Habari

JIMBO LA UZINI NA MZALENDO

Kwa hakika ukumbi wa Mzalendo umezidi kujijengea sifa kubwa ya kujadili mambo hasa mambo makubwa makubwa ya nchi ya Zanzibar.

Katika wakati ambao nimefurahi sana na ukumbi huu ni pale ilipotoa habari ya masuala ya ‘wizi wa bahari kuu’ unaotaka kufanywa na Tanganyika kupitia Tibaijuka. Hapa iliwaamsha Wazanzibari wengi tu, na hata BLW walikuwa hawajui sana nini kinaendelea. Na akina sisi ‘vishawishi’ tutakoleza mambo. Shukri lilaah – tumefanikiwa angalau kujua na kufahamu, na huenda akina CCM wale vizuu wakafumbua macho.

Ama hii mada ya CUF-Uzini na ushindi wake NO.3; pia imenifurahisha sana. Nimeingia moyo sana kuona baadhi ya wana-ukumbi kwa hisia zangu ni wakereketwa wa CUF na inawauma -pia wamekubaliana na mimi kuwa ‘CUF lazima ibadilike’ kama taasisi. Si vizuri kama wataganda hapo hapo – kuwa mambo mazuri.

Wengine wamesema mimi ni CUF ? – la hasha. Mimi ninaweza kusema kuwa ‘nilikuwa sympathetic wa CUF) kuanzia 1992-95, na reason moja tu: uzanzibari. Niliona CUF wanakuwa na ajenda ya UZANZIBARI, then nikaona tunaelea katika bahari moja. Ghafla wenzangu hawa walibadilisha mpigo, walianza kuwa na sura ya Ki-CCM CCM, na policy zao zilikuwa hazifahamiki tena mpaka sasa. Mimi sikuwahi kuwa mwanachama wala sitokuwa mwanachama; si CCM – si CUF wala Chadema. Ila kama kitatokezea chama kwa dhati kabisa kitapigania course ya ZANZIBAR — hicho nitajiunga nacho. Lakini iwe kwa dhati na tuwaone hivyo – sio akina Said Soud wa AFP au akina Nassor Ndevu wa TADEA sijui chama gani na gani

Itakavyokuwa Mzalendo inajitahidi sana katika kuchemsha chemsha bongo zetu – inawezekana sana kuwa mawazo yangu hayakubaliki – hilo ninalijua. Lakini ninazo sababu – mimi focus yangu ni moja tu: UKOMBOZI WA ZANZIBAR. Sasa kama nitamuona mtu au chama kinacheza cheza na hili – sikubali – ndio mnaona mizinga hiyo ninairuishia CUF na CCM.

Tuseme mfano mmoja: Maalim Seif (VP1) mpaka sasa ana mawazo mazuri sana juu ya governance na hasa GNU; lakini hawezi kupush zaidi ya uwezo wake. Mfano, ingalikuwa hii GNU ni GNU ya CUF – yaani CUF ndio NO.1 na Maalim seif ndiye angalikuwa Rais, isingalikuwa hivi – let’s say GNU hii ingalikuwa imefanywa na CUF. Lakini tatizo ni kuwa CUF wameingizwa ndani ya GNU, wameingizwa ndani ya nyumba ya watu (ugenini) that’s inakuwa vigumu kw amtu kama Maalim Seif kusukuma agenda au zile ideas alizokuwa nazo kabla ya election.
Mimi namjua vizuri sana Maalim Seif, na nina kaa naye; lakini nina hakina hataki kuniambia tu kuwa ‘amegonga mwamba’. Angalia juzi ametoa hotuba pale Bwawani, juu ya REDET ametoa vision yake juu ya GNU – tena safi kabisa na mustakabali mwema wa Zanzibar.

Lakini ukimtoa Maalim Seif – basi sitaki kusema mengi — funika kombe ……apite. Angalia Juma Duni, wizara ya afya — mpaka leo analia na ICU pale Mnazi Mmoja Hosp. Kweli hosp haina pesa au maskhara tu. Michango iko wapi; vile vifaa vilivyotoelwa misaada iko wapi n.k nk.

Tukirudi katika mada zetu hasa hii ya CUF-Uzini – CUF lazima wafanye kitu kinachoitwa ‘self evaluation’. tena critical sio mchezo mchezo. haya mambo ya complacency ya CUF basi tena. Mimi kama CUF itarudia tena vision/ajenda yake ya Uzanzibari – basi tutakuwa pamoja. Hivi wlaivyo sasa ..NO.NO.NO na pia NO CCM NO CCM.

Share: