Ikiwa maridhiano Zanzibar yatakuwa kweli , Karume atajenga

Written by  //  15/07/2010  //  Habari  //  5 Comments

Na.B.OLE,

Itakuwa ni historia kubwa na ambayo haitasahaulika Zanzibar ikiwa maridhiano yaliofikiwa kati ya Mh. Karume na Maalim Seif yatakuwa ni ya kweli.

Wazanzibar walio wengi bado wana wasi wasi mkubwa juu ya hili, kutokana hasa na historia ya Chama Tawala kutokupenda mabadiliko ya upepo wa kisiasa Zanzibar.

Kuna wale wanaofikiria kwamba maridhiano haya ni shinikizo kutoka kwa Jumuiya za Kimataifa na kuna wale ambao wanafikiria kwamba labda ni kutokana na makundi ya wahafidhina kujigawa na kufikiria kulipiziana visasi zidi ya kundi litakalopata madaraka na lile litakalokosa.

Pia kuna wale wachache waliojengwa na fikira za utakatifu na kuona kwamba yaliopita yameshapita Zanzibar kwa wakati huu, inahitajika amani na utulivu kwa Wananchi, hoja ambayo kidogo ni dhaifu hasa tukiangalia hali ya Zanzibar ilivyojigawa kimakundi.

Zote hizo zinaweza kuwa ni sababu ya maridhiano lakini ukweli ni kwamba nani anajua kama haya maridhiano yatakuwa ya kweli ?

Na lengo la maridhiano haya ni nini na kwanini Mh. Aman akubali maridhiano wakati huu, kuna umuhimu gani na hasa ukichukulia kwamba yeye anamaliza muda wake wa uongozi na ashachopata kinamtosha, ni kitu gani anahitaji zaidi ? Kwa nini asibakie kuwa mstaafu kama vile Dr. Salmin akawa anasemea pembeni tu lakini hamkeri mtu?

Sote tunaelewa kama Rais Aman kafanya mengi yakiwemo Mazuri na mabaya. Moja kati ya baya kubwa ambalo Mh. Amani amelifanya kwa Wazanzibar ni kudhulumu nafasi hiyo ambayo anayo hivi sasa, kwani hakuipata kwa ridhaa ya Wazanzibar wenyewe bali ameipata kwa njia ya dhulma na udanganyifu wa tume kwa kupitia chama chake. Hilo litakuwa ni kosa lake atajuana yeye na mola wake kama ana amini kwamba iko siku ya malipo.

Lakini kama ni kweli basi zuri moja ambalo litampatia sifa kubwa na kujijengea heshima kubwa na hata pengine kufuta mabaya yake yote ni suala zima la maridhiano kama kweli yeye binafsi ana azma njema na dhamira hiyo.

Atakuwa ni kiongozi pekee wa Zanzibar ambae juhudi zake angalau za kukaa meza moja na wapinzani tu zimeonekana ,kwani viongozi waliopita hawakutaka hata kusikia kauli ya neno maridhiano likitajwa miongoni mwa Wazanzibar.

Tulishuhudia zaidi kibri, mbwembwe, vitisho, uhasama na maneno yenye kukejeli miafaka hiyo na hata kufikia kufananishana na wanyama kama vile mbwa, yote yalitokea sio rahisi kusahaulika kwani yatabakia ni historia, na historia mara zote hukumbukwa licha ya kuwa kuna watu wataumia na kuna wengine labda watafurahia hata kama ni mabaya yaliotendeka au mazuri.

Sote hatuwezi kubisha kuhusiana maridhiano yaliopita huko nyuma kwamba hayakuwa na lengo la mapatano bali ilikuwa ni usanii wa kisiasa na kupoteza muda ili wananchi wachoke na wimbo huo wa maridhiano.

Kwani haya maridhiano sio mara ya mwazo kufanyika na mwisho wake hali inakuwa mbaya kuliko ilivyokuwa mwanzo. Tumeshuhudia miafaka zaidi ya miwili na hakuna hata mmmoja uliosimama na hii ndio sababu walio wengi wana wasi wasi na haya maridhiano yaliopo leo hii.

Ni vyema tukajikita katika upande wa kheri kuliko kuelekea kwenye shari, tuchukulie haya maridhiano mara hii yatakuwa ya kweli. Kama ni hivyo basi Mh. Aman atajijengea heshima kubwa na historia ambayo haitasahaulika katika Taifa la Zanzibar.

Kwani atakuwa ni kiongozi pekee alieonesha kwamba kweli anajali kuona migogoro Zanzibar inamalizika licha ya mabaya yake aliofanya , lakini kuna uwezekano wa kusahaulika na matokeo yake akaonekana ameifanyia jambo kubwa Zanzibar na kila mtu kumuombea dua za kheri.

Sifikirii kwamba hichi kinachoendelea hivi sasa Zanzibar kwamba viongozi wengi ndani ya chama cha Mapinduzi wanakiunga mkono, kimawazo yangu ni kwamba Mh. Amani anaonekana kama ni msaliti ambae anashirikiana na upinzani kukisaliti chama chake, hoja ambayo inaungwa mkono sana na Wahafidhina.

Ubaya zaidi unaonekana kutokana na huyu mtu ambae anashirikiana nae yaani Maalim Seif ambae Wahafidhina wa Zanzibar hawataki hata kumsikia achilia mbali kumuona akiingia ikulu kufanya mazungumzo ya amani kuitakia mema Zanzibar na watu wake.

Sote tunaona ajabu hadi kufikia leo hii na wakati kama huu,kwamba imebakia miezi michache na uchaguzi mkuu, huku tukiona Zanzibar iko shuari bado, melody na Janjaweed hawajanza kufanya vitu vyao ni jambo la kushukuru na kupigiwa mfano, ama kweli tukiamua kila kitu kinawezekana.

Waswahili wanasema tusiandikie mate wakati wino upo, tusibiri tuone na tushuhudie mwisho wa maridhiano yetu, ili tuweze kujua nani ni mkweli na nani alikuwa akicheza shere zidi ya Wazanzibar.

Ni imani yangu kwamba mwanga mzuri na alfajiri njema imeshaanza kuonekana Zanzibar, hatuna budi kushirikiana kwa pamoja na wale wote ambao hawataki kuwaona Wazanzibar wakipatana na kuitakia mema Zanzibar basi mola wetu, wewe unajuwa vyakuwafanya watu hao.Zile dua za Maisara zichukuwe mkono wake kwa watu hao waovu na wakorofi.

Amen.

5 Comments on "Ikiwa maridhiano Zanzibar yatakuwa kweli , Karume atajenga"

  1. mfurukutwa 15/07/2010 kwa 7:42 um ·

    Baada ya manyang’unya mengi aliyofanya Dk. Karume, ameona amalizie uzuri. Hii ni ile hekaya ya jamaa aliyeuwa watu 99 na akamalizia wa 100 baada ya kutopata jawabu muwafaka lkn bado akawa anahitaji kutubu!! Kwa mtazamo mwengine Dk. anaonenyesha kuwa ni mtoto wa mjini hakulelewa shamba kidombo na kwengineko! Anajua wazi kuwa kama hajaweka mazingira safi chechote kinaweza kutokea dhidi yake…hadithi ya Chiluba wa Zambia!!

  2. Junius 15/07/2010 kwa 8:23 um ·

    @B.Ole,
    Turudi nyuma kidoogo mwaka 2000 wakati Amani A.Karume alipotangaza kuchukuwa fomu ya kuwania kuteuliwa na chama chake. Kauli aliyotoa wakati akichukua fomu alisema,anajuwa muarubaini wa matatizo ya kisiasa Zanzibar na kuahidi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa iwapo atachaguliwa.

    Tumeshuhudia mizengwe na vitimbi vilivyotangulia kuwa si yeye aliyetakiwa na wakubwa wa wakati huo na kwa kuwa “king makers” wapo upande wa pili yeye akaibuka mshindi na akaapa kufuata matakwa yao, la kwanza likiwa kukubali kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri la Mh.Mkapa. Hakukuwa na cha serikali ya mseto aliyoahidi wala cha nini.

    Tunaulizana kwanini sasa, at the eleventh hour Karume anarukia maridhiano?
    Kwanini jibu lisiwe kwanini Dr.Salmini alilazimisha Dr.Bilal awe mgombea urais mwaka 2000?
    Kwangu mimi nitaendelea kuamini kuwa malengo ya maridhiano haya kwa upande wa Maalim Seif na kwa upande wa rais Karume ni tofauti kabisa, hayalingani hata kidogo na tafauti yake ni kama mashariki na magharibi.

    Tumeshuhudia namna Karume alivyoingia madarakani kwa nguvu za dola na kumwaga damu, kiufupi kijambazi jambazi.Isitoshe wakati wa utawala wake tumeshuhudia namna alivyoendesha nchi kibaguzi na kimitafaruku ambayo mbali ya kuifanya kwa wananchi wake bali ndani ya chama chake. Kujilimbikizia mali na maeneo ya ardhi yaliyochukuliwa na kupewa masahiba zake ni jambo la kawaida tuliloshuhudia katika utawala wake.

    Sote mashahidi kuwa alimteua shemeji yake Mansour Yussuf Himid kusimamia wizara ya ardhi na nishati….kwa makusudi ya kusimamia miradi yake. Haya yote na mengine yalifanyika kwa mda wa miaka kumi na bila shaka Karume anafahamu mda utafika itabidi aache madaraka.
    Kikubwa anachokihofia ni KISASI kwa watakaokuja ambao alishawajuwa(akina Dr.Bilal).
    Mkikumbuka Dr.Bilal aliwahi kusema “sitalipa kisasi”.
    Aliowahofia zaidi ni walewale aliowabaguwa na kuwanyanyasa wakati akiingia madarakani kwa kuwa tu walimkataa kiswandui na akawashinda machinjioni Dodoma kama Dr.Shein.

    Karume amecheza karata yake vizuri kwa namna mbili, kwanza kukubali MARIDHIANO, pili KUPATA MGOMBEA ANAYEMTAKA YEYE (DR.SHEIN). Haya yote yameshamtengezea mazingira salama ya kuondoka marakani na dhambi za wizi,utesaji na mauwaji ya watu wasiokuwa na hatia bila ya hata kuulizwa nyoko, na kamwe anaonekana shujaa.

    Maridhiano yamekuja na yanafaida kwa Karume iwapo mpango wake wa kupata mgombea anayemtaka ungefeli na yamekuja mwanzo kabla ya Dr.Shein kukubali wito wa Karume na Kikwete kuingia katika kinyan’ganyiro cha urais. Hivyo ni afadhali kuwa please wapinzani na Maalim seif kwa nia ya kuwa disturb watakaomfatia iwapo watashinda.Kwa hayo Seif angetumika kumkingia kifua karume,aliye asisi naye siasa za maridhiano.

    Kwa karume maridhiano haya ni salama kwa ustaafu wake na hatapata bughdha alizompatia mwenzake, Dr.Salmini alipostaafu. Na kupata mgombea wake aliyembebesha siasa hizo hizo za maridhiano ni zaidi ya ushindi katika maisha yake ya ustaafu.

    Kwa Maalim Seif ni wazi kuwa si mara ya kwanza kutafuta umoja wa Zanzibari,ameshajaribu mara kadhaa kwa nia safi kuratibu siasa za maridhiano(siku hizo muwafaka) ili yawepo mazingira mazuri ya kufanya siasa za ushindani wa kistaarabu. Ndiyo nikasema awali kuwa malengo ya Maalim Seif na karume katika maridhiano ni tofauti.Mmoja (Karume)anasalimisha roho yake,mwingine (Maalim Seif)anapigania umoja wa kweli.

    Ikiwa maridhiano yatakuwa ya kweli wa kustahili credit ni wazanzibari waliovumilia adha na shida zote,mpaka wamelazwa kiza miezi mitatu, wakiongozwa na Maalim Seif ambao kwa mda mrefu amekuwa akipigania siasa hizo bila ya mafanikio kwa kuwa tu wakubwa hawakuwa na nia ya kweli ya kisiasa.
    MUNGU IBARIKI ZANZIBAR
    J

  3. Gumegume 16/07/2010 kwa 5:35 mu ·

    B.OLE, Kwa kweli unayozungumza na maoni yaliyotolewa na wachangiaji ni sawa kabisa. Hata hivyo pamoja na kuwa wenzangu wameeleza juu ya azima aliyowahi kuitoa Rais Karume hapo nyuma alipochukua fomu kuwa alikuwa anahubiri Serikali ya Kitaifa lakini hakuitekeleza. Ni kweli kabisa na hii ndio ambayo inatufanya pia kutupa mashaka dhana ya kuundwa kwa Serikali ya Kitaifa. Linalojitokeza hapa CCM inawengi sio Karume tu, na kinachotokezea ni kuwa bado kuna wahafidhina wengi ndani ya CCM wanapinga dhana hii kwa sababu tu watakosa nafasi za uongozi ndani ya Serikali. Kundi hili linaonekana linawapiga debe wengi kwa hiyo utekelezaji wake unataka kwanza kuwe na ‘good wll’ pamoja na umakini. Hivi sasa kwa taarifa inasemekana kuna wanaodai kwanini Karume hakuunda yeye Serikali ya Kitaifa katika uongozi wake na kutaka mrithi wake atakapokuja ndio aunde serikali ya umoja wa kitaifa?

    Kwa ujumla wake ninalokusudia kusema hapa ni kuwa bado dhana hii ya kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar linasuasua na linatiwa utata na baadhi ya wale wahafidhina waliondani ya Serikali na ndani ya CCM, hata hivyo bado tumuombeni Mwenyezi Mungu awatie ilham hawa mahafidhina kwanza waikubali dhana hii na pili kwa Karume kuharakisha huu mchakato wa kuunda Serikali ya Kifaifa. Ikiwa dhana hii itafanikiwa ni kweli itamjengea heshima kubwa Karume na kufuta ya makovu kwa wapinzani wake na wazanzibari kwa ujumla yao kutokana na mambo mbali mbali yaliojitokeza hapo kabla.
    Wachunguzi wa mambo ya siasa za Zanzibar wa ndani na nje ya Zanzibar pamoja na Jumuiya ya Kimataifa wanayangalia na kufuatilia kwa karibu…kwa maana ya kusikiliza yanayoendelea na kutokezea Zanzibar, juu ya hatua mbali mabali zinazochukuliwa katika kufanikisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa baada ya Uchagauzi wa mwezi Oktoba. Pia wachunguzi hao wanafikiria mbali zaidi ikiwa mpango huu wa maridhiano utafanikiwa basi kuna uwezekano mkubwa wa Raisi Karume kufikiriwa kupata ile zawadi wa viongozi bora inayotolewa kila mwaka, ambayo miaka hii miwili iliyopita imekosa kuchuliwa na viongozi wa Kiafrika. Kwa hiyo, ‘let hope for the best may be President Karume will be able to turn the coin’ na pengine mwaka ujao kama naye atakuwa mkweli na kulifanikisha hili la Kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Laa ikiwa na yeye alikuwa na lengo la kupoteza ajenga na kutaka kujijengea umaarufu ili watu wamuone amemaliza vizuri ‘shauri yake’ kwa Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki. Binafsi sitarajii kabisa kuwa kauli zake alikuwa anatudanganya; kalini kama binaadamu pia sina sababu ya kuamini aslimia mia moja (100%). Hata hivyo, bado kwa kiasi fulani nina imani kwa vile amezungumza kwa hiyo tuendelee kumumba mwingi wa rehma ili ndoto za kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ifanikiwe Zanzbar kwa lengo lile lile la kuwa na umoja na mshikamano wa Wazanzibari wote.’Sio siri, kuiondoa mbegu hii ya ubaguzi ambayo ilitiliwa maji sana na Kamando akisaidiana na Bilal ni kubwa na bila shaka litamjengea hatma njema sio tu kwa watu hapa Zanzibar au Tanzania bali hata kwa Mwenyezi Mungu mbele ya haki. Kwa upande wetu kbwa tuendelee kuoma kheri juu ya hili.

    Wabilah Taufik

    Gumegume
    guzina maana kuwa wanaongea na liangalia

  4. mtu kwao 16/07/2010 kwa 11:01 mu ·

    A.alaaykum ndugu zangu…Mimi ninataka kujua hivyo hivyo kwanini karume asifanye yeye serikali ya umoja???hii ni sinema karume hastahili chochote cha kupongezwa ili ni kutiwa ndani kwani kamwaga damu pia…Kama serikali ya umoja akefanya wakati hip alipoona mambo magumu mpaka damu kumwagika…iweje Leo hii atake maridhiano tusiwe wajinga jamani tuamkeni tusiwe karume kasema anataka maridhiano tukamuona kafanya jambo la maana Ana lake jambo anataka kinga huyo!anajua atakiona cha moto Kama Hana mtu wake ktk serikali tuamkeni tushirikiane wazanzibar sio serikali ya mseto ndio itakayo tutoa hata Kama seif atakia ktk serikali ya mseto si ndio nchi itaendelea na yeye atajisahau Kama wengine na mtakuja kuona…

  5. Ghalib 16/07/2010 kwa 12:09 um ·

    AH HIZI NAONA KAMA SIASA
    B.ole
    Kumekuwa na maridiano mengi ya kiasa zanzibar kama miwili imepita na huu ni wa watu,na mikataba huwa inakuja kila kipindi cha uchaguzi,ili watuwekee imani kuwa serikali itatenda hali na tutakuwa na imani na serikali,pia kuwa shuwariiii zanzibar wakati wa uchaguzi ili wachukue nchi kimya kimya hata mkizinduka tayari wameshaivaa.

    mimi naona kama wanatuma moto wetu hivi,tukiangalia huko nyuma tulikotoka,lakini inshaa kheri,ikiwa znz itapinga ndioo asilimia 80-90 halafu ccm iyende kinyupe basi laana watazipata kwa wananchi,mana ndio imejitundika ccm.

    kazi kwao.

Comments are now closed for this article.