Bwana Haji Gora Haji – Hazina isiyokwisha
Written by Ashakh (Kiongozi) // 23/01/2012 // Habari // 11 Comments
Naam leo nimepata nafasi ya kuonana na nyota adhimu katika fani ya utungaji Zanzibar, Bw Haji Gora Haji. Kwangu mimi ilikuwa fursa adhimu katika maisha yangu kwa mara ya kwanza kuonana naye uso kwa uso.
Bw Haji Gora ametanda kwenye fani hasa ya utunguja wa mashairi pamoja na uandishi wa vitabu. Bila ya shaka ni hazina kubwa kwa Zanzibar na kizazi chake. Kuna mengi kwa vijana wetu wanaweza kujifunza au kurithi kutoka kwake.
Amma kwa upande mwengine srikali yetu imeshindwa kuienzi hazina hii isiyokwisha. Kiujumla maisha ya msanii huyu hayaendani na juhudi alizochukuwa kuisambaza sanaa katika jamii yake. Bw Haji hakupata elimu rasmi, alianzia katika shughuli na kazi za uchukuzi wa mizigo.
Kwa mchango wake mkubwa hasa pale alipotunga vitabu visivypongua tisa na kutumika katika mafunzo ya kiswahili ndani na nje ya nchi, tulitarajia serikali nayo kwa upande wake ingeweza kuienzi nyotA hii.
Hata hiii idara ya Mila na Utamaduni nayo imeshindwa kutayarisha japo tamasha la kumkumbuka wakati bado yuko hai. Bw Haji Gora sasa hivi anatayarisha shairi lake l akuhuzunika na kukumbukwa kwake, akisema tunamsubiri mpaka keshaingia kaburini ndio tuanze kuhuzunika.
Kuna mengi natarajia kuyapa kutoka kwake. leo nimeona nije na kampeni maalumu ya kutaka hazina hii isiyokwisha ienziwe. Tuanze na sisi Wazalendo kumuenzi, sina shaka na serikali kwa upande wake itafuatia.
Bw Haji Gora haji hazina isiyokwisha. Tumuunge mkono.
Tega sikio kuna mengi kutoka kwake.






11 Comments on "Bwana Haji Gora Haji – Hazina isiyokwisha"
KICHWA CHA HABARI HAKIENDI NA MADA!
mimi nikimpenda mzee gora pale nilipokuwa nikipoteza muda wa kuzungumza naee mimi na mjukuu wake haji gora haaaaa lipata mengii alinisimulia vipi nad ikhwa safaa ilianziswhwa na jina lake la mwanzo likiwa nad shubu baada ya hapo ikaja nadikhwan safaa akaniambia vipi chama cha cuf kiliaziswha tumbatu chini ya marehemu mzee maburuki mwaznzo kikijulikana kwa jina la ZUF na badala ya hapo akanihadith mambo ya uhuru wa 63 akanuambia jinsi uwovu wa karume na na nyerere na kupotea uhuru wa zanzibar huyu mzee nimemmisi sanaaaaaaaaa ninamuhamuu lakini hatutaka tujuwe kitendawiliiiii hapa huwa akitukatisha mazungumzo ila akituimbia mashairii utapendaa mungu ampe mazuriiiii
haji ukikaa nae muulize akuambie kile kitendaweiliii
HATA HALIKUNIKI SEKEBBUKE WAENZIWE NDIO MAANA ZANZIBAR KUMEKUWA MICHOZO YA KITANGANYIKA INACHUKUWA NAFASI MAANA SAI TUNAUWA TANGANYIKA WANAPANDA CHIMBENI HATA WAKIVAA MATAMBARA LAKINI YANAENDANA NA UTAMADUNI WETUUUU
ASHAKH(KIONGOZI)
ANAJARIBU KUBADILISHA TOPIC AU MADA INAYOHUSU MASLAHI YA ZANZIBAR NA KULETA HABARI ZA HUYU MZEE. SIO WAKATI WAKE HUU KUJADILI MZEE WA ASILI ZILIPENDWA.
TUWEKE MIKAKATI YA KUMGOA SHAMUHUNA NA KUNDI LAKE SIO KUZUNGUMZA ALINACHA NA ZILIPENDWA.
MUBADILIKE KATIKA KUTETEA MASLAHI YA ZANZIBAR.
@Dume la Chakechake..kumbuka
Huwezi kuendelea mbele kama utasahu ya nyuma(kale). yakiwemo “utamaduni, mila, desturi” inavyotakiwa yote hayo ni kukuzwa. Kwani maadui wenu mara nyingi katika mbinu moja wapotaka kuwatawala ama kuwapachikisha mambo yao ni kuwasahaulisha vizazi vimpya mila, desturi na tamaduni zao. kiufupi elimu (elimu ni ya njiya nyingi) hii itakuwa ya mambo ya kale(historia)
Kumbuka hizo nchi zote zilizoendelea zina hadithi zao za zaidi ya miaka 1000. Katika karne hizo pia wamepigana kisiasa kidictor mpaka kidemokrasia lakini wamejitahi kutuza asili na tamaduni zao tena kwa maandiko.
Tumuunge MIKONO mzee na kama wapo wengine pia wajitokeze ili waandike.
@Dume la chakechake
Inaonekana wewe ni mgeni kwenye ukumbi huu. Hii ni mara ya mwanzo kusikia jina hili. Ni kama mwezi tu ndio nimepungua upekuzi.
Alakullihal, hii mada pia nayo inahitajika kupata mikakati ya ukombozi kamili. Kwani na yeye ni miongoni mwa wanaharakati asiyeficha hisia zake. Zaidi basi anasema bora kila mtu chanjale.
Mtanganyika apingwe, Shamuhuna aondoke, zanzibar ihuike, tonge ifike mdomoni, nakadhalika yote haya hayataki kuzungumzwa likaachwa jengine, bali yazungumzwe kwa pamoja.
wakati tunasubiri mengi kutoka kwa mzee Gora tunaomba musisahau kutupa historia yake kamili .
Hongera sana kwa kutuletea taarifa za huyu Mzee. Mimi nilikuwa nikimsikia sana ijapokuwa sikumfahamu kwa sura. Kwa mtu ambaye hakuwa na elimu kubwa lakini akaweza kuwasiliana kwa kuandika hadithi ni mafanikio makubwa ya kuigwa na vijana.
Tuandike historia yake, waandishi chukueni hiyo kama ni changa moto. Siyo kila siku siasa siasa siasaaaaaaaa.
Hadithi ya Siti binti Sadi tumeifahamu kwa sababu marehemu Shaaban Robert alichukuwa nafasi kuiandika.
Mukipata nafasi tuleteeni na za wengine akina Mashaka na wenzake Bi Njiwa na kadhalika. Nakubaliana na Sh. Haji Gora siyo musubiri mpaka wameingia kaburini ndiyo munaanza sifa.
@ Dume la chake chake
Ndugu yangu dume haliwi kama ulivo ww, hiyo ni ishara ya ubaguzi, unajiona ww ni dume la chake chake, lakini alichokifanya babu huyu wa kitumbatu kina mchango hata kwa kizazi chako.
Ukweli ni kwamba huyu mzee kasahauliwa kwa kutokana na mtazamo wake wa mambo ya siasa, basii!!!
Mzee smart sana . Hakupata elimu rasmi na antunga vitabu vya Kiingereza (e.g: THE SECRETS OF GININGI). Kama angesoma sijui ingekuaje.