Hisia za watanganyika – mabadiliko ya katiba ZNZ

Written by  //  10/08/2010  //  Habari  //  25 Comments

Kujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.

Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.

Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa “maadui wa ndani”.

Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:

Zanzibar ni nchi ambayo eneo lake la mipaka ni eneo lote la visiwa vya unguja na pemba ambayo kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa jamhuri ya watu wa Zanzibar ….Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda jamhuri ya muungano wa Tanzania
Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):

1. Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.

na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi “ngapi”? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?

Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo “LOTE” la Tanzania bara na eneo “LOTE” la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema “wanyama wa mwituni”?

Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini… (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:

(
3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye
mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi,
wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko
wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya
eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa,
hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri
ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia
nchi.

Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!

I couldn’t be more blunt than that.

Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):

Mr. Speaker and Honourable Members, The Union which I am recommending to this House today is a serious matter, deserving your most deep consideration. It will not be without difficulties. There will be plenty who will see in this development an indication that Africa WILL unite, and they will the exert all their efforts to frustrate our union, sow doubts, and cause disaffection. Against this we have to be on our guard. For once this Union comes into existence it become our duty to protect it and maintain it.

May God help us and our brothers in Zanzibar and Pemba to fulfill this responsibilities.
Ooh how prophetic!!!

I’m standing on guard, by CHOICE!

Source:Mzee Mwanakijiji Via JF

25 Comments on "Hisia za watanganyika – mabadiliko ya katiba ZNZ"

  1. yusuf 10/08/2010 kwa 1:42 um ·

    ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.
    TAFADHALI FAFANUA HAPO JUU ULIVYOSEMA KUNA NCHI MOJA
    AMBAYO NI JAMHURI YA MUUNGANO
    INAVYO FAHAMIKA KITU KIMOJA HAKIUNGUNI
    MWISHO UMEMALIZIA IMETOKANA NA KUUNGANA KWA NCHI MBILI HURU
    SASA NI NCHI MOJA AU MBILI TUNAVYOFAHAMU MUUNGANO WOWOTE NI SEHEMU MBILI
    KATIBA ZOTE SI MSAHAFU IKIWA YA MUUNGANO NAYO INAWEZA KUBADILISHA PIA KWA HIVYO WAWAKILISHI WANAHAKI YA KUJADILI

  2. seletochiy 10/08/2010 kwa 1:45 um ·

    MTOA MADA
    NAOMBA UNIELIMISHE ZANZIBAR IMEUNGANA NA TANGANYIKA NDIO IKAPATINA TANZANIA NAFIKIRI NIKO SAWA!
    HAPA TUNAIONA SERIKALI YA ZANZIBAR TU SERIKALI YA TANGANYIKA IKO WAPI?

  3. ashakh 10/08/2010 kwa 1:52 um ·

    Ikiwa watanganyika mumekereka basa mutakereka sana. katiba imerekebishwa na vipengele vya kuitambua kuwa nchi na mipaka yake vimetiwa.

    Ikiwa munataka shari tuko tayari kwa shari hiyo la ikiwa munataka kheri pia tuko tayari kwa kheri vilevile.
    Zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa nchi. Mukapenda au mukachukia.

    Leteni jeshi, vifaru, nk, Wazanzibar tuko tayari kwa kupigana mpaka dakika ya mwisho.

    Mara kadha tumewambia daini nchi yenu Tanganyika, mumeona ni upuuzi. Sisi tunadai nchi yetu Zanzibar.

    Viongozi wetu, mara kadhaa, wameleta hoja za msingi mukajitia mapamba ya masikio, mukajivisha miwani za kijani, na mwisho mukajitia udongo wa vichwa eti musifahamu. siwakti tena wa kujibu kwa hoja, ni wakati wa kujibu kwa vitendo.

  4. seletochiy 10/08/2010 kwa 2:09 um ·

    MLIOKO GENEVA JIANDAEI KUWAPOKEA VIONGOZI WETU WANAKUJA KUIONDOA BENDERA YA TANZANIA IBAKI YA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR:

    LEOO TUMEFURAHIKA UNGUJA NA PEMBA YOTE SOTE TUNASHANGIRIA WAWAKILISHI KUTULETEA JAMHURI YETU M.MUNGU AMETUBARIKIA UNGUJA NA PEMBA YOTEEEE

  5. Ghalib 10/08/2010 kwa 2:16 um ·

    Mtoa mada
    Umejizonga sana,Tanzania ni baina ya nchi mbilia Tanganyika na Zanzibar,vipi wewe usemeni kuna nchi moja ? sasa kama unataka jibu,subiri imalize uchaguzi mkuu utaona kuwa zanzibar sio nchi au laa. Na hapo ndio utajua Tanzania ni nchi moja na mipaka yake yote au laa. Na hapo ndipo utajua kama Kuna nchi inaitwa tanganyika mume ifuta na kuita Tanzania,kazi kwenu.
    Sisi tunachojaribu kukufamamisha kuwa Zanzibar ni nchi ambayo eneo lake la mipaka ni eneo lote la visiwa vya unguja na pemba ambayo kabla ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa jamhuri ya watu wa Zanzibar ….Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda jamhuri ya muungano wa Tanzania ,naona munakuwa na kihere here,ndio kutapa tapa kwenu,mambo taratibu tunakuja.

  6. mahluk 10/08/2010 kwa 2:46 um ·

    asalam alaikum vipi tena naona mambo yanaanza hapa inaonyesha wabara ndio wanao upenda muungano sasa kipi kinacho wakera wanaona shida kuitwa watanganyika mbonasisi tunaona fahari kuitwa wazanzibar mambo bado wamezoea hao chao ni chao chetu ni chao almasi dhahab gas zote ni zao peke yao ila mafuta ndio yawe ya pamoja jamani hili mmeona wapi misaada yote mnachukua nyinyi z’bar hawapati leo kusema zanzibar ni nchi iliyo ungana ndio iwe nongwa muungano huu una maslah na tanganyika na sio z’bar hongera wanzanzibar kuweni na umoja mungu ibariki zanzibar mungu wabariki wazanzibar wote kila kitu kina mwisho wake hakuna muungano wa mtu mkubwa na mtoto ila itakuwa ni hila ya kumzulumu mtoto kwani ulipo taka kuungana na mtoto hukujua kuwa mtoto atakuwa na mambo ya kitoto mbona hamjaungana na burundi ruwanda uganda kila lenye mwanzo ujue lina mwisho tunataka zanzibar mpya yenye neema na amani sasa na nyinyi daini tanganyika yenu

  7. showayb ali 10/08/2010 kwa 3:11 um ·

    Yakhe,
    Amechukua muda mwingi kuandika kitu ambacho akimuhusu. Zanzibar ni ya Wa-Zanzibari wala si ya Wa-tanganyika. WAcha Zanzibar ijiamulie mambo yake.

    Tulishawajua mbinu zenu za kuifanya Zanzibar kuwa ni Mkoa wa Tanzania. Haya yalithibitika wazi wazi ndani ya Ukumbi wa Bunge na Pinda akawa ndie kiranja wetu wa kuitukana Zanzibar kuwa si Nchi. Walikuwa wakisema kisha waliyaamini waliyikuwa wakisema. Sasa iweje?

    Wa-Zanzibari tunajipanga na ikiwezekana kama hatutakubaliana basi tutauvunjilia mbali huo Muungano. Zanzibar haitokuwa ya mwanzo kutoka katika Muungano duniani bali itaongeza tu idadi ya nchi kama hizo.

  8. M.O.B 10/08/2010 kwa 4:23 um ·

    ZANZIBAR Act 1963
    1963 CHAPTER 55
    An Act to make provision in connection with Zanzibar becoming an independent State within the Commonwealth.

    1 Operation of existing law(1)Subject to this Act, on and after 10th December 1963 (the date on which Zanzibar ceases to be a protectorate and becomes an independent State within the Commonwealth and which is referred to in this Act as “the appointed day”) all law which, whether being a rule of law or a provision of an Act of Parliament or of any other enactment or instrument whatsoever, is in force on that day or has been passed or made before that day and comes into force thereafter, shall, unless and until provision to the contrary is made by Parliament or some other authority having power in that behalf, have the same operation in relation to Zanzibar, and persons and things belonging to or connected with Zanzibar, as it would have apart from this subsection if there had been no change in the status of Zanzibar on the appointed day.
    (2)Schedule 1 to this Act shall apply to the enactments there mentioned (of which those in Part I are enactments applicable to Commonwealth countries having fully responsible status, and those in Part II are thereby excepted from the operation of section 1(1) of this Act), but that Schedule shall not extend to Zanzibar as part of the law of Zanzibar.
    (3)Subsection (1) of this section applies to law of or of any part of the United Kingdom, the Channel Islands and the Isle of Man and, in relation only to any enactment of the Parliament of the United Kingdom or any Order in Council made by virtue of any such enactment whereby any such enactment applies in relation to Zanzibar, to law of any other country or territory to which that enactment or Order extends.

  9. Bosco 10/08/2010 kwa 4:57 um ·

    “Sasa hawa wahuni wa zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyengine nje ya hii NCHI moja?” haya ni maneno ya mtoa mada ambae ameshakata tamaa.
    Mtoa mada ameandika mada hii kwa jazba kubwa,chuki nyingi,khofu kubwa. Kitendo cha kutuita wazanzibar kua ni wahuni si kitendo cha ustarabu lkn sikulaumu kwani tokea lini wewe na ustarabu? Si umezoe kula mizoga iliyokufa? Si ndio hawa wanaokula panya? Kutokutaja jina inaonesha kua hujiamini na unachokisema.

    Kurejearejea maneno inaonyesha jazba na ukosefu wa elimu ulionao.
    Kutuita wahuni inaonyesha chuki ulizonazo. Kama nakosea basi waombe radhi wazanzibari kwa kuwaita wahuni.

    Ama kuhusu muungano na bunge la tanganyika kuridhia muungano hayo sisi hayatushitui kwani wazanzibari, karume na baraza la mapinduzi hawakutia sign hati ya muungano kwa maana hiyo muungano haupo.

    Nabado kwani hata wazanzibari hatujaiweka madarakani hiyo serikali yetu mambo ni hivyo sijui tukiwa na serikali ya wananchi kamili itakuaje.

    Nakumbuka maneno ya ismail jusa alipowambia watanganyika kua kama wanataka serikali moja tanzania nzima basi labda ije kutawala bahari na miti zanzibar lkn kwa kuwatawala wazanzibari haiwezekani, kwa hiyo mtoa mada maneno unayasikia hayo? Hayo ni maneno ya wazanzibari wote.

    Kama ni uhaini basi kafanya nyerere alipopinga maamuzi ya wabunge wa tanganyika walipopitisha sheria ya serikali tatu. Huwezi tutisha kwa kutuita wahaini ni bora zaid ya uhain lkn tuwe na nchi yetu zanzibar yenye amlaka kamili, na nikaribuni hivi. Wewe endelea kuzubaa halafu uone mungu atakavyokufanya.
    Unajua banaa kujadiliana na watanganyika ni rahisi sana kwani hawajui ispokua kuiba. ZANZIBAR OYEE ZANZIBAR DAIMA. Mungu inusuru zanzibar na kila shari na balaa aamin.

  10. butiama 10/08/2010 kwa 5:19 um ·

    A/A NDUGU WANA UKUMBI WA MZALENDO MLIOCHANGIA MADA HII NAONA MMEPOTEZA MUDA WENU ADHIMU KUCHANGIA MADA HII LAKINI HII MADA HAINA KICHWA WALA MIGUU SIJUI HUYU ALIYEIWASILISHA KWENYE HIYO FORUM YAO ANA UFAHAMU GANI NA MUUNGANO HUU

  11. jaluo 10/08/2010 kwa 5:35 um ·

    A/a
    Mtoa mada naona umetoka ndani ya mstari kwa kuwaita waheshimiwa wawakilishi na wanasheria ambao ni learned profession kuwa ni wahuni.Huna budi kuwaomba radhi.
    Muulize Jaji nyalali na mheshimiwa Jaji Kissanga walivyopendekeza serikali 3 walifanya hivyo kwa nini?nyalali yuko mbele ya haki lakini Jaji Kisanga bado yupo hapo tanzani na juzi tu amepokea pHd yake kutoka Birmingham university
    Pia uliposema baba wa taifa nakunukuu kwamba alisema may god bless us and our brothers in zanzibar and pemba to fulfill this responsibility.Je alimaanisha nini kwanini asiseme neno us tu lakini aliendelea kusema brothers in zanzibar and pemba hiyo pekee inaonesha kwamba tangu mwanzo kuna vitu au nchi tofauti
    Mtoa mada ikiwa shida yako ni umoja wa africa basi umechelewa maana hakuna hata muungano mmoja wa africa
    Nchi za africa zalizojaribu kuungana hazikudumu kwa sababu hizohizo mmoja kutaka kummeza mwenzako na kutokuwa wasafi na kutokusikiliza maoni ya wanasheria eg senegal na gambia.

  12. Bigfather 10/08/2010 kwa 5:43 um ·

    Hayo yalikuwa maneno ya mfamaji kwamaana mfamaji haachi kutapatapa , Zanzibar imeonesha kwamba ni nchi hasa pale ilipoamua kupiga kura ya maoni ya kutafuta ridhaa ya (wananchi wa Zanzibar) na sio Tanzania au labda Tanganyika, hilijambo liko wazi sana wazanzibari wameshaamua ni serekaligani wanataka sasa kama kunamalalamiko juu ya hili nduguzetu wa tanganyika nyinyi mlalamikieni JK ambae ameunga mkono kila hatua ambayo wazanzibari wamechukua , sasa kama kunatatizo ndani ya katiba tunamuomba bwana Pinda asimame tena atuambie jee Zanzibar ni nchi au la. Asanteni.

  13. msafiri 10/08/2010 kwa 6:13 um ·

    A/A warahmatullahi wa barakat. kwanza nnaunga mkono maoni ya ASHAKH ahsante sana Ashakh kwa kuwafahamisha kwanza hawaijui maana ya ZANZIBAR wanasema mungu wabariki nduguzetu wa Zanzibar na Pemba wametutawala miaka mingi lakini mpakaleo hawaijui Zanziba, hawajui kama ZANZIBAR ni Unguja na Pemba, nakama wanatutajia JWTZ kututisha hilo halipo wakati wa kupigana umekwisha, tukotayari kwa lolote na hii ndio itakua Jihadi yetu kwani kupigania nchi ni JIHADI tukotayari kwa lolote, sisi wa ZNZ tunaunga mkono bunge la jamhuri ya watu wa Zanzibar.

  14. ssalumss 10/08/2010 kwa 6:43 um ·

    yote ni hayo yalifikaje kutuita sisi wahuni,sasa inakuwaje nyinyi mnataka kuungana na wahuni!Wazanzibari tulikuwa tumelala lakini Tunamshukuru Mungu kwa kumpa uweze mh. Pinda kutuamsha katika usingizi,si mnasema hatuwezi kujitegemea bala ya bara sasa mnalalamika nini,just tunakuonesheni kuwa tunaweza kufanya hivyo,nawashukuru viongozi wetu wa zanzibar kwa kulishtukia hilo,
    kuja kwetu bara just tumekuja kuwapeni maadili mema maana hamna ustaarabu kama wewe mwandishi ulivyofanya huna ustaarabu kwa kutuita sisi wahaini pmj na viongozi wetu.
    nyinyi endeleeni kuchimba dhahabu,almasi n.k yote sisi hatuna shida navyo. lkn
    sisi tunataka tuchimbe mafuta nyinyi nayo mnataka.
    hapo nyinyi mmezidi na offside.
    I LOVE ZANZIBAR

  15. mumewetu 10/08/2010 kwa 6:59 um ·

    Mtoa mada katupotezea muda kwa kuisoma mada yake ambayo sehemu kubwa imejirudia, hii ni kuonyesha wazi khofu kubwa imewaingia Watanganyika.

    Sisi Wazanzibar USTAARABU umo katika damu zetu, tumezowea kusema “HESHIMA NI KITU CHA BURE” ndio maana tukawa tunawaheshimu wakubwa na wadogo.

    Leo huyu CHOGO anawaita viongozi wetu tuliowachagua WAHUNI hali tunajua kwamba muhuni mkubwa kwa kipindi hichi ni Mizengo Pinda, lakini mimi ninamuambia hii ni rasharasha tu MASIKA yataanzia November mwaka huu, hapo ndio atajulikana nani muhuni.

    MUNGU IBARIKI ZANZIBAR

  16. showayb ali 10/08/2010 kwa 7:06 um ·

    Hii Katiba ya Muungano ni dhahiri kuwa ilikuwa ni Fabrication na wala si katiba ya maridhiano kati ya Zanzibar na tanganyika kufanya Jamhuri ya Muungano. Kama muliitunga nyinyi Wa-Tanganyika basi itawarudia wenyewe. Sisi hatumo, sisi tuanrekebisha Katiba yetu ya Zaznibar.

    Iko wapi Katiba yenu ya Tanganyika? Itafuteni muirekebishe na hakutakuwa na M-zanzibari atakayenyanyua domo lake kuwaambia suuuuuuuu basi nanyinyi muufyate mdomo wenu.

    Kama mumekataa Serkali tatu basi onjeni joto ya jiwe.

    Balahau siye kwenye Serikali moja hamutupeleki ng’oooooooo!

    Hiyo katiba ilitengenezwa kuongoza mazuzu lakini leo hawapo Zanzibar kwani hata ndugu zetu CCM walioko Zanzibar wameukubali uzalendo na kuungana kutokana na Utapeli wa Ki-Tanganyika.

    Jamani munakumbuka wakati Muungano ulipowaweka Afisa wa Polisi ambao wanadaiwa kuwa walikuwa wakishiriki katika wizi wa mali Zanzibar hususan wakati wa Uchaguzi. Basi haya Ujiti na macho.

    Kabla ya Serikali ya Dr Salmin Wa-tanganyika walikuwa wakiingia Zanzibar kwa Karatasi Maalum (Passport ya Zanzibar) baadae Dr salmin akaiondoa, sijui kwa sababu gani lakini huu ni uthibitisho wa Kuwepo kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

    Kuondolewa kwa Passport hiyo ilikuwa ni njama ya kuivamia Zanzibar.

    Wa-zanzibari haturudi nyuma ni kusonga mbele tu.

    Tutazitumia Elimu zetu na Raslimali zetu kuwaelimisha Wa-Zanzibari wa chini mpaka waelewe juu haki yao na waiunge mkono SMZ katika mapambano ya kuikomboa.

  17. makame silima 10/08/2010 kwa 7:26 um ·

    WAZANZIBAR MUNAUJUWA UKOLONI MAMBO LEO? NDIO HUU.HAWA JAMAA WALIPOKAA KTK BUNGE LAO LA TANGANYIKA NA KUFUTA KUFUTA JINA LA TANGANYIKA NA BADAE KULITA JINA LA TANZANIA KUNA MZANZIBAR YOYOTE ALI SHIRIKISHWA KATIKA MAAMUZI HAYO? KAMA YUPO ATUELEZE AU WATANGANYIKA WATUPE USIBITISHO NI NANI.ISPOKUWA NI UJANJA WAKUTAKA KUTUFUNIKA KWA KOTI LA NYERERE NA KUIMEZA ZANZIBAR. NA KAMA TUMEUNGANI NI TANGANYIKA NDIO MSHIRIKA WETU SIO TANZANIA? NA KAMA NI JAMUHURU YA TANZANIA. BASI SISI TUNAJUWA NI REPLICAN OF TANGANYIKA AND ZANZIBAR. NDIO UKAONA BALOZI ZOTE ZA ULIMWENGU ULIO UNGANA UTAONA ZIMEANDIKWA SEREKALI YA WATU WA SOUTH KOREA NA NOUTH KOREA,SENEGAL NA GAMBIA,SHECO AND SLOVAKIA ITC. SASA VIPI SISI TUWE SEREKALI YA WATU WA TANZANIA? INAMANA MUNATUFANYA MAJUHA SISI WAZANZIBAR? TUWE MKOA WA PWANI WAKATI NI NCHI? MUKITULETEA TABU TUTARUDI KTK KURA YA MAONI TUKIKATE HISHI KIDOMA X2 CHA MUUNGANO FAKE HUU MZIZI WA FITNA UFE.

  18. Mtu-wakale 10/08/2010 kwa 7:27 um ·

    Mwishoni mwa miaka 1960 au kati ya mwaka 1966 na 1969 nakumbuka kama leo kuna siku Mzee Karume {marehemu} katika mkutano wa hadhara ambao ulifanyika katika bustani za manispaa ya zanzibar, sasa ni Karume House, alisema “muungano huu usiwababaishe wananchi, maana muungano ni kama KOTI tukiona linatubana tutalivua… Muungano si kitu cha kuwatisha wananchi”. Hayo ndio yalikuwa maneno yake Marehemu mzee Karume.

    Alisema kuwa ikifika miaka kumi faida na hasara za muungano zitaangaliwa ili kujuwa hasara na faida na kama hasara ni kubwa tutalivua KOTE maana litakuwa tayari linatubana, alisisitiza.

    Nyerere {Julius} naye katika uhai wake alisema katika moja ya mikutano yake, sikumbuki mwaka gani lakini, alisema katiba si msaafu. “Katiba inaweza kurekebishwa [kubadilishwa] ama inaweza kuandikwa upya kwa sababu katiba si msahafu..ndio.. ndio.. katiba si msahafu {msaafu}”; Nyerere, alikuwa anasema kwa kutilia mkazo maneno yake. Nadhani ni wakati ule alipokerwa na wabunge walijiita G55.

    Mtoa mada ya hapo juu yuko tofauti na mchakato wa wa marekebisho ya katiba ya Zanzibar, yanayo jadiliwa hivi sasa katika baraza la wawakilishi. Mada yake zaidi inatowa vitisho, dharau na matusi jambo ambalo kwa karne hii ya 21 halikubaliki kabisa.

    Tanzania ni nchi mbili zilizoungana, Tanganyika na Zanzibar, moja imefutwa katika ramani ya dunia kwa makusudi. Zanzibar, ipo bado ndani ya ramani ya dunia. Sitaki nichambue sana sina muda.

    Mtoa mada anasema “hawa wahuni wa Zanzibar, wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyengine”; Unatakiwa kuelewa kuwa Zanzibar, haikutangaza kujitenga wala kuvunja muungano. Na hata hayo marekebisho ya sasa ya katiba ya zanzibar, yanasema kuwa Zanzibar ni nchi kamili ndani ya Tanzania. Hii inaondosha utata na kumuonesha Mizengo Pinda kuwa Wazanzibari si maji yake, akatafute maji yake akoge.

    Wakati huo huo, wewe mtoa mada hapo juu, wacha kujenga fitina na vifungu vyako uchere vya sheria. Zanzibar ina watu wake na viongozi wake, kama huko Bara ni wanaume, leteni hizo pingu za kuwafunga hao wajumbe wa baraza la wawakilishi tuone. Huu ni wakati wa uwazi na ukweli na si kutishana.

    Tanzania bado ni jamhuri ya Muungano. Bado ina mfumo wa Serikali mbili ya Muungano na ya zanzibar. Serikali ya zanzibar, ina mamlaka yake, inaweza kufanya chochote katika katiba yake bila kuingiliwa na Serikali ya muungano almuradi haivunji muungano. Hata hivyo ukifika wakati, ikaonekana muungano sasa basi, ujuwe itakuwa basi na siku hiyo haipo mbali.

  19. obama2 10/08/2010 kwa 8:34 um ·

    ASALAM.
    NDUGU ZANGUNI HUYU JAMA ALOTOA IYO MADA KUSEMA “Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja” MIE NAONA HAWA WATU HAWANA HISHMA WALA BUSARA NA HAWANA HIKMA.WANAHITAJI KUFUNDISHWA ADABU KWANZA.KABLA YA KUELIMISHWA.

  20. mrfroasty 10/08/2010 kwa 8:39 um ·

    Unajua kuna matatizo fulani ambayo wengi wa watu kutoka Tanganyika wanapungukiwa.Kila mtu anakuwa anajivunia utaifa wake na uzalendo wake, lakini kwa bahati mbaya nilisoma utafiti fulani unasema watanzania (watanganyika) ni watu wasio na tabia hii duniani.Sina uhakika ni kwanini, lakini huenda ikawa ni ile dhana ya kuwa Tanganyika ni taifa ambalo mipaka yake ya kuundwa na wakoloni.

    Anyways, long story short naona wengi wenu muna mawazo ya kizamani ya miaka 64 tokea Nyerere alivyokuwa hai akitisha tisha wazanzibari na kuwaita wahaini.Mnasahau kama muda umeshapita na leo tuko karne nyengine kabisa, ambayo ukweli wa mambo wazanzibari wengi hawataki muungano.

    Personally, kama mzanzibari nimefurahi sana na momentum ya siasa za kwetu zinavyokwenda.Yaani ni juzi tuu saturday tumefanya re-union ndogo kufurahia GNU n.k.Hili la katiba kubadilishwa na kuwa nchi, ndio nimezidi kufurahi na naomba M.Mungu aniweke hai nishuhudie taifa langu likiweka tena bendera yake hapo U.N kama ilivyokuwa kabla ya Mhaini Nyerere kuja na wazimu wake.

    Sasa kusema M.Mwanakijiji unanisomea mie katiba ya Tanganyika, halafu ndio mjadala unaanzia na katiba hio naona kama unajisumbua.Maana hio katiba yenyewe ndio msingi wa matatizo haya ..

  21. Bosco 10/08/2010 kwa 9:34 um ·

    Mimi nahisi miongoni mwa sababu za watanganyika kutokujivunia utaifa wao ni;

    (1) tanganyika yenyewe imeuzwa tokea zamani kwa mjerumani. Kwa hivyo hawana taifa kimsingi ispokua wanababaishwa tu wajanja wamesha kula hela tokea zamani.

    (2) wanataka kutumia utaifa na rasilimali za zanzibar kama vile kiti cha zanzibar UN ili na wao wawe na taifa. Wanakhofu kubwa ikiwa zanzibar itavunja muungano wao watakua vipi? Kwani hawajawahi kua na kiti UN na uhuru kamili hawakupata hawa jamaa. Hii tanganyika mpaka leo ni kolony la mjerumani.

    (3) watanganyika karibu 99% ni wajinga wakutupwa hawajui lendalo wala lirudilo je watajua utaifa hawa? Kwani ushawahi kusikia samaki akidai utaifa?. Mimi nimekaa nao sana hawa jamaa hawana mawazo yoyote ya maana labda kuiba,kunywa pombe na uzinzi. Yaani wamekaa kama samaki tu ukiwatilia chambo umewakamata wote hata kwa tsh 500 tu hawaaminiki. Mimi nawahurumia sana lkn sijui hawa watu wamelaaniwa au vipi? Ebwanae hawa watu wanashida sana lkn huwezi jua mpaka utembee vijijini. Na akitokea mtu kutaka kuwasaidia wanamdhalilisha, kwa mfano ali hasan mwinyi alipowatoa kutoka kwenye minyororo ya udhalili wa nyerere, udsm walimchora vikatuni vya uchi,kikwete nae wametoa picha za uchi ktk zeutum na leo hii wanampiga vita, mimi si hisi kama hawa ni binaadamu wa kawaida.

  22. bigbod 10/08/2010 kwa 9:37 um ·

    DUUUU!….INAONESHA HAWA JAMAA WANAFURAHI WAKIONA WA ZNZ HAWAPATANI………..YAANI WAMEANZA KUPOTEZA DIRA …. ZANZIBAR NI NDOGO NA TANGANYIKA NI KUBWA SANA KWA NN HAWA JAMAA WANAINGANGANIA KUNA NINI?

  23. yusuf 11/08/2010 kwa 7:50 mu ·

    S/ALYKUM NDUGU ZANGU WAZANZIBARI GANDI NA MADELA WALIPOKUWA WAKIPIGANIA UHURU WA NCHI ZAO WALIAMBIWA WAHAINI NA MAGAIDI LAKINI WAZALENDO WENZAO WALIWAITA WAKOMBOZI NA MASHUJAA KWA KITENDO HICHO HICHO KWA HIVYO TUMUACHE HUYU MTOWA MADA ASEME ATAKAVYO WAHUNI MAHAINI LAKINI KWETU SISI NI MASHUJAA NA WAKOMBOZI
    TUNAMKUMBUSHA WIMBO MAARUFU WAKIZANZIBARI
    MSEGEJU ANA NGOMBE NA MIMI NA NGOMBE ZANGU
    NA MWAMBIA TUCHANGANE HATAKI
    KWAREHI NA KWENDA ZANGU

  24. ashakh 11/08/2010 kwa 2:22 um ·

    Wazalendo, kwa kiasi tumeweza kujibu mapigo ya tanganyika kwa nyanja zote. Hatuina budi klujipongeza kwa hili.

    Wako waliokuja na matusi wa,ejibiwa kwa matusi, walikuja na dharau wamepewa dharau, kwa werevu wamejibiwa kwa werevu. Kuna mpaka waliodiriki kuwaita magozi, wengine walifikia kuwaita mafudu. Hii yote ni kuonyesha kuwa tuko tayari.

    Sasa lililobaki kwa Watanganyika ni kumtafuta Kikwete na kuanza kumla nyama. Zuri zaidi nyama ya Kikwete angalau ina rangirangi na kwa vile yuko karibu na pwani inakuwa na uchumvi hivyo kuufanya utamu kunogea.

    Kwa upande wetu wazalendo hatua nyengine inahitajika. Tujipange vizuri kuelekea hatua ya pili. Hapa ndugu zetu wanasheria siwakti wa kukaa kimya. Tumeona baadhi yao wamedodosa kwa vijisheria, tunataka tuwatolee vitabu na sio ibara. Hivyo wanasheria wa Kizenj hebu zipitieni hizo katiba na nyinyi mufanye manjonjo yenu. Tunataka tujenge hoja na iso twende kichwa mchungwa.

    Jengine kwa wale wezee wetu hebu tupeni zile kumbukumbu za hotuba za Mzee Karume alizokuwa akizungumzia Muungano. Hapa tunaweza kupata funzo. Japokuwa tayari funzo lipo kwani hakuna hata rais mmoja wa Zanzibar isipokuwa Sh Ali Hasana, ambae hakuutukisa muungano. Hizi za mwanzo ni muhimu sana kuzipata.

    Hatua ya pili ya mashambulizi inahitajika kwa haraka sana. Tuna basi tuwe na kauli moja. Tusijanze kujitafuna midomo, mara serikali tatu. mbili, moja, au tujadili nk.

    Hatua hi ni simple tunataka ridha ya wananchi jee wanautaka muungano au laaa. Wakisema wanautaka ndio tuwaulize tena, haya serikali ngapi au muundo gani. Kinyume chake tutakuwa kama ng’ombe kujinzua ndio kujipinza.

  25. Idriss 12/08/2010 kwa 10:51 mu ·

    Mabadiliko haya yanatoa taswira njema kwa Zanzibar; kwa kutambuliwa kama nchi haina maana kuvunja Muungano. Kilichopo hapa ni kuwa Zanzibar bado imo katika mwevuli wa Muungano; tofauti ni kuwa kwa kuwa ina fursa ya kuendesha mambo yake kama mamlaka yenye serikali kamili, basi ufanisi wa hili ungehitaji mabadiliko kama haya. Tukumbuke kuwa tokea awali Zanzibar ilidhamiria kuwa na Muungano si kufuta jina lake. Tanganyika kwa upande mwengine wameamua kufuta hilo jina na kutumia “mwevuli wetu” wa pamoja; kwa hivyo ikiwa hili lipo tangu awali ubaya wa Zanzibar kuendelea kusimamisha lile jina lake uko wapi? Mbona hatuja ususa Muungano?

Comments are now closed for this article.