana siasa aliepo pichani.

Mchoro 1.
“Meer Veiligheid, Minder Immigratie” yaani Usalama zaidi, punguzo la wageni.

Mchoro 2.
#Nederlands velig yaani Uholanzi ilio salama, PVV (chama cha siasa hicho) kinasema kitasafisha safisha kila kitu na kufukuza na kuhamisha materorist (kwa maana ya waislamu) na wahalifu wote kutoka nchini uholanzi.

#Minder immigratie yaani punguzo la wageni, ongezeko la wageni litatugharimu fedha nyingi mabilioni ya Euros.

#Stop de islamisering
Zuia uislamu unatuletea vilemba na vishungi na maninja tuu…uhalifu jihad etc.

[singlepic id=238 w=320 h=240 float=]
[singlepic id=237 w=320 h=240 float=]

Anyways translation kutoka lugha moja kwenda nyengine ni ngumu, lakini nilitaka nikuachieni vidokezo vya kampeni za uholanzi na ukarimu tunaokaribisha wazungu na kunyenyekea watu hawa.Ukiwa nchini mwao ndio utapata kuwafahamu vizuri.

Mara ya mwisho nilikuwa natoa pesa hapo Darajani kwenye ATM, wallahi niliona machungu kuna waafrika tele tumejipanga.Lakini alipokuja mzungu, basi wale Janjaweed (JKU excusee mwa) walimkaribisha mzungu tuu…sie waafrika alituona hatuna maana!

Ni hayo tuu kwa leo, hili ni somo kubwa kwa wazanzibari wanaofakamia wazungu.!

Maasalaam,
mrfroasty

2 Comments on "Kampeni za uchaguzi nchini uholanzi (wale makaburu wa afrika"

  1. mstahamilivu ismail 08/06/2010 kwa 9:02 mu ·

    Assallam Allaykum jamia ?
    ALLAH Hasemi uongo pale
    alipotuambia msiwafanye hao makafiri kua rafiki zenu wa karibu,kwani yy ni mjuzi zaid tusioyajua sisi. cha kushangaa leo sisi ndio tumefanya kimbilio letu kwao eti tunaaona watu wema,imefikia watu kuuza DINI yo kwa kutaka PASSPORt. lakini inshaallah atuoneshe zaid ili tupate kuzinduka; AMEEN.
    Mstahamilivu.

  2. mrfroasty 12/06/2010 kwa 3:38 um ·

    Unajua hii story inaendelea, mara ya mwanzo nilipokea posta hii kwenye sanduku la barua.Nilishangaa, lakini nikaona haya tuu.Mshangao wangu ni kuwa kwenye sanduku langu nimeweka stika maalum kukataza kuwa sitaki matangazo ya aina yoyote.

    Sasa majuzi baada ya posta ya mwanzo, nimeikuta nyengine mdachi kanitilia kwenye sanduku langu.Nikakasirika nikaitupa chini karibu na sanduku hilo….Leo nimeikuta tena mwananchi kaichukua kaitia tena kwenye sanduku langu!

    Kumbe hata hawa majirani nacheka nao kijicho upande, wanasoma jina langu kwenye sanduku la barua na inaonesha wana mengi rohoni mbali na tabasam wanaloniekea.

    Anyways, hiyo ndio hali….mjiti na macho.

Comments are now closed for this article.