Habari

Huwezi kufungia mitandao ya kijamii

Taarifa iliyosambaa kutoka Ikulu inatishia kufungia mitandao yote ya kijamii. Lengo ni kumzuwia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania asikosolewe, asishauriwe wala asielekezwe.

Kwamujibu wa sheria na orodha ya mambo ya muungano suala la technology ya Habari haimo kwenye orodha hiyo. Wakati jambo la Muungano ni mawasiliano.

Jee kufungiwa huku kutaathiri hadi Zanzibar?

Au itakuwa ni kule kwenye himaya yake ya Tanganyika.

Kwa upande mwengine Tanzania imepata viongozi wa ajabu ambao hawajuwi zama gani wanaishi. Ikumbukwe walitumia mabilioni kutengeneza network infrastructure, kwa madhumuni ya kuboresha mawasiliano. Nchi imeingia kwenye digit kwa madhumuni ya kunufaisha na kuboresha mawasiliano. Na hata uwekezaji wa mitandao ya simu imbayo imetoa ajira nyingi na kukuza ushuru wa na pato la nchi. Waswaghiruhu wakabiruhu

Vipi leo viongozi kama hawa wasio jijuwa wala kujitambua wanatishia kufungia mitandao ya kijamii, jee wametathmini hasara amma athari zake.

Kama niliposema kwenye issue ya umeme na hapa nasema vilevile, hawawezi wala hawathubutu kufungia mitandao ya kijamii. Ikiwa watafuta mbinu ya kujilinda kwa karne hii wamepitwa na wakati.

Tutawasuta hapahapa pale watakaposhindwa kutekeleza azma yao. Wanachoweza kufanya ni kitisho cha mtu mmoja mmoja kama hivo kuzuwia post yake lakini sio kufungia. Mchezo unaendelea, subiri tuone

Share: