Mahakama za Kiislamu Kenya ‘batili’
Written by administrator // 24/05/2010 // Kimataifa // 1 Comment
Jopo la majaji limeamua kwamba, kuwepo kwa mahakama za kiislamu nchini Kenya ni kinyume cha sheria na inaleta ubaguzi.
Majaji hao watatu wamesema mahakma hizo maarufu kama “mahakama za Kadhi” zimeipendelea Uislamu zaidi ya imani nyingine, na kwamba ilikuwa kinyume na katiba kwa kuwa Kenya ni nchi isiyotawaliwa katika misingi ya kidini.
Mahakama za kiislamu zimezua ubishani mzito katika katiba mpya iliyopendekezwa nchini humo.
Katiba hiyo inatarajiwa kupigiwa kura ya maoni mwezi Agosti mwaka huu.
Mahakama za Kadhi- zilizoanzishwa wakati wa utawala wa kikoloni wa Mwingereza – aghlabu hushughulikia masuala ya ndoa na urithi kwa Waislamu wachache waishio Kenya.
Makanisa nchini Kenya yalifikisha malalamiko yao kuhusu suala hilo mahakamani miaka sita iliyopita.
Kama sehemu ya makubaliano ya kugawana madaraka ili kumaliza mgogoro kufuatia uchaguzi wa mwezi Desemba 2007, ilikubalika kuandikwa kwa katiba mpya.
Chanzo:bbc




One Comment on "Mahakama za Kiislamu Kenya ‘batili’"
HAYA YOTE WAMEYATAKA HAO AKINA SHEIKH MOHAMMED SHAMTE, SEHEMU YA PWANI ILIKUWA NI SEHEMU YA MAMLAKA YA SULTAN WA ZANZIBAR LAKINI KWA UPOFU WAO WAKAZUGWA NA MALKIA WA UENGEREZA WAKAIWACHIA BURE. WAMEWAACHIYA KWA MKATABA TENA MKATABA WENYEWE WA KUANDIKIANA BARUA.
KWA KWELI TUKIRI KUWA ZANZIBAR IMEANZA KUULIWA ZAMANI TANGU ENZI ZA HAO MOHAMMED SHAMTE NA JEMSHID, HAWA WALIKUWA HAWAANGALII MBALI, SEHEMU ZA MWAMBAO NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA NCHI WAO WAKAENDA KUMKABIDHI JOMO KENYATA SASA TUNAONA HIVYO DUNGU ZETU WANATAKA KUWADHALILISHA.
LAKINI HII WANATAKA WAISLAMU WAANZISHE JIHADI YA KUDAI HAKI YAO, NA KWA KWELI WATAJUTA MAKAFIRI WA KENYA MAANA SASA KUTAKUA HAKUKALIKI, INSHAALLAH WAISLAMU WA KENYA MUTAFANIKIWA HII NI MIONGONI MWA MITIHANI NA ALLAH ANATUJARIBU KWA SABABU ANAULIZA KWENYE QURAAN KUWA “HIVI MUNAFIKIRIA YA KUWA MUTAACHIWA TU HIVI HIVI MUSEME MUMEAMINI BILA YA KUJARIBIWA KWA MITIHANI ILI ALLAH AMJUWE NANI NDIE NA NANI SIE” ALLAH ANASEMA KUWAELEZEA WAISLAMU WALIOPITA KUWA YAMEWAFIKA MADHARA MAKUBWA NA MITIKISIKO MPAKA WAKAFIKIA KUULIZA NI LINI HASA NUSRA YA ALLAH ITAKUJA, LAKINI TUJUWE YA KUWA NUSRA YA ALLAH IKO KARIBU ISIPOKUWA JIHADI NDIO MUHIMU.
MAISHA YA ULIMWENGU NI MAPITO TU.