Habari

JEE KATIBA YA ZANZIABR NAYO HAIPASI KUJADILIWA NA WANANCHI?

Wakati tunajitayarisha kutoa maoni juu ya katiba mpya ya Tanzania kuna jambo moja ambalo tumeli sahau ni kwamba nalo ni kuhusu katiba ya Zanzibar.
kama lengo la ujio wa katiba mpya ni kuboresha utawala bora ,basi hilo lingeenda sambamba na kubadilishwa kwa katiba ya Zanzibar .Na pia ni fursa pekee kwa wananchi wa Zanziabr nao wakapata kutoa maoni ya katiba yao wanyao itaka.
Hii ingekuwa fursa adhimu kwa wazanzibari nao kuwa na katiba ya nchi yao ambayo wameishiriki katika kuiandika.
Katiba ya sasa imeboreshwa lakini inahitaji mabadiliko muhimu ili kwenda na changamoto nyingi zinazilikabili zanzibar kama taifa.moja ni mstakabali wetu ndani ya muunganno.
ni ukweli usio fichika ya kwamba roots ama mzizi wa uhai wa muungano umeanza kuoza na si mbali mti huu utaanguka…japo wapo watu hawataki lakini sasa wazanzibar wengi hawautaki.
hivyo katiba ya wazanzibar inahitajika ambayo itaweka wazi mambo yafutayo
Dini-katiba ya zanzibar haina budi kutamka wazi kwamba zanzibar ni nchi ya waislam inayoheshemu dini nyengine za raia wake wote,
katiba inatakiwa iweke wazi uwezo wake juu ya masuala ya mipaka na mali zake za asili kama ardhi, bahari,anga na madini pamoja na mafuta na gas
katiba iweke wazi ya kwamba mzanzibar anayo haki ya kuishi popote na kwa kufanya hivyo hakumuondolei urai wake na haki zake za kupata ajira,yeye ama watoto wake,
haki ya kumiliki ardhi iwekwe wazi na ni kwa ajili ya wazanzibari tu
wazanzibar wanao ishi nje ya zanzibar kama hawajakuwa raia wa nchi nyengine wana haki ya kuwa na vitambulisho vya zanzibar
iwekwe wazi ya kwamba zanzibar ni nchi huru aamayo iliingia Kwenye muungano na tanganyika, na ina uhuru wa kujitoa ndani ya muumngano huo kama itaona hakuna maslahi kwa taifa
katiba iweke wazi juu ya kazi za rais na wasaidizi wake
katiba iweke uwezo wa serikali kuomba misaada,kuingia mikataba ,kujiunga na jumuiya yoyote ambayo inaona ni kwa maslahi ya taifa
katiba impe rais uwezo kujadiliana na tanganyika juu na mambo ya muungano
mambo yalio ndani ya muungano ambayo haya kuwa ratified na zanzibar yasitambuliwe kisheria kwamba ni ya muungano.
mambo ya posta,uhamiaji,anga,mawasiliano ya ndege, radio ,simu yasiwe ndani ya muungano,
katiba itoe uwezo wa kuanzishwa kwa banki kuu ya watu wa zanzibar amabyo itakuwa na jukumu lakusimamia uchumi na mambo ya fedah ya zanzibar.
katiba itoe uwezo kwa serikali kuanza mchakato wa kuanzisha fedha yetu.(hili ni lazima kwani tuna endesha uchumi wetu bila ya msaada wa tanganyika na hatuwezi ku control ukuuaji wetu wa uchumi, hatuwezi kuzuia infalation,devaluation ya fedha kwa mfumo wa sasa.
katiba iruhusu zanzibar ijiunge EA Community kama zamanai..na isiwakilishwe na tanganyika.
mengiine changieni.
ila wawakilishi wetu pelekeni hoja hii barazani ili wananchi wa zanzibar nao wajadili na kuibadilisha katiba yetu.

Share: