Habari

Imwendee Balahau Shein, Chotara Aboud na Haji Omar Kheir

Risasi na mabomu yarindima Kangagani usiku huu

16/12/2016

Kuna taarifa za kuaminika kuwa milio ya risasi na mabomu imekuwa ikisikika huko Kangagani Pemba.

Hali hii imewafanya wakaazi wa Kangagani usiku huu kuyakimbia majumba yao na kukimbilia misituni kupata manusura.

Chanzo cha hali hii ni kuwa wananchi kukataa kutajwa jina la Balahau Shein kwenye khutba ya Ijumaa.

Tokea mchana wakati wa swala ya Ijumaa hali imekuwa tete kwa wakati wa Kangagani ambapo waliswali Ijumaa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi huku mkuu wa mkoa wa kaskazini na mkuu ya wete wote wakihudhuria.

Wiki iliyopita vijana 7 wamekamatwa na polisi hadi leo hii bado wako mahabusu.

Bado haijajulikanwa ni watu wangapi wameumia kwenye mashambulizi haya, lakini inasemekana majeruhi ni wengi.

Pia haijulikani hadi sasa ni watu wangapi wamekamatwa.

Balahau Shein amekuwa kinyaa hata kusikikia jina Lake miongoni mwa wananchi wengi wa Zanzibar, hii ni dalili kuwa amekatalika, hatakiwi lakini bado hajataka kuwa mwerevu wa kusalimu amri, bado anataka aendelee kudhalilika, na atadhalilika hapa Duniani na huko mbele ya safari, ataendelea kulaanika mpaka mwisho wa Dunia, Historia itamuhukumu yeye na Mabazazi wenzake wote, wanaoihujumu Zanzibar na watu wake.

Laana za Allah ziwashukie wote wenye nia mbaya na Zanzibar na watu wake, ameen

Hii ndio Hali ya Zanzibar Kwa ujumla

inaendelea!!

Balahau Shein, Chotara Mohammed Aboud na Mtwana Haji Omar Kheir

Mnasema kuwa Siasa isiingizwe katika dini, wala siasa isiingizwe katika mahubiri ya dini, sasa Kwa nini katika Ibada yetu ya Sala ya Ijumaa mnalazimisha litajwe jina la Balahau Shein, inahusu nini Ibada ya Sala na jina Lake?? Je haya ndio mafundisho? Na kama hivyi Basi kiongozi wa kuombewa dua si yoyote, Balahau Shein hayumo katika list ya wanaopaswa kuombewa dua, Dua anaombewa kiongozi muadilifu, anayetenda haki, kuipigania na kuifata hata kama itakuwa dhidi yake.

Kwa hivyo kulazimisha uombewe dua Wakati wewe hustahiki, Kwa sababu wewe na Mungu muna ugomvi, hii dua haikufai badili yake itageuka kuwa nakama kwako kwa sababu wewe na Makhulafaa wako nyote madhalimu.

Dua ya kumuombea Balahau Shein Ni sawa na Maombi ya Yule Mnafiki aliyekuwa akimfanyia vitimbi Mtume SAW, halafu alipokaribia kutoka roho akamuomba Mtume akifa amzike na kanzu yake, kwa sababu ameivaa Mtume kanzu ile na atanusurika na adhabu, Mtume akamtilia masAhaba wakastaajabu na kuhoji, Mtume akawaambia hii haimfai kitu, kwa hiyo hikadhalika mfano huo kwako Balahau Shein, kung’ang’ania kwako usomewe Dua kwenye khutba za Ijumaa Ni kuomba nakama na maangamizo ya Milele tena unayafanya hayo kwa mtutu wa Bunduki, huku Ni kujikaanga kwa mafuta yako mwenyewe.

Nakuonea huruma sana Balahau Shein, jutia kwa Mola wako na Kwa Zanzibari kabla majuto hayajawa Mjukuu.

Hizi Ni zama za Uwazi na Ukweli Zanzibar

@makalilive.com

Tagsslider
Share: