HOTELI ZA KITALII NUNGWI ZATEKETEA

Written by  //  09/09/2010  //  Habari  //  4 Comments

Hoteli za Kitalii Zawaka Moto Nungwi
Salma Said
ZAIDI ya hoteli nne za kitalii na nyumba 12 za wananchi wa kijiji cha Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja zimeteketea vibaya kwa moto jana majira ya saa 7:12 mchana katika kijiji hicho.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo wamesema awali waliona moto na moshi mkubwa ukitokea katika maeneo yenye hoteli za kitalii na baadae moto huo kusambaa katika hoteli nyengine ambazo zilikuwa zikiwaka kwa kasi kubwa kutokana na upepo uliokuwa ukivuma baharini nyakti hizo.

Kamanda wa ppoli mkoa wa kuskazini Unguja, Mselem Masoud Mtulya alithibitisha kutokea kwa moto huo na kuzitaja hoteli zilizoungua ni pamoja na Rummi ambayo imeteketea vibaya sana kwa kuwa ndio iliyoanza kuwaka na baadae moto huo kusambaa na kurukia katika hoteli iitwayo Bwagamoyo ambayo imeungua paa lote la hoteli hiyo.

Kamanda Mtulya alisema baadae moto huo ulishika katika hoteli ya Union ambayo nayo imeungua vibaya vyumba vya kulala na eneo lote la baa, ukumbi wa chakula na maduka ya vifaa na nguo za kitalii yaliokuwa ndani ya hoteli hiyo.

Aliitaja hoteli nyengine ni Diving Center ambayo nayo ilitekeleta katika eneo lake la ukumbi uitwao East Afrcan, ukumbi wa jambo brothers, sehemu ya jikoni yote imeungua na baadhi ya vyumba na kumbi zake zikiwa zimetekeleata vibaya sana.

Aidha alisema licha ya moto huo kusambaa kwa kasi lakini wageni wanane waliokuwa wamelala ndani waliwahi kuokolewa huku wengine wakiwa wamekimbia ambao wengi wao nyakati hizo walikuwa nje ya hoteli hizo na baadhi yao walikuwa wakipunga upepo na wengine walikuwa katika sehemu za kulia wakijipatia chakula.

Alisema nyumba za wananchi nazo hazikusalimika kutokana na moto huo ambapo zaidi ya nyumba 12 ambazo zipo karibu ya hoteli hizo zilizoungua zimeshika moto kutokana na moto huo kusambaa kwa kasi kutokana na upepo na kuwa zimeezekwa paa za makuti ambazo hushika moto haraka.

Kamanda Mtulya alisema chanzo cha moto huo hakijajulikana bado lakini jeshi la polisi linajitahidi kutafuta chanzo halisi cha kuzuka moto huo kabla ya kutoa taarifa sahihi kwa vyombo vinavyohusika.

Wakizungumza kwa jazba wananchi waliokuwa karibu na hoteli hizo na wengine nyumba zao zilizochomeka wamesema ingawa hawajui chanzo cha moto huo lakini wameshuhudia moto ukiwaka na ndipo walipopeana taarifa ambapo baadhi yao walikuwa nje ya nyumba hizo wakitafta riziki.

“Mnajua tena muda wa sikuukuu umewadia huwezi kukaa nyumbani lazima uhangaike utafute chaza, ukate kuni ukalime mwani ndipo upate pesa ya mkate na hali hiyo hiyo kwa nguo ya sikukuu lakim,a ujitume na ndio tukasikia kuwa kuna moto lakini sisi tulikuwa humo katika harakati za kutafuta riziki” alisema Mwanajuma Makame.

Akielezea mkasa huo wa moto kijana aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Machano amesema baada ya kuwaka moto na kuanza kurukia katika nyumba walikwenda kuita gari la kuzima moto hapo hapo lilitoka kwa kasi kukimbilia eneo la tukio lakini matokeo yake kufika halina maji.

“Hili gari la fire limekuja kwa kasi sana lakini bahati mbaya lilipofika hapa halina maji hata tone moja na ndipo lilipokwenda mbio kule baharini kuchota maji ya chumvi na lilipofika kule likaganda na kwa kweli wananchi walilizomea sana hili gari… kwa hivyo msaada wa wananchi ndio uliosaidia sana kuokoa nyumba nyengine zisiwake moto” amesema kijana huyo.

Alipoulizwa Afisa mwenye dhamana ya gari hilo, Shaukuru Shukuru alithibitisha gari leke kwenda eneo la tukio lakini alikataa kusema kwamba gari halikuwa na maji na kwamba lilikwamba baharini “Hapa sasa hivi tunakunja kunja vifaa vyetu tumeshamaliza kazi ya kuzima moto…” alisema na kuongeza.

“Unajua wananchi wana maneno mengi wao kila kitui wanakichukuliwa kisiasa lakini bwana maji katika hari letu yalikuwepo na huko baharini kuwa tumekwenda kuchota maji ya chumvi sio kweli kabisa maji yalikuwepo na ndio yaliozima moto” alisema Shukuru ambaye alisema wamekamilisha kazi hiyo majira ya saa 11 jioni.

Moto huo umefanikiwa kuzimwa jana jioni baada ya jeshi la polisi, vikosi vya uokozi na wananchi kushirikiana kwa pamoja na kuuzima moto huo ambao ulikuwa ukisambaa kwa kasi katika maeneo mengine ya nyumba zilizokuwa karibu na hoteli hizo.

Tatizo la hoteli kuungua moto limekuwa likitokea mara kwa mara visiwani Zanzibar ambapo mwezi uliopita jumla ya hoteli za kitalii na nyumba zaidi ya sita ziliteketea kwa moto katika kijiji cha Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.

Hoteli zilizoungua mwezi uliopita ni pamoja na Visitors Inn, Sau Inn na Bungalow ambapo zote zipo eneo la Jambiani ukanda wa pwani ambapo kumbi na zaidi ya vyumba 12 vya kulala wageni viliteketea kutokana na moto huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Augustine Olomi pamoja na kuwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo siku hiyo lakini hadi leo hajasema chanzo cha moto huo kilitokana na nini zaidi ya kuahidi kuwa suala hilo linashughulikiwa na jeshi la polisi.

4 Comments on "HOTELI ZA KITALII NUNGWI ZATEKETEA"

  1. Bosco 09/09/2010 kwa 8:02 um ·

    Kamanda wa polisi mkoa wa kusini unguja Augustine olomi.

    Hawa ndio mfano wa makamanda wetu tulionao zanzibar.

    Kuhusu kuungua nyumba mimi nawapa pole watu lkn nimefurahi kuungua kwa hizi hoteli ingawa ni ndogo ndogo lkn ndio mungu ameamua kuondoa ufuska mwenyewe kwakua sisi tumeshindwa.

    Eid mubarak

  2. sale 09/09/2010 kwa 8:39 um ·

    Mtumee ..Kuna majina ya Olomi na Augustine tena yameshika madaraka ya juu Zanzibar? msalieni mtume jamani…

  3. phillemon mikael 10/09/2010 kwa 11:00 mu ·

    …du sale nyie ni wabaguzi na wadini..hadi inatia kinyaa……nausea..!!…kwani hiyo ni KMKM ,Mafunzo ,valantia au JKU…acha kuwa mjinga bwana….ina maana wakristo walioko visiwani hata kama ni asilimia ndogo…hawatakiwi kupewa kazi ….ubaguzi tu umewajaa baadhi yenu…kwani yule kamanda wa polisi aliyewapa silaha shujaa weenu wa mapindzi..john okello,….si anaitwa Kisasi!?

  4. sale 10/09/2010 kwa 11:53 mu ·

    Phillemon mikael, sizungumzii ubaguzi wa dini mi nakubaliana na mtu yeyote na dini yake lakini ndio ninapozungumzia Zanzibar unaweza kusema ndio nimbaguzi kwa sababu zanzibar ina majina yake na dini zake za asilia kama vile Waislamu, mabaniani, wahindi,shia, na Kisasi pia Mzanzibar mwenye uchungu hakuja Zanzibar kutafuta maisha …Lakini kwa nini hamfahamu jamaniiiii mnapozungumzia Zanzibar,,,Tuko njiani kujenga chama cha Kislamu hapo nyumbani na kitashika madaraka ya serikali siku za mbele

Comments are now closed for this article.