Habari

Hali ya Masheikh ilivyo gerezani

Jana nilibahatika kuswali swala ya Ishaa katika msikiti wa Ijumaa Biziredi, I say kulikuwa na ustadh fulan akitoa taarifa kuhusu hali ya halisi ya kesi zinavyoendelea na hali ya afya ya mashekhe wetu.

Kwa ujumla hali zao ni mbaya saaana. Katika maelezo yake, ustadhi alisema kuna mmoja wa masheikh wetu hali yake mbaya kwa maana ya ubaya. Tayar hawezi chochote kila kitu asaidiwe hata akienda haja ndogo na kubwa lazima ashikiliwe.

Kuna sheikh mwengine yeye tayar amehasiwa. Walimbada vya kutosha hadi wakamvunja pumbu.

Sheikh mwengine amepigwa sehemu ya kichwani wakati wa kumuhoji. Hivyo wamesababisha maradhi ya kila mara kuanguka na kupoteza fahamu.

Ustadh alifafanua sana kuhusu hali halisi ilivyo kuhusu mashehe wetu.

Baadhi ya wasikiliazi waliokuwepo walishindwa kujizuwia na Kuanza kutokwa na machozi msikitini.

Loooh watu wametokwa na iman jamani, mtu anafanya kitu utafikir atabaki maisha. Mwenyezi Mungu awalaan wote waliohusika na udhalilishaji huu.

Jumla masheikh walioko ndani ni 52.

Miongoni ni driver wa Amir Farid. Kijana mdogo sana alikuwa hajawahipo kufika Daresalam ila aliijua kwa kukamatwa na kupelekwa huko.

Kijana huyu kapelekwa Arusha na amebambikiziwa kesi ya kulipua bomu kanisani huko Arusha.

Tagsslider
Share: