Uingereza Yapongeza Serikali ya Mseto Zanzibar
Written by Bostoki // 04/08/2010 // Kimataifa // 2 Comments
Serikali ya Uingereza imewapongeza wakazi wa Visiwa vya Zanzibar kwa kupigakura za kukubali serikali ya mseto baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Waziri wa Uingereza anayeshughulika masuala ya Afrika, Henry Bellingham alimpongeza Rais Aman Abeid Karume pamoja na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Seif Hamad Rashid kwa kuweka historia ya kumaliza siasa za chuki ma uhasama visiwani humo.
” Tunaitakia Zanzibar kila mafanikio wakati ikiendelea na siasa za kushirikiana, ” alisema Waziri huyo katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana. Vilevile alisema Uingereza imepongeza Rais Jakaya Kikwete kwa malengo na juhudi zake za kufanikisha tukio hilo la kihistoria.




2 Comments on "Uingereza Yapongeza Serikali ya Mseto Zanzibar"
Tunaomba sawazisho kwenye jina la katibu wa CUF.Linaonekana halipo sahihi.
sawazisho jengine ,nini serikali ya MSETO badala ya Serikali ya Kitaifa which is which ? kama hutojali