Mifano ya wapinzani kupinga matokeo ya uchaguzi barani Afrik

Written by  //  09/03/2010  //  Kimataifa  //  Zima maoni

Maandamano ya upinzani kuendelea Togo:
Vyama vya upinzani nchini Togo, vimesema maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais nchini humo, yataendelea hii leo kama ilivyopangwa, licha ya serikali kuharamisha maandamano hayo.

Msemaji wa serikali amesema, maandamano hayo yameharamishwa kwa sababu leo ni siku ya kazi. Siku ya jumamosi wiki iliyopita Rais Faure Gnassingbe, alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais, matokeo ambayo yamepingwa vikali na vyama vya upinzani.

Wanaharakati hao wameapa kuendelea na maandamano yao licha ya polisi kutumia vitoa machozi kuwatawanya siku ya jumomosi katika mji mkuu wa Lome.

Chanzo:bbcswahili

Comments are closed.