Urais Zanzibar:Mpambano wa Dk. Shein, Maalim Seif
- Siasa za Upemba, Unguja nje
- Bilal na Nahodha hoi NEC
Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (kushoto), akisalimiana na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, walipokutana wakati wakijipitisha kusalimia wajumbe wa Halmashauri Kuu makao makuu ya CCM mjini Dodoma jana.
Ilikuwa kama ile methali ya ‘siku njema huonekana asubuhi’ kwa Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, alipowasili Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), jana asubuhi kuhudhuria kikoa cha Kamati Kuu ambacho kilikuwa na kibarua cha kuchekecha wagombea waliojitokeza kuwania kuteuliwa kuwania urais wa Zanzibar, kwani alilakiwa tofauti sana na wajumbe wengine waliojitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein (kushoto), akisalimiana na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, walipokutana wakati wakijipitisha kusalimia wajumbe wa Halmashauri Kuu makao
Dk. Shein ambaye ameibuka kuwa mgombea urais wa Zanzibar baada ya kuwabwaga wenzake wawili kwa kura ndani ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, sasa atapambana na mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, kuomba ridhaa ya Wazanzibari kuingia Ikulu ya Zanzibar katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31, mwaka huu nchini kote.
Dalili njema kwa Dk. Shein zilianza kujitokeza tangu asubuhi baada ya wajumbe wengi wa NEC na hata wa Kamati Kuu kufika mbele ya ofisi za CCM Makao Mkuu kumlaki kwa unyenyekevu mkubwa, makaribisho ambayo akina Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha; Naibu Waziri Kiongozi, Juma Shamhuna na Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk. Gharib Bilal, hawakuyapata licha ya kwamba nao ni viongozi wa kitaifa pia.
Majina ya Dk. Shein, Nahodha na Dk. Bilal ndiyo yalipitishwa na Kamati Kuu kwenda NEC kwa ajili ya kupigiwa kura kumpata mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia chama hicho.
Dk. Shein aliwadondosha Nahodha na Dk. Bilal, kwenye kura zilizopigwa na wajumbe wa NEC, huku akijikusanyia kura 117 dhidi ya kura 54 za Dk. Bilal na kura 33 za Nahodha, ambaye alionekana kuwa chaguo la vijana wengi. Jumla ya kura zote ilikuwa 204.
Ushindi wa Dk. Shein ambaye baadhi ya waasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar juzi walitoa tamko kwamba ndiye kiongozi anayestahili kupokea kijiti kutoka kwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amewafunga mdomo wapinzani wake waliokuwa wanaeneza kuwa alikuwa anabebwa tu na watawala wa Serikali ya Muungano na wale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), huku mwenyewe akiwa hana ngome yoyote ya kisiasa ndani ya CCM.
Kwa ushindi wa jana, sasa Dk. Shein anaingia kwenye kinyang’anyiro cha urais kupambana na mkongwe wa siasa za Zanzibar, Maalim Seif anayerusha karata yake kwa mara ya nne akitafuta ridhaa ya wananchi kuingia Ikulu.
Maalim Seif, akiwa pia ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa SMZ, pamoja na kutokufanikiwa mara tatu kuingia Ikulu, yaani mwaka 1995, 2000 na 2005, akiwa amepambana na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour, mara moja na Karume mara mbili, anaamini kwamba hajawahi kushindwa kwenye uchaguzi huru na wa haki visiwani huko.
Hata hivyo, tofauti na chaguzi zilizotangulia, mwaka huu Maalim Seif anapambana na mwanasiasa kutoka Pemba, kisiwa ambacho ndiko iliko ngome ya CUF, ikijizolea kura na viti vingi vya ubunge na uwakilishi tangu mwaka 1995.
Hisia za Upemba na Unguja safari hii hazitakuwa na nguvu katika uchaguzi wa urais Zanzibar, kwa sababu kwa mara ya kwanza tangu Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, marais wote wa awamu sita, wametoka kisiwa cha Unguja. Kwa yeyote atakayeshinda, Dk. Shein au Maalim Seif, atakuwa ni rais kutoka Pemba.
Marais wa Zanzibar waliotangulia mbali na Amani Karume, ni baba yake mzazi, Abeid Amani Karume; Aboud Jumbe; Ali Hassan Mwinyi; Abdul Wakili na Dk. Salmin Amour.
Kuteuliwa kwa Dk. Shein kuwa mgombea urais wa Zanzibar mbali ya kuleta changamoto ya mpambano wa wagombea kutoka Pemba, na kwa maana hiyo kuwa na uwezekano wa kubadilisha nguvu ya vyama vikuu vya siasa kisiwani Zanzibar, CCM na CUF, pia inaacha kibarua kingine nyuma juu ya nafasi ya Mgombea Mwenza wa Rais Jakaya Kikwete, ambaye anawania kiti cha urais kwa muhula wa pili, lakini bila kupingwa ndani ya chama chake akisubiri kupitishwa na Mkutano Mkuu unaoanza leo mjini Dodoma.
CHANZO: NIPASHE
Zanzibar ni Shein, BILAL, NAHODHA SI RIZIKI

Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein, akipunga mkono kusalimia wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na wanachama wengine mjini Dodoma jana, mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Makao Makuu ya CCM maarujfu kama 'White House'. Dk Shein jana alipitishwa kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho.
MBIO za urais wa Zanzibar ndani ya CCM zilifikia ukingoni jana wakati Makamu wa Rais, Dk Ali Mohamed Shein alipopoibuka na ushindi wa kishindo, akimbwaga mpinzani aliyeonekana kuwa wa karibu, Dk Mohamed Gharib Bilal. Dk Shein, ambaye amekuwa makamu wa rais tangu mwaka 2001 baada ya Dk Omar Juma kufariki, alikusanya kura 117 za wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM iliyokutana mjini hapa jana na kumuacha mbali Dk Bilal ambaye alipata kura 54, ambazo ni takriban nusu ya kura alizopata mshindi.
Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha alishika mkia katika majina matatu yaliyopelekwa na kamati kuu ya CCM iliyokutana jana asubuhi na kumaliza kikao chake mchana. Nahodha, ambaye alikuwa na umri mdogo kulinganisha na wagombea wenzake wawili, aliambulia kura 33 tu.
Dk Bilal na Nahodha walikubaliana na matokeo hayo na kutangaza kumuunga mkono Dk Shein, ambaye sasa anatakiwa kujiandaa kwa mpambano mkali dhidi ya chama kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar, CUF, ambacho kimeshamteua mwanasiasa mkongwe, Seif Sharrif Hamad kuwania kiti hicho kwa mara ya nne baada ya kuangushwa na Dk Salmin Amour mwaka 1995 na baadaye Rais Amani Abeid Karume mwaka 2000 na 2005.
Kumalizika kwa mchakato huo kunaifanya CCM sasa itue mzigo ulioonekana mzito na itamalizia shughuli za kujiweka sawa kwa uchaguzi mkuu wakati wa mkutano wake mkuu uliopangwa kufanyika leo na kesho kushughulikia mambo mablimbali, ikiwa ni pamoja na kumbariki Rais Jakaya Kikwete kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano.
Harakati za kumpata mgombea wa CCM zilitawaliwa na kila aina ya kampeni, huku Dk Shein akikumbana na rafu hata kabla ya kuja Dodoma baada ya baadhi ya watu kusambaza vipeperushi vilivyokuwa na maandishi yanayohoji uhalali wake wa kusimamishwa na chama kuwania urais.
Dk Shein alidaiwa kuwa hakujiandikisha kupiga kura Zanzibar na hajaishi visiwani humo kwa miezi 36 mfulululizo na hivyo kupoteza sifa ya kuwa mgombea. Hata kabla ya kutulia kwa tuhuma hizo, habari zilienea mjini hapa kuwa makamu huyo wa rais aliwasilisha barua ya kujiengua kwenye kinyang’anyiro hicho.
Lakini jana, Dk Shein alionekana kuwa mtu anayejiamini na alisalimiana na wajumbe wengi waliokuwa eneo la majengo ya ofisi za makao makuu ya CCM, akionekana kutaka kura za kila mjumbe, wakiwemo wauzaji wa nguo za chama hicho ambao hufanya shughuli za nje ya ofisi hizo.
Aliwasili kwenye viwanja hivyo majira ya saa 4:25 asubuhi akiwa na ulinzi mkali na alilakiwa na baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Baada ya kusalimiana na baadhi ya wajumbe na viongozi wa CCM, Dk Shein aliyeonekana kujaa tabasamu, alienda moja kwa moja kwa wanachama na wajumbe wa CCM wa mikoa mbalimbali na kuwasalimia kwa kuwapa mkono.
Kitendo hicho cha Dk Shein kilivuta hisia za wanaCCM wengi ambao walianza kumkimbilia, kujipanga na kusubiri mkono wake.
Lakini Dk Bilal, ambaye awali alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuteuliwa kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho baada ya kufanya vizuri mwaka 2000, alionekana kutokuwa katika hali ya kawaida na mara baada ya kutua kwenye viwanja hivyo aliingia ndani moja kwa moja na baadaye kutoka nje na kuelekea kwenye gari kabla ya kurudi ndani bila ya kuzungumza na mtu yeyote.
Baada ya kushuka kwenye gari, Dk Bilal Bilal aliinua kofia yake ya CCM na kuishusha kuangalia waliopo eneo hilo kuingia moja kwa moja kwenye ukumbi wa mikutano.
Balozi Ali Karume, ambaye ni mdogo wa rais wa Zanzibar, ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingia kwenye viwanja hivyo na alipishana na Dk Shein kwa takriban dakika tatu tu.
Balozi Karume aliwasili viwanjani hapo akisindikizwa na wapambe wake, mkewe na baadhi ya wanafamilia waliovalia sare za CCM. Alisalimiana na baadhi ya wazee wa CCM, akiwamo Dk Shein ambaye alimfuatia.
Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha aliingia baada ya Dk Shein na kupokewa kwa bashasha na vijana wa CCM. Baada ya kusalimiana na baadhi ya wazee, Vuai alienda moja kwa moja kuwapa mkono wanachama waliokusanyika kumsubiri.
Kitendo chake kiliibua shangwe kwa wajumbe na watu wengine ambao walimwimbia nyimbo za kumsifu wakati akisalimiana na watu waliokuwepo kwenye viwanja hivyo.
Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shemhuna aliwasili saa 5:08 akifuatiwa na Mohammed Raza na baadaye Mohammed Yusuph Mshamba aliyeingia moja kwa moja mkutanoni na kutoka baadaye kuonana na waandishi wa habari akiidokeza Mwananchi kuwa ana matarajio ya kuteuliwa.
Haroun Suleiman, ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, aliwasili eneo hilo lakini muda mfupi baadaye, aliondoka. Hata hivyo, wagombea Mohammed Aboud ambaye ni Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Omar Sheha hawakuonekana katika viwanja hivyo.
Mji wa Dodoma na viunga vyake ulifurika wanachama wa CCM ambao wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu utakaompitisha mgombea urais wa chama hicho kesho.
Ujio wa watu hao umefanya nyumba nyingi za kulala wageni kufurika na watu wengi kukosa mahala pa kulala jambo ambalo pia lilisababisha msuguano baina ya wamiliki wa nyumba hizo na wateja ambao awali walikubaliana kwamba wangehama kuwapisha wajumbe hao.
Awali kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika jana mjini hapa kilipitisha majina matatu kati ya 11 walioomba kugombea urais wa Zanzibar.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alitangaza majina hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kikao hicho cha kamati kuu
Mwananchi
Sheni apeta
na Martin Malera, Dodoma
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemtua Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, kuwa mgombea urais wa Zanzibar.
Katika mchuaano huo uliohusisha wagombea 11 wa awali, baada ya mchujo wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu jana mjini Dodoma, walibaki watatu: Dk. Shein, Dk. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha.
Dk. Shein aliwaangusha washindani wenzake wawili kwa mbali, kwani alipata kura 117, Bilal akaambulia kura 54 na Naodha akapata 33.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Zanzibar kumpata mgombea urais kutoka Pemba tangu uhuru na mapinduzi mwaka 1964.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, alisema kura zilizopigwa zilikuwa 204.
Alisema: “Nahodha bado ni kijana sana, Zanzibar itamhitaji na taifa litamhitaji; Bilali ni kiongozi mzoefu taifa litamhitaji na Zanzibar itamhitaji, wamekosa hili mengine yapo.”
Dk. Shein alisema iwapo atashinda atafanya kazi kuhakikisha analinda umoja, utulivu na amani na kamwe hataiongoza Zanzibar kwa kishindo.
“Imani mliyonipa wajumbe ni kubwa sana, imenitia moyo sana, nitashirikiana na wenzangu 11 kuhakikisha tunapata ushindi wa kishindo, lakini neno kubwa nitandeleza umoja, utulivu na amani na kamwe sitaongoza Zanzibar kwa kishindo,” alisema.
Wakati Dk. Shein akitoa hotuba fupi, meza kuu iliyokuwa na Rais Kikwete, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na wajumbe wengine wa NEC walikuwa wakipiga meza kushangalia.
Mara baada ya matokeo kutangazwa, wajumbe wote hasa kutoka Zanzibar, walilipuka kwa shangwe na nyimbo za kumpongeza Dk. Shein huku wengine wakisema Zanzibar imepata kiongozi safi.
Sasa mchuano mkali utabaki kati ya Dk. Shein na mgombea wa upinzani, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, ambaye naye anatoka kisiwa cha Pemba.
Jana asubuhi Kamati Kuu (CC) iliteua majina matatu Dk. Shein, Nahodha na Dk. Ghalib Bilal.
Majina hayo ndiyo yaliyowasilishwa kwenye kikao cha NEC.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dk. Bilal kufika hatua hiyo kwani mara zote mbili alizowahi kugombea mwaka 2000 na mwaka 2005, jina lake lilikuwa likiishia kwenye kikao cha Kamati Kuu.
Kwa hatua hiyo, bado mchuano mkali uko kwa Dk. Bilal na Dk Shein wenye washabiki wengi visiwani Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo, wagombea tisa miongoni mwa 11 walioomba kuteuliwa, walitinga katika viwanja vya ukumbi wa White House kwa staili ya aina yake.
Mgombea aliyeanza kuonekana nje ya ofisi za CCM ni Balozi Ali Abeid Karume, aliyefuatana na familia yake.
Balozi Karume alionekana akizunguka katika maeneo tofauti, huku akiwa amezungukwa na wanafamilia wake.
Muda mfupi baadaye aliwasili Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohemed Shein ambaye alipokewa na viongozi waandamizi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), wakiwemo baadhi ya mawaziri.
Dk. Shein aliamsha shamra shamra baada ya kwenda moja kwa moja mahali walipokuwa wamekaa mamia ya wanachama na wafuasi wa CCM kutoka Zanzibar ambao walilazimika kusimama na kusalimiana naye huku wakiimba nyimbo za kumpongeza.
Sababu kubwa iliyofanya Dk. Shein ashangiliwe kwa nguvu ni kutokana na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari jana kuwa Makamu huyo wa Rais, amejitoa katika kinyang’anyiro hicho.
Dk. Shein aliyeonekana kuwa mwenye furaha, alizungumza na kucheka mara kwa mara na Wazanzibar hao na watu wengine waliokuwa katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM, huku akiwaambia kuwa hajajitoa kuwania kiti hicho.
Pia alikwenda hadi eneo la nje ambapo kuna wafanyabiashara wanaouza bidhaa mbalimbali zenye nembo ya CCM na kusalimiana nao kwa kuwashika mikono mmoja baada ya mwingine.
Kisha alirejea na kwenda hadi jengo la White House, palipofanyika kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama hicho.
Wakati Dk Shein akirejea kuzungumza na wana-CCM hao na kuelekea White House, alikutana na Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, wakasalimiana na kubadilisha mawazo kwa muda usiozidi dakika tatu.
Hata hivyo, Dk Shein aliendelea kuekelea White House wakati Nahodha alikwenda kuzungumza na wana-CCM waliokutana na Dk Shein.
Tofauti na ilivyokuwa kwa Dk Shein ambapo shamra shamra zilionekana kwa watu wote, Nahodha alishangiliwa kwa vigelegele hasa kutoka kwa kundi la vijana wa CCM waliokuwepo katika viwanja vya Makao Makao ya chama hicho.
Vijana hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali ikiwemo iliyosema “wapende wasipende ni wewe tu.”
Nahodha alihitimisha `ziara’ hiyo na kuelekea kwenye ukumbi wa White House.
Hatua ya kuzunguka na kuzungumza na wana-CCM iliyofikiwa na Dk Shein na Naohodha, ilimstua Balozi Karume ambaye pia alianza kufanya kama walivyofanya watangulizi wake hao.
Lakini kilichokuwa tofauti na Dk Shein na Nahodha, wana-CCM walionekana kumpa mikono pasipo kushangilia, badala yake wanafamilia wake walionekana wakipiga makofi pasipo kuungwa mkono na Wazanzibar wenzao.
Kisha ilikuwa zamu ya Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar, Dk Ghalib Bilal, aliyefika Makao Makuu ya CCM na kuingia moja kwa moja kwenye ukumbi wa White House.
Dk Bilal alishuka kutoka katika gari lenye namba T 887 ABR, akavua kofia na kupunga mkono kuelekea mahali walipokuwa waandishi wa habari, wapiga picha na maofisa wa usalama, huku akionekana kutokuwa mwenye furaha.
Hakutaka kusalimiana na watu kama walivyofanya watangulizi wake na kuingia moja kwa moja ukumbini, huku baadhi ya watu waliotarajia ujio wake wakihoji kama alishaingia au la.
Kisha aliwasili Naibu Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Ali Juma Shamhuna, ambaye alitembea kwa ukakamavu, akitabasamu na kupunga mikono kwenda kuwasalimu wanachama na wafuasi wa CCM kutoka Zanzibar.
Hata hivyo, tofauti na Dk. Shein na Nahodha waliokuwa wakipeana mikono na wafuasi hao, Shamhuna alikuwa akiwapungia mikono na kushikana na wachache.
Baada ya Shamhuna, ilikuwa zamu mfanyabiashara maarufu Mohammed Raza ambaye hakwenda kuwasalimia wanachama wa CCM, badala yake alionekana kuzungumza na watu waliokuwa katika viwanja hivyo, huku akionekana dhahiri kukata tamaa.
Kisha aliingia Yusuph Mohamed Mshamba ambaye hakupata mapokezi, badala yake alikwenda moja kwa moja kwenye ukumbi wa White House.
Ujio wa Mshamba hakuwa na bashasha kutokana na wengi kutomfahamu nay eye mwenyewe kutoonyesha makeke.
Alipofika katika mlango mkubwa wa kuingia ukumbini humo, wapiga picha kutoka vyombo vya habari walimuomba asimame ili kumpiga picha.
Mshamba alitii ombi hilo na kusimama kwa takribani dakika moja huku akipigwa picha.
Hatimaye aliingia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar, Haruna Ali Suleiman, akiwa kwenye gari lenye namba STK 2229.
Suleiman alikwenda kuwasalimia wanachama na wafuasi wa CCM kutoka Zanzibar, kisha aliingia kwenye ukumbi wa White House.
Kamati Kuu ya CCM ilikutana jana kuanzia saa sita mchana, ambapo ilitarajiwa kujadili majina ya wanaotaka kugombea urais wa Zanzibar, kisha kupendekeza majina matatu yatakayowasilishwa kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM.
tzdaima
Ni Dk Shein, Pemba yaweka historia
ZANZIBAR imejiwekea historia mpya ya kisiasa baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumchagua Dk Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wake katika Uchaguzi Mkuu baadaye
mwaka huu.
Kuchaguliwa kwa Shein kunamaanisha kwamba, kwa mara ya kwanza, Rais wa Zanzibar atatoka Pemba.
Dk Shein ni mzaliwa wa Pemba, mpinzani wake katika uchaguzi Mkuu ujao, Maalim Seif Sharif Hamad pia ni kazaliwa kisiwani humo.
Mmoja kati yao ana uhakika wa kumrithi Rais Amani Abeid Karume ambaye anamaliza muhula wake wa pili wa uongozi wa Zanzibar akiwa Rais wa Awamu ya Sita.
Tambo, shutuma na mikikimikiki ya kinyang’anyiro cha kuchaguliwa kubeba bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu Zanzibar, jana zilifikia ukingoni kwa wajumbe 117 wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kati ya 204 kumkubali Dk. Shein kuwawakilisha.
Katika uchaguzi huo, Waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal alipata kura 54 huku Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha akipata kura 33.
Kazi inayobaki sasa ni kwa wafuasi wa vyama hivyo viwili vyenye ushindani mkubwa visiwani kujipanga na kuendesha kampeni za kistaarabu muda utakapowadia, ili hatimaye wananchi wampe ridhaa mmojawapo kuiongoza Zanzibar kwa miaka mitano.
Kuchaguliwa kwa Shein kugombea urais pamoja na Maalim Seif pengine kutapokewa kwa faraja kuu na wakazi wa Pemba ambao kwa muda mrefu kilio chao kimekuwa ni kutoa rais wa Zanzibar.
Hiyo inatokana na ukweli kwamba, Shein na Maalim Seif wote ni wazaliwa wa Pemba na hivyo utakuwa sasa ni uamuzi wa wananchi kuona ni nani atawafaa katika kuwaongoza, lakini pia pengine ni faraja zaidi kwani wote wanaunga mkono maridhiano ya CCM na CUF.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Shein aliwashukuru Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wote wa NEC kwa kuonesha imani kwake na kuomba ushirikiano kwa wenzake
katika kupata ushindi wa kishindo.
Aliwashukuru pia wagombea wenzake 10 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo pamoja na wawili walioingia katika hatua ya mwisho ya kupigiwa kura na kupatikana yeye mshindi.
Alisema wote walikuwa na vigezo sawa, ambapo pia aliahidi kuchota hekima na busara kwa viongozi wastaafu waliomtangulia katika kuivusha Zanzibar endapo atachaguliwa hatimaye
kuwa Rais wa saba.
Kwa kupatikana kwa mgombea huyo wa Zanzibar, CCM leo itaanza Mkutano Mkuu wake huku ikiwa tayari na wagombea wake wawili katika nafasi ya urais.
Rais Kikwete ni mgombea pekee wa nafasi hiyo kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na atapigiwa kura kesho kama Katiba ya CCM inavyoelekeza.
Rais Kikwete alijitokeza peke yake kuwania nafasi hiyo katika siku ya kwanza ya uchukuaji fomu Juni 21, mwaka huu na hadi kufikia siku ya mwisho ya kurejesha fomu, Julai mosi, alikuwa mgombea pekee wa urais.
Kwa hiyo, kesho anatarajiwa kupigiwa kura ya Ndiyo au Hapana na wajumbe 1,968 wa mkutano huo kwenye ukumbi wa Kizota nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
Rais Kikwete anatarajiwa kupata kura za kishindo kwa sababu tayari wajumbe wengi wa mkutano huo wameeleza kuridhishwa kwao na jinsi Serikali ya Awamu ya Nne chini ya uongozi wake, ilivyofanya kazi katika miaka mitano inayomalizika.
Hata mabango ya CCM yaliyoupamba Mji wa Dodoma hivi sasa yanaeleza kila kitu kuhusu hilo, kwani madogo kwa makubwa yenye picha ya Rais Kikwete akiwa na fulana ya kijani,
yana ujumbe usemao, “Chaguo letu ni Kikwete.”
Baada ya Rais Kikwete kupigiwa kura na kuchaguliwa kusimama tena kuwania muhula wa pili na wa mwisho, anatarajiwa kumtangaza mgombea mwenza wake baada ya kuanza kufanya kikao na Kamati Kuu.
Majina kadhaa yametajwa kuwania nafasi hiyo yakiwemo ya Dk. Salim Ahmed Salim, Zakia Meghji, Muhammed Seif Khatib na Nahodha na Shein waliokuwa katika kinyang’anyiro cha
urais wa Zanzibar jana.
Mkutano Mkuu huo wa CCM ambao wajumbe wake wengi tayari wako mjini hapa, unatarajiwa kupokea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2005/10.
Kazi ya kuwasilisha utekelezaji huo wa Ilani itafanywa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa upande wa Serikali ya Muungano na Nahodha kwa upande wa SMZ.
Serikali ya CCM imeeleza kwamba utekelezaji wa Ilani hiyo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta mbalimbali, jambo ambalo hata Rais Kikwete alilielezea siku alipochukua fomu
ya kuwania tena urais.
Rais Kikwete alisema anaamini ametekeleza ipasavyo Ilani hiyo na sasa anaomba atumwe tena kufanya kazi hiyo na kuahidi kuwa akichaguliwa tena, atawatumikia Watanzania kwa
Ari Zaidi, Nguvu Zaidi na Kasi Zaidi.
habari leo


Kwangu hizi si sad news hata kidogo.Hakuna tofauti ya wengine na Dr Shein wote ni CCM na ndio walitufikisha hapa tulipo.Angalau HIYO NEC imefanya jambo la maana kuondoa ule mwiko uliojengeka kuwa CCM haiwezi kutoa mgombea urais kutoka Pemba.
Nimeimove hio habari kwenda kwenye “Tetezi” kwa maana hio habari haijakuwa confirmed ni kidokezo tuu.Habari kamili tuvute subra kidogo…
Na wale walio Zanzibar watupashe yaliojiri.
mia chini ya mia
Wembe ni ule ule
Sasa ni saa 4:30 usiku huko nyumbani, kikao si kimekwisha? Tupeni habari za uhakika basii
sahihisho sheni kapata kura 117,bilal 54,shamsi 33
ommykiss, wembe ni ule ule upi? ua umekusudia alionyolewa Bilal mwaka 2000?
Kwanini ziwe Sad news? Si tunataka maridhiano na huyu Dr Shein kama kapita kweli si tunaambiwa yeye yupo tayari kwa hali na mali kuhakikisha Maridhiano yanafikia malengo yake ya kuwa kitu kimoja na kuondosha tafauti zetu za kijinga jinga ambazo zishapitwa na wakati.
wallahi sasa ndo watajua kama hichi chama kina wenyewe na wako dodoma sio zanzibar. poleni sana watu wa kisonge
mbwa kumtafuna mbwa mweziwe siajabu mgombe kumpiga mweziwe sishangai mzuzi kumbada mamaye nikawaida punda kutowa utupu wake hatharani nifahari kwake mchawi kumuuwa kakaye si viroja habari ndohiyo ccm wote sawa ukiwa mwehu au kichaa ukiwa kibaraka au bwana wote sawa kwangu mimi sheni nahoza bilali chungu kimoja ,hasara kwawazanzibar EWE MOLA TWAKUOMBA TUNUSURU NA MAHASINI WA NCHI YAONA MALIZAO NA WATOTOWAO
Sioni kuwa ni SAD NEWS. Bado nawaza ikiwa Bilal atapita Kisonge itafanya nini? Pia ikiwa hakupita Kisonge itasema nini?
Nimesikitishwa sana na namna ndugu zetu walivyoufanya huu uteuzi na ulikuwa unanitia wasiwasi. Binafsi niko 50-50 kwa Bilal lakini maneno na vitendo vya Kisongeo niliona hakutakuwa na Salama.
Ikiwa hii taarifa ni ya ukweli sasa ni kumsikiliza Shein atatwambia nini sisi wananchi. Tukumbuke yale aliyokuwa akisema akiwambia CCM kwani Halmashauri kuu ndio iliyomchagua. Baadae ndio anakuja kwetu wananchi ili tuweze kumchagua. Tutege macho na masikio kusikiliza kitu gani atatwambia, huku akili zetu zikiwa makini kupima kile anachotwambia.
@Muunguja
Hongera sana kwa usahihi wako. Najuwa uko jikoni hivi ndio tunavyo wataka watu kama nyinyi. Nakuomba tafadhali tuongeze, sio utupe utandu tu. Wengine njaa zetu kubwa, atleast tupate tushibe.
Kuna principle isemayo usitowe ultimatum kuwa ukifanya “x” basi mimi nitafanya “y”, mpaka uwe una hakika kuwa huyo unaemwambia kama atafanya hiyo x, na wewe kweli una uwezo wa kukamilisha vitisho vyako.
Sasa nataka niwaone hao akina Baraka Shamte na maskan ya Kisonge kama wanaume kweli, wafanye hayo waliyosema watafanya kama Bilali hakupitishwa.
Hasira ya Mkizi faida ya mvuvi.
Kutoka Makamo wa Jamhuri ya Muungano hadi Makamo wa Zanzibar. Hongera Dr. Shein.
Dr. Bilal — jamani nyinyi mlioko majuu naomba muunganisheni na Mahmoud Ahmadinejad aende Qum kuongeza nguvu ktk ile mitambo ya nyuklia. Wanamaskani kaka Kisonge msiwe na wasiwasi Maalim Seif hazikatai kura zenu na atawatumikia wazanzibar wote bila ubaguzi.
A a,wanaukumbi,kwanza namtakia kilalagheri MH SHEIN,sasa znz imefungua ukurasa mpya,makundi sasa basi na yasipewe nafasitena,mwisho wamaji nitope,lamuhimu sasa wanzanzibar tujenge umoja wetu, kusiwepo kulaumiana na kusutana ,nahakuna mshindi mshindi ni mzanzibar,tusahauni yaliopita tugange yajayo, tunakuomba ALLAH, SHEIN AWE KIONGOZI WA UMA
Kwa kusema hapa wazanzibar tunapata somo kwa wenye kuelewa kuwa siasa ya chuki na ubaguzi usio na shina wala kilele umepitwa na wakati.sasa ni wakati wazanzibar wenzangu wa kuwaangalia wagombea wetu wa vyama vyote ni yupi mwenye uchungu na hii nchi yetu na mwenye imani na wazanzibari.
jamani tuwe makini tusije kumpa kura kiongozi ambae hana imani na zanzibar yetu wala wazanzibari wenyewe hawajali.
pia nachukua nafasi hii kumponngeza ndugu sheni kwa kupata nafasi ya kugombea urais wa zanzibar na tunamuomba kuunga mkono yale aliyoyakuta yaloanzishwa na maalim seif na dk amani karume pia ni matarijio yangu kuwa ni mtu atakaehimiza free and fair election nchini.
mungu ibarike zanzibar na watu wake
aamin
eeeeeeh zanzibar dah jina lake taamu lakini mambo yanayoikumba mungu labda atuletee mtume mussa aikate bahari tutokee marekani
Naungana na Muarab, tunaomba vyama vyetu vyote vifanye kampeni za salama. Pia tume ya uchaguzi itayarishe mazingira ya kufanyika kwa uchaguzi wa huru na haki.
Mwisho ni vyama vyote kukubali matokeo. Ikiwa CUF imeshindwa, imeibiwa, au imepokonywa, nawao wanahaki ya kufungua ukurasa mpya wa kusema “TUMEKUBALI TUMESHINDWA”. Kwa upande wao CCM ikiwa hesabu ndio zimekwenda mchomo pia nawao waseme “HONGERA!! TUMESHINDWA”
Huu ndio msingi wa ujenzi wa Zaninzibar mpya. Vilevile ndio kuepukana na zile siasa za kuchuki au kuleta misiguano.
halfu nyinyi mnaonekana ni wepesi wa kusahau kwani jama aliyepewa jina la abdulla na wezee wake na akajipiga kwajina la jakaya alipoahidi kuwa atamlinda kaka yake Amani mlifikiri anatani saleo live ZNZ surs mbayaaaa mlilieni mamaenu ASP wajinga ndio waliwao na werevu mtakula nini? asante sana
Kwangu mie sioni baya lolote kwa kuchaguliwa Shein na baraza kuu la CCM.Na bado nimeona ni kheri kubwa sana!!nimesema hivi kwa kuelewa tena kwa siku nyingi sana kuwa ndani ya chama cha CCM kuna matabaka ya killa aina!!khasa hapo kwetu Zanzibar!!kuna wale ambao wanajiona kuwa wamezaliwa ndani ya chama na kujukuu, kwahivyo wana haki zaidi kuliko mwengine yoyote!! kuna na wale sisi tumepinduwa, kwahivyo mtu yoyote mwengine huwa kwao hana haki yoyote hata kama mwenzao wenyewe!!haya si ya kuzuwa, ni ya kweli na wenyewe wanayajuwa sawa sawa!!na ndio kwa maana zikatoka kauli za kusema kuwa [ kama hakuchaguliwa Bilali hakukaliki safari hii, safari hii zamu yetu] Ingekuwa kuna mshikamano wa kweli zisingesikizana kauli kama hizi za kijinga ambazo zinapalilia chuki na uhasama baina ya jamii ya Wazanzibari wenyewe kwa wenyewe!!tukizisikia zamani kauli za chuki pia kusema kuwa Mpemba hatawali Zanzibar!! kauli hii akiambiwa Maalim Seif Shareef kama kwamba si Mzanzbari mwenzao!! Sasa hii kutokea kuchaguliwa Shein kuwa ndie chaguo la chama huko Dodoma na kuwa yeye pia ni kutoka Pemba!! itavunja ule mzizi wa fitina na chuki za wamaskani kujilabi kwa kauli ovu kama hizi kuwa hawakusikilizwa!! Sasa kama kweli CCM ina wenyewe Zanzibar, basinatujionee hao maskani watafanya nini baada ya tokeo hili!! wako waliotamka kuwa watairudisha ASP yao, wako waliosema kuwa watajienguwa CCM na kujiunga na vyama au kufunguwa chama chengine na kadhalika!! lakini haya hayawafalii chochote!! na wala hawawezi kufanya jambo lolote kinyume na chama chao!!kilichobaki ni kidomodomo tu hakifalii lolote!! wanasahau kwamba wakati sasa umebadilika na watu wamechoka kufarakanishwa kwa siasa za chuki na ukhasama!! Natuwaone kama wana ubavu wa kususia chama chao kama kweli wana uwezo huo!!yanini kuandikia mate na wino upooo ?????
ASALAM,
Hongera Dr Shein kwa kuchaguliwa kua kiongozi kama habari hii ni ya kweli.
Kwavyovyote vile alochaguliwa na CCM kua mgombea uras kwa Zanzibar basi huyo atakua kiongozi wetu, kwavile Wazanzibari ndio sisi,na haswa kama kura ya maoni itakubali kuunga serekali ya umoja wa kizanzibari.
Kwani ni matarajio Rais Atakua Maalim Seif au atakua Mr Shein na hao ndio viongozi watakaotuwakilisha Wazanji,nimuhimu na niwajibu wetu wananchi kuwapa ushirikiano ili kuivuusha nchi yetu na kuiweka pazuri zaidi ya ilipo sasa.
Lakini pia ni muhimu na niwajibu pia kwao viongozi wetu kutumikia wana nchi bila ya upendeleo wowote wakichama au kiuzawa.
Naitakia kila la kheri zanzibar yetu na wa Wananchi wake katika kufungua ukurasa mpya wa kufukuzia maendeleo yalotukimbia kwa masafa marefu.
sasa ni wakati mpya tunahitaji mawazo mapya,viongozi wenye fira mpya za kiuzalendo.
Asanteni.
WanaMzalendo, nikweli CCM ni CCM may be there will be not management change! But lets hope for the best at least the card has been shifted the otherside. Also, it is said that Dr Shein is supporting the so called’Maelewano’between the Zanzibar Revolusionary Government President Dr Aman A. Karume and Civic United Front General Secreatary Maalim Seif Sharif Hamad. In anyway we need to be very carefully as CCM are always dynamic. So they may be positively to develop this ‘Maelewano’ or otherwise. However, let ray for the best.
Again lets come back to Kisonge group; what will they do with Baraka Shamte? Will they return there CCM membership cards? To my knowledge Kisonge propagandas has significantly affect Bilalto win because they make themselves as speaker of CCM members. Very unfortunately they didn’t imagine themselves as nothing to CCM. CCM can proceeds without Kisonge but will Kisonge survive without CCM?. If really Kisonge is confident and have support from other CCM members as they claimed, we want them to see to do what they have said earlier as Bilal has been kicked off. Free advice to Bilal, you are my teacher your old enough; please take a rest and ask forgiveness from Zanzibaris and ‘Allah’ because as the Chief Minister in the Kamando regime you run the ran the Government badly…..
Nimeconfirm kama ni news ya uhakika.Hii habari imeondoshwa kwenye Tetezi na kuwa habari kamili.
MZALENDO tutafanya polls maalum kwa ajili ya kumchagua rais wa Zanzibar.Wazalendo wanaombwa wapige kura zao kuonesha ulimwengu nani anakubalika na MZALENDO kama ni rais wa Zanzibar.
Hayo ya mgombea yashamaliza, waliopenda haya walionuna wanakaribshwa kujiunga na vyama vyengine.Kisonge mnakaribishwa kujiunga na upinzani au kuanzisha chama chengine cha siasa kama hamujaridhika na mwenendo wa Dudumaa.
Kila la kheri
Zanzibar njeeemaaa na itazidi kua njema mimi ulingo wa siasa sijawahi kuwemo na haswa ninavowaona watu na ubinafsi kuwatawala hakuna mmoja anoshangiria bila ya kujali maslahi yake binafsi na uzawa wake si ccm si kafu ni waunguja si wapemba… sipo sijayaona zaidi ya recodi mbili tatu ila wapemba jamani waachieni watawale alau muone kutakua na uongozi wa aina gani kwani mpemba ssi ntu??
ila na nyie mliotoa pongezi nyiiingi hapa msidhani kama watu wapumbavu hawajui kiini cha furaha yenu, na hao walioishia kusema punda na uchi wake ndo yanayokataliwa mpemba anapopewa kitu inakua watu hawalala nasema hivi kwa kujua wenyewe mnajijua zaidi
hata hivo inapendeza namna inavoonyesha kua mko tayari nyote kumuunga mkono Sheni hata kama kitakachoshinda ni ccm na kuonyesha kuwa tayari kumpa mashirikiano kuipeleka Zanzibar mbele bila ya kujali chama atokacho, ingawa sina hakika kama hili linaashiria kinachojaliwa ni uunguja na upemba zaidi kuliko u CUF au u CCM, na sijui ndio maana Juma Duni kamwe hatopewa nafasi ya Seif (yaliyokuwepo Dodoma na kwengine yapo) au ni kwasababu ya hizo nyadhifa zilizoahidiwa zinopambwa kwa jina la serikali ya “umoja”/”maridhiano” na ikiwa sio hivo hili joto la pongezi nawaomba wazinzibari woote walionyeshe iwapo sheni akishinda lakini kura ya maoni isipopita hapo nitaamini kweli pongezi hizi ni za kikweli kweli
Kusema ukweli mimi nnamini wapemba watendaji zaidi, huyo sheni mimimmoja wapo nikimuombea kutokana na uelewa wake na ustarabu alionao, dini na vitu vingi vyengine, ila wasiwasi uliotanda ni fujo tashtiti na kusukumana visogo huku tukiendelea kupakana mafuta kua serikali yetu ya umoja maelewano na maridhiano ilhal iltukijua fika hapo watu hawataelewana, hakutokua na hicho kinachopakwa sukari sasa hivi. na ukisoma between the lines kwenye hapo juu utahakikisha shauku ya kufanya hayo
ikiwa kisonge walitoa kauli za jazma kwa ajili ya bilali, huu si wakati wa kila mtu kusema “tunataka wafanye!” manaake nini hio… ushindi kwa mvuvi. na kwanini imekua ajabu kwa bilali kueka kinyongo haliyakua kuna threat ya kunyimwa haki yake kwa mara ya tatu, kwani hili la kwanza, Sefu hakusema jino kwa jino, si akasimama, na jicho kwa jicho si pia kasimama, na roho kwa roho au imesahaulika? na mimi mpaka leo nasema Cuf wameshinda na wanadhulumiwa kiasi waseme wanavosema ule ni uchungu wa kudhulumiwa, lakini tazameni mnaoshindwa kuplay fair… hamuezi kusema bilali anafanya hivo kwasababu its too much. mimi mtu anaeonewa mara zote niko pamoja nae, na bilali na sheni kwenye resi hizi kwangu walikua na nafasi mmoja asihisi sheni amenyimwa kwasababu mpemba na wala bilali kwa makosa aliyofanya salmin, hao kisonge sababu tu, kisa ni salmin na ukiritimba wake na haswa si kwasababu kawagawanya wapemba na waunguja, tusijidanganye kua bara wanatupenda kiasi hicho!!! sababu kubwa ni kutishia kuvunya muungano, kitu ambacho pia ni positive kwa cuf, bilali angeingia akavunja muungano, ccm zanzibar peke yake isingekua na uwezo wa kuiba kura za CUF ikazisha Cuf ingeshinda tu.. ikawa tumejikomboa once and for all. lakini hivi sasa Shein awezi kuwaendea kinyume bara kwahio ilobaki tutizame tu khatma, tuache kujidanganya na kudanganyana. Ikiwa tunashikana tusishikane kinafik kutaka ujira wetu, wapo tunaotamani kurudi nyumbani lakini migogoro isokwisha inatukatisha tamaa na tutake tusitake kama hatujavunja muungano whether through CUF au CCM Zanzibar hatujakwamuka tutapangiwa hivihivi kila siku
Nawasilisha
Kuhusu kura hapa mzalendo tungesubiri kidogo, pengine huenda kuna wagombea wengine (kuotoka vyama vyengine) wakajitokeza. Hii itapelekea kuwapa nafasi nawao kushirki kwenye kura hiyo.
Pia itaongeza chaguo kwa vile wagombea watakuwa ni wengi.
Dr.Bilal awemo …Just kidding
P:S
Poll tayari nishaitengeneza ikijumuisha Shein na Seif.Sina data yoyote kuhusiana na vyama vyengine.Naomba tupeane update juu ya hilo.Tutasubiri kama 1 week halafu tutaifungua poll hio upande wa kulia kama kawaida inshallah.
Maasalaam,
mrfroasty
Sasa Serikali ni yetu walosema mpemba hatawali sasa Tushachukuwa Ikulu Ali Mohamed Shein Rais wa Zanzibar na sema haya kwa sababu chama cha CCM hakishindwi ndio maana namtabiri ni Rais hata kwa kura yake moja tu atakayojipigia mwenyewe Shein maadam ni CCM basi atatoka mshindi tupo hapa jamani na haya maneno nayasema mimi, Lapili Seif Sharif Hamad Wazir Kiongozi kama watakubali matokeo ya kura za Mseto. Kwa maana hiyo wapemba wawili tayari tupo madarakani Ikulu sasa niyetu balahauuuuuu huu ni wakati wetu sasa tuachane na mambo ya ukabila ufisadi chuki na majungu tuwe pamoja tujenge nchi yetu .
Haya ni nyinyi kisonge tuwaone sasa hizo Ahadi zenu mnotowa kama wanaume basi fanyeni hayo mliyoyaahidi CCM Haitishwi kwa maneno , Kashindwa RAIS wenu DR SALMIN ANAEJITA KOMANDOO Aliambiwa ajitowe OIC Akatowa ukali msitikise kibiriti , Alipoitwa Dodoma alijuwa kujitowa mbio, SASA KISONGE SAFARI HII JANJAWIRI WANAKUJA KWENU HAPO CHIPS HAZITOUZIKA HAPO .
Swadakta Mnyonge
Nafurahi kua maneno yangu hapo juu hayakuanguka chini…
Ukweli ndo huu
a/a wana ukumbi mimi kitu cha mwanzo nampongeza dr. Shein kwa kuchaguliwa kuwa mgombea wa zanzibar inshallah awe kiongozi wa kheri juu ya zanzibar mpya .
pili hawa watu wa kisonge waliosema wataanzisha chama chao kama dr.Bilal hakuchaguliwa mimi naona haina haja ya kuanzisha chama kwa sababu muda umekenda hizo kura zao za urais wampe maalim Seif tu na inshaallah mungu atawalipa kwa hilo wabillahi tawfiq
A.Alykum..
Kusema ukweli me nimeshangazwa sana na matokeo haya..na imenifanya nifirie,pengine ni kweli yasemwayo,CCM zanzibar haina maamuzi tena sasa..
Ila mi kawaida yangu huwa naangali vitu kwa upande mwengine wa shilingi,nilikuwa na mategeo kiasi flani kuwa kwa system ya CCM ilivyo basi ni logical kuwa Shein atashinda,kwani ukiangalia CCM zanzibar wamekuwa outnumbered na CCM bara,na hakuna kiongozi wa bara anaetaka maamazi ya zanzibar yawe hayo hayo!!Ila ile picha ninayo iangalia mimi hapa ni kuwa,kwanini Dr Shein akubali kuacha nafasi ya makamu wa rais wa Tanzania na kuja kugombania nafasi ya urais zanzibar ambayo kuwa ni unlikely atapata urais..
A.watanganyika wamemuondosha huyu kwa kuwa wanajua kuwa itapomaliza kipindi cha Kikwete basi yeye ndio atakuwa favourate wa kugombea urais Tanzania(watanganyika hawalitaki hilo)
B.Wanamfanya Shein kuwa ni kibarua wao since ni mtu pekee wa CCM zanzibar watakae weza kumcontrol kama alivyokuwa karume..tukumbuke,Bilal alivyokuwa kambi ya salmin,watanganyika hawakuwa na contorl ya zanzibar kiasi hicho kama ilivyo kwa awamu ya amani..
..Kusema ukweli..mimi naona kuu nahisi kuna kitu kimetendeka hapa,na vyvyote itavyokuwa shein ametoswa bila ya kujijua na once akiwa rais zanzibar..basi zanzibar tutabakia na maridhiano yetu ila tusahau kuhusu kujinyakua kwenye makucha ya watanganyika..!!
Mi inanisikitisha sana kuona kuwa bado watanganyika wana lengo la kuitawala zanzibar kinamna moja au nyengine!!Mungu atasimama nasi inshallah!!
@ Shamuhuna: Kama ukilinganisha control ya Tanganyika kwa Zanzibar wakati wa Salmin na wakati huu wa Karume nafikiri utagundua kuwa wakati wa Karume Zanzibar imefanya vizuri zaidi ya wakati wa Salmini.
Nikupe jambo moja tu. Ni wakati wa Salmini ndio zanzibar ilipomaliza kuhamishiwa Bara. Umesahau kuwa Salmini ndie aliyekubali Raisi wa Zanzibar kuvuliwa cheo chake cha umakamo wa Muungano?
Sasa tuje wakati wa Karume. Kwa mara ya kwanza mjadala wa masuala ya muungano umekuwa na nguvu kupita vipindi vyote. Ni juzi tu msukumo wa kuyatoa mafuta katika mambo ya muungano umeanza na tayari hatua za kufanya hivyo zimechukuliwa. Na inshaallah tunategemea karibuni tu mafuta yetu tutarejeshewa wenyewe. Jee, dogo hilo?
Jamani mnafurahia Sheni wakati hajaonyesha msimo wake juu ya umoja wa wazanzibari na serikali ya mseto? Nadhani mmesahau wakati wa mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu.
Ni Shamhuna na Haroun tu ndio ambao wamesema wazi kuwa wanataka kura ya NDIO katika referandum. Shein hakusema msimamo wake. Leo watu wanasema eti kwa vile Shein ni chaguo la Karume ambae anapendelea maridhiano basi na Shein pia atakuwa anayataka.
Sasa kama anayataka alishindwa nini kusema wakati bosi wake Karume kasema hadharani?Tutahadhari na kuwahukumu watu kwa matendo ya watu wengine.
Raisi anapoingia madarakani huwa hana mkataba na mtu aliyemueka na uongozi wote huuendsha kwa utashi wake.
Kama viongozi waliopita wanaathari kwa wajao basi tungeona kina Salmini nao wangejenga majumba ya maghorofa au yanayofanana na hayo unguja na pemba kama alivyofanya Abeid Karume au kwa uchache tusingeshuhudia chuki, fitna, ubaguzi na unyanyasaji wakati wa Salimin.
Kwa hivyo ni kusema kuwa Shein na yeye ana uwamuzi binafsi wa jinsi ya kuiongoza nchi na yeye ndio atakuwa mas’ulu wa jinsi ya aliyoyatenda. Msimamo wake binafsi ni muhimu kumhukumu kama ni mpenda maridhiano ama la na si kutumia kigezo cha watu aliokaribu nao.
Ama kwa upande wa Bilali mimi naona amejimaliza mwenyewe kwa uendeshaji wa siasa zake mbaya na chafu. Na kuna baadhi ya watoa maoni hapa waliwahi kuonya kuwa makundi ya Kisonge, vitisho, na kumwaga makaratasi ndio yatammaliza Bilali.
Kweli hili ndilo lililotokea. Yawezekana kuwa CCM bara walishamkacha Bilali na hawakuwa na nia ya kumchagua, lakini matendo yake ndio yaliyomzamisha zaidi.
Komandoo kuibuka Dodoma pia kulichangia kummaliza Bilali kwani kuli-prove beyond doubt kwamba mtandao wao ni mmoja.
Hapa wazanzibari tupate funzo kuwa chuki, dhulma na ufisadi si jambo la kutiliwa nguvu. Badala yake tuhimize mshikamano wetu kuijenga Zanzibar iliyoporomoka kiuchumi, kimaadili na kila kitu kutokana na matendo ya chuki za viongozi wasio waadilifu.
mimi naangaliya zaidi kufika salama tu sitajali njia gani tutapita sababu huko nyuma tulisimama njiani kwa mda mrefu tukiwa hatuna dereva madhubuti sasa na huyu kama ndie anategemewa kukabidhiwa usukani [kama ccm itachukuwa tena baada ya uchaguzi 2010] mimi binafsi siamini kama kachaguliwa kwa nia ya kuifikisha zanzibar wanapotaka wazanzibar wafike ila kapewa kwa kuifikisha zanzibar pale watanganyika watakapo wao ifike, ila sasa ni wakati wa kuelekeya kwa ALLAH atushushie rehme zake inshaalah tutafika salama..
nimesema zamzni serikali ya Zanzibar haina nguvu yoyote ya kuchaguwa kiongozi wamtakae sisi sasa nchi au visiwa vyetu tumekuwa kama mtoto mchanga, tunachaguliwa nguo gani tuvae na chakula gani tule na ambri zote zinatoka wapi? dodoma ndiyo ilivyo mimi naona safari hii labda kiongozi atoke kwenye chama chengine ndio kutakuwa na hope na visiwa visiwa vyetu maana ccm ndiyo ileile mtoto wa nyoka ni nyoka tu. Wakutegemewa sasa ni M.Mungu Subhana Allah Waataalla ndie wakutusaidiya na wakumtegemea basi maana sera zote za ccm zinatoka dodoma na Pinda alisema baraza la wakilishi Zanzibar wanasema na kujifurahisha tu mambo yote dodoma na huyo Mzee Shein alikuwa tayari ameshapita walikuwa wanasubiri wamtangaze tu haya mambo ya kura danganya toto tu kwani kura ngapi zimeshapigwa na matokeo yake je haya basi tumeshachaguliwa nguo ya kuvaa sasa tusubiri chakula tu na sijuwi tutalishwa nini. M Mungu ibariki Zanzibar Amin
Musijali ndugu zangu wa kisonge kwa kutochaguliwa Mr. Bilali. Kuchaguliwa kwa sheni sio kuwa Rais wa Zanzibar.Inshaallah rais wa Zanzibar hatakua Shein kwasababu sio chakuo la Wazanzibar bali chaguo la Wazanzibar ni Maalim Seif Sharif Hamad huyo ni chaguo la Wazanzibar.
As, alaikum
salam wazanzibar, kwanza kabisa nampongeza mshindi dr sheni,kwa kuanza mnakumbuka kikwete alisema kuwa ataumaliza mgogoro wa wazanzibar watu wakamuona muwongo basi kwa taarifa huu ni mwanzo tu , pili eeee bilali kwani ulifikiri mutatawala kila siku kwa shuki na vitisho , kuwapiga watu, kuwaharibu watoto wa kike, kuwarejesha wapemba kwao, kuwavujia nyumba , kuwambia watu mapanga mnayo yanoweni na mabaya kadha wa kadha jee mungu si asumani , sasa zamuyenu mukifanya fujo hilo hilo jeshi lenu janjawid litatumwa kukuwekeni sawa, tatu watu wakimwita salmin eti commando nadhani safari hii kageuzwa jku , na raza uwache kidomo domo chako wapemba safari watakupiga mikwaju tena hazarani ,tena usije ukajisifu mimi ukereketwa utawajuwa wapemba ni nani watakupiga mikwaju kama mshezo wa ngombe , raha tupu kutesa kwa zamu, umeme tushapata, rais tushapata, waziri kiongozi tushapata , ikulu tutaingia eeeeeeehee , na kisonge safari tutawarusha roho wakitaka wasitake lazima tuwakatishe viuno , wao si walisema katu mpemba haingi ikulu , kisonge msewe unakuja kutesa kwa zamu.
Nyie mnashabikia tu, mwaka wa mpemba unajua hata huyu SHEIN upemba wake unatiliwa Question- Mark ???
Hana ,tofauti wa Ali Hassan Mwinyi kubambikwa Uzanzibari ,kumbe ni miundombinu.
Mbona, mnajisahau .Zanzibar ni pahala penye unafiki mkubwa miongoni mwa watu.
La msingi,tukitupilia mbali upemba na unguja kwa kuuona zaidi Uzanzibar na si uzawa tu,kwani Salmini ndio kindakindaki uloyafanya mnayajua nyinyi.
La maana, dhati ya kujenga,uwezo na imani ya kweli ya kufuta – siasa chafu.
For 15 years ago,Zanzibar imekwama ,kisiasa,kiuchumi na kijamii.Huko baraza, ni commedy tupu za TOM&JERRY.
Ukurasa mpya unahitajika ufunguke, kwetu kumuomba Allah S.W awafungue macho waliolala uzalike umoja wa kweli.
Masaalam….
Asalamu Alaikum,
Ndugu zangu wazanzibar, nawaombeni sana kuwacha maneneo maneno Tumuombe Mwenyezi Mungu mambo yetu wazanzibar yaende kama vile tulivyoaanzisha. mambo ya kusema kuwa kachaguliwa “Mpemba” au “Bilali kakosa” au “kisonge wanalia” haya hayasaidii kujenga umoja tuliounzisha na badala yake tutanza kupandisha ari za wale wabaya wa zanzibar za kukataa au kwenda mbali na makubaliano yetu.
Huyo Shein ni CCM na bilali ni CCM, na CCM wamepitisha Mgombea wao kama VIle CUF walivyopitisha Mgombea wao na vyama vyengine halikadhalika.
Sasa CCM wasione kwamba mgombea wao ndio ashakuwa Rais ingawa kwa tume tuliyoizoweya tunajuwa itamfanya awe hivyo, lakini mambo ya kuwaka mtu kiongozi ni lazima yapate amri kwa mwenye dunia naye ni Subhanna llahu Wataala, wakati wowote anaweza kufanya atakavyo yeye.
salamz wana ukumbi wote, hapa hapana upemba wala uunguja, kinachitizamwa na ccm bara ni nani ataeweza kuwa kibaraka mzuri, SHEIN NI KIBARAKA MZURI, dr salmin unaona sasa, umemfunza mwari wako shein na sasa ndie yeye anekutovukia adabu, haya shein watumikie hao wabara kuliko sisi wazanzibar wenzio, kama hatujajuta wala hatujuti tena, hii ni wazi kuwa wazanzibar hatujitawali, sisi bado tunatawaliwa na wabara, shamhuna nakubaliana nawe kuwa shein hauziki hata kwa bure na wapiga kura wa zanzibar, kwa taarifa yetu tujue sasa tayari kikwete ametia battery mpya ktk remote yake (shein) atamfanya anavyotaka yeye, ili mimi bado nna wasiwasi na hayo matokeo, ktk vikao vya juu vya nec ya ccm, kuna ile kura batili ya “MPISHE MWENZIO AMEKOMAA KISIASA” isijekua hii nayo imetumika kwa bilal, au ndo nchi hii kwa vile imekombolewa na wafanyakazi na wakulima na ndio maana wasomi hawatakiwi tena??? pole bilal riziki yako bado ipo, na kila alie kupa mgongo basi hapahapa duniani atajutia, kwa taarifa tu wanamzalendo wenzangu, SASA NI MWISHO WA CCM ZANZIBAR, na kwa hapa kikwete umefanikiwa sana, hali ya kua ukijua kabisa shein hauziki zanzibar, au ndo “TUNACHUKUA TUNAWEKA WAA” haya kazi kwako sasa, ccm wana kazi ngumu sasa kumpigia kampeni shein (au remote itatumika na hapa)haya sasa tule tugawe.
maa ssalam.
Hongera sheni, nimefurahi kusikia kwamba sheni ni chaguo kutoka Dodoma.CCM Shein, CUF Seif wote wapemba yeeee.
Hawa vibaraka basi siku zote wawe kutoka Unguja tu?
Sisi wengine tumefurahia si kwa sababu ataleta mabadiliko yeyote ya kiuchumi, lakini ni kule kupinga kauli za CCM Zaznibar ati Mpemba hatawali.
Kauli zilizo kuwa hazibadiliki au tuseme zenye uhakika ni za mmoja tu naye ni Allah (SW).
Mungu akaja kupitisha rehma zake na Shein ikampitikia achaguwe Waziri kiongozi kutoka Pemba, Wa-Unguja watahisi vipi?
Inshallah Mwenyezi Mungu awe ametutakabalia dua zetu za maisara. Atupe mapenzi baina yetu, ili tupigane na adui ubaguzi. Hii iwe ni chachu ya kuleta maendeleo na azitupiliye mbali husda za Kisonge za kutaka kuleta machafuko Zanzibar.
WanaMzalendo, Kwa kweli ni ningeanza tu kwa mara nyengine Kumpongeza Dr Shein. Chamsingi hatujui nani atakuwa Rais wa Zanzibar lakini tunaomba yoyote atakayeingia ikulu ya Zanzibar ile bendera ya maridhiano ipepe. Tumechoka na chuki na ubinafsi. Kwa bahati Dr Shein huna makundi lakini wako wengi sasa hivi watakuja hasa wale wenyenjaa kwa hiyo ni wajibu wako wawajua watu wa aina hii. Kila la kheri tunatarajia Dr Shein na Maalim Seif mara hii tutaona kampeni na siasa za kistaarabu. Wote watu ambao mumejijengea heshima kubwa katika jamii.
Nimefurahi sana sana kusikia chaguo la CCM ni Dr. Shein maana angalau tutapata afuweni sisi Wazanzibari maana tumechoka na U-Salmin usio na faida na manufaa kwa Wa-Zanzibari.
Inshaadhwa tunaomba uwe uchaguzi huru, usio na matusi wala vurugu ili tuishi kwa amani na mapenzi ili tulete maendeleo kwenye visiwa vyetu.
Profile ya Dk.Shein
DK Ali Mohamed Shein na Dk Mohamed Ghalib Bilal ni Wazanzibari wasomi ambao wamekuwa kwenye anga za kisiasa kwa muda mrefu, lakini Bilal ndiye amekuwa akiutamani urais wa Zanzibar na amepambana kwa vipindi viwili bila mafanikio.
Mara zote mbili aliangushwa na rais anayemaliza muda wake, Amani Abeid Karume, ambaye aliingia Ikulu ya Zanzibar mwaka 2000 na kufanikiwa kutetea kiti chake mwaka 2005.
Dk Shein alizaliwa Machi 13, 1948 katika Kijiji cha Chokocho kilicho wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba.
Alipata elimu ya msingi na sekondari kisiwani Unguja. Alisoma katika Shule ya Wavulana ya Gulioni kati ya mwaka 1956 na 1964 na alijiunga na Shule ya Sekondari ya Lumumba mwaka 1965 na kumaliza mwaka 1968.
Mwaka 1969 alikwenda nchini Urusi kujiunga na Chuo Kikuu cha Vorenezh kwa kozi ya maandalizi ya mwaka mmoja kabla ya kujiunga na elimu ya Chuo Kikuu. Baada ya kumaliza kozi hiyo (mwaka 1970) alijiunga na Chuo Kikuu cha Odessa kusomea masuala ya tiba ya magonjwa ya binadamu (medical biochemistry) hadi mwaka 1975 alipohitimu na kutunukiwa shahada ya uzamili.
Mwaka 1984 alienda Uingereza kuchukua masomo ya shahada ya juu ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Newcastle.Alihitimu masomo hayo mwaka 1988 na kutunukiwa shahada ya uzamivu (PhD). Dk Shein alipata pia mafunzo mengine mbalimbali katika fani ya tiba na uongozi ndani na nje ya nchi.
Aliwahi kufanya kazi katika nafasi mbalimbali katika Serikali ya Zanzibar na kwa nyakati tofauti tangu mwaka 1969. Aliwahi kuwa karani katika Wizara ya Elimu, Zanzibar na Msaidizi wa Katibu Mkuu katika wizara hiyo.
Aliwahi pia kuwa mkuu wa Idara ya Huduma za Maabara katika Wizara ya Afya, Zanzibar mwaka 1979 na kudumu katika nafasi hiyo hadi mwaka 1984.
Mwaka 1989 aliteuliwa kuwa mkuu wa Idara ya Patholojia katika Wizara ya Afya na mwaka 1991 aliteuliwa kushika nafasi ya meneja wa Mradi wa Kudhibiti Ukimwi, Zanzibar huku akiwa na majukumu mengine ya kutoa ushauri kwa wizara. Aliingia kwenye siasa tangu akiwa mwanafunzi.
Alijiunga na Umoja wa Vijana wa chama cha Afro Shiraz tangu akiwa shuleni na mwaka1968 aliteuliwa kuwa katibu wa habari wa Umoja wa Vijana wa Afro-Shiraz kwenye Shule ya Sekondari ya Lumumba.
Dk Shein aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Oktoba 1995 na Novemba aliapishwa kuwa Naibu Waziri wa Afya Zanzibar. Mwaka 2000 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Jimbo la Mkanyageni, kisiwani Pemba.
Mwaka huohuo aliteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Katiba na Utawala Bora wa SMZ. Alidumu katika wadhifa huo hadi Julai 2001 alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa na kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kiti hicho kuachwa wazi na Dk Omar Ali Juma aliyefariki ghafla.
Mwananchi
Nania aliyesema Dr Shein ni chaguo la Bara?
Kwenye magazeti jana tulimsoma natepe na Moyo wakisema Dr Shein ndio chaguo zuri.Kwa CCM Zanzibar, wawili hawa wana nguvu ya aina yake mithili ya Nyerer na CCM Bara. Hawa ndio walio muungasha Dr Salim Ahmed Salim mara zote.
Tujaaliye Dr Shein hakuwa chaguo la Zanzibar. Sasa Tatizo liko wapi? Siku zote wamekuwa wakiambiwa kuwa huu mfumo si mzuri. Tunakwenda pale kama nchi mbili kwenye Bunge na Chama. Chama tokea 1977 kimekuwa na nguvu kuliko serikali. Kwa hiyo ni lazima wajumbe wa NEC wawe na uwiano katika kutoa maamuzi ya juu. Isichukuliwe Zaznibar ni kama mkoa kutokana na udogo wake wa kiramani na watu wake.
Kwa kumalizia nawaomba Wa-zanzibari wasije kufanya makosa kwenye kupiga “ndio” kwa serikali ya umoja wa Kitaifa. Tukifanikiwa kwa hili, tutakuwa na nguvu za aina pekee na hasa tunapokwenda Bara. Tusijaribu kufikiria kuvunja Muungano, bali tufikiriye kuimarisha Muungano unao kubalika kwa maslahi yetu sote. Panapo kuwa na mijadala ya wazi na wananchi kushirikishwa, basi tutapata kitu safi.
Hakuna kinachonivutia kwenye uteuzi wa mgombea wa CCM kwa kuwa si yoyote kati yao anaonekana au walau kuwa na dalili ya kukata mirija yakinyonyaji ya muungano. Hivyo Dr.Sheni ameshapitishwa na watanganyika kuwa kibaraka wao Zanzibar, hatakuwa na sauti ila kutikia hewalla kwa kila kitu na zile kelele za “mafuta yetu, mafuta yetu…”karibuni zitakuwa kelele za mlango kwani mlinzi wa mirija ya unyonyaji ameshawekwa.
Kufadhiliwa kubaya, regardless sheni anatoka wapi madhali kawekwa hapo na wenye chama hata kuwa hapo kwa manufaa ya wananchi, tusubiri tu.
Kadhalika, mtu ambaye atalala kwa usingizi mnono na furaha saivi ni Amani Karume, ambaye ameshampata wa kulinda udhalimu wake na wizi wakati akiondoka madarakani.
Kipigo chengine kwa wazanzibar, wala tusifikiri kuwa watanganyika kwa kumpitisha Sheni wamewapendelea wapemba waongoze nchi. Sheni anabakia kuwa kibaraka wao na wao watamtumia kama walivyowatumia watangulizi wake kuifisidi nchi na watu wao wenyewe. Tusubiri tulie kilio cha kwikwi mara hii,maana shoka limepata mpini wa kweli sasa,miti yote itashika adabu yao!!
Kama kuna dua ambayo ni ya kuomba na ndicho kilichobaki kwa wazanzibar kupiga ndiyo kura ya maoni ili tuwe na serikali ya pamoja ambayo interference za watanganyika zitakuwa closely monitored and dealt with unity.
MUNGU IBARIKI ZANZIBAR
J
OMMYKISS NA KUMEKUCHA
mbona mnatuchanganya? wembe gani tena huo alonyolewa bilal mwaka 2000 na mwaka 2005, basi washauri ccm wabadilishe katiba yao kua mtu akifanikiwa kuwa rais ni lazima abakie nafasi hiyo kwa vipindi viwili, pia akimaliza kipindi cha pili aruhusiwe atoe mtu anaemtaka yeye awe mrithi wake, au mnaonaje hiyo wanamzalendo??? lakini hapa napata mashaka ya matokeo hayo, au ndo MAPINDUZI DAIMA,pole babu yangu dr bilal.
@ GUMEGUME, kakwambia nani shein hana makundi? ni juzi tu kina mansoor wanapigana vikumbo nyumbani kwa shein maisara kupeleka ujumbe kutoka kwa “MZEE” pole sana gumegume.
thanks,zanzibar ni njema atakae aje
@Kassim,
Mwenzetu hebu tupe hizo faida za muungano ambao unataka tusifikirie kuuvunja.Kumbuka sasa ni miaka 50 (nusu karne) wazanzibari wamekuwa njia panda na kuganda kujiletea maendeleo sababu kuu ni Muungano.
Unataka tuendelee na miaka mengine 50 ya kujadili na kutatua kero za muungano.Zaidi ya hapo, umetuacha pangu pakavu kwa kusema tusifikirie kuuvunja bila ya kutupa sababu yoyote ya kuonesha faida tulizopata baada ya kustahamili kwa muda wa nusu karne.
Pengine suala kwako, jee tusingelikuwa na muungano tungelikuwa wapi kimaendeleo?
Kwa kumalizia toa maoni yako na ujisimee nafsi yako, usijaribu kuwaambia wazanzibari wasijaribu kufikiria.Hii ni kauli ya vitisho na kidikteta, watu wanatakiwa waachwe huru kufikiria.Napenda kuwahakikishia wazanzibari kuwa watapiga hatua kubwa sana za kimaendeleo pindipo watavunja muungano.Wana kila sababu ya kufikiria kuuvunja, na ndio njia sahihi ya kujikwamua na matatizo yao mengi ya kimaendeleo.
Maasalaam,
mrfroasty
@Positivu,
Nakubaliana na wewe ni kweli kabineti yote ya Karume ilikuwa nyuma ya Dr.sheni na usishangae atakapowekwa madarakani baadhi yao wakaendelea kama kawaida na nyadhifa zao. Na Karume ndiye alimshawishi Sheni kwa kisingizio cha MARIDHIANO ambayo kwa Karume hayana faida kinchi bali kwa nafsi yake.
Ni wazi kuwa hataguswa na midhambi yake akiondoka madarakani maana mtu wake yupo na jaalia hiyo serikali ya ukweli na uwongo ya umoja wa kitaifa inaundwa ndiyo kabisa kwa kuwa itakonekana kaiasisi yeye basi hakuna atakaye mgusa.
Nilichokuwa nakiomba yule bibi(Fatma Karume) aache kupayukwa payukwa na kulia lia kuwa mwanawe anasingiziwa wizi, labda nimkumbushe awe fair, si mwanawe hata mjukuu wake Ahmed Karume ameshawadhulumu shamba la ekari si kidogo wakaazi wa Nungwi mkoa wa kaskazini Unguja, na mradi mkubwa hoteli ya kitalii umeanza. Kwa hiyo si mwanawe tu, ukoo wake wote wezi pamoja na yeye na akiendelea kubisha tutamfunuwa mpaka na yeye.
Kama Bi.Fatma anamuona mwanawe safi, basi ajitazame na yeye anayechukuwa mali za serikali kwa miradi yake binafsi kwa kisingizio cha “marehemu bwana”kapoteza roho itakuwa vipipa vya maji ya UUB.Loo!bibi hana haya yule, mwanawe kaifisidi nchi na yeye ameshamtafuta kibaraka kama yeye kwa kusaidiniana na mabawana zake wa tanganyika kumaliza kilichobaki.
Washukuru sana Zanzibar haina msitu, wangeshika adabu yao,tumechoshwa na upuuzi wao!
J
Kwako Junius
Huwa nakufuatlia sana comments zako unapozitoa wakati uko kwenye mzalendo na jamii forums.Huwa napendelea sana comments zako jamii kwani ni miongoni wa wazanzibari wachache walioweza kuwa up in arms na ndugu zetu wa upande wa pili haa katika masuala yanayohusiana na Zanzibar.
Kwenye jamii forums uko very well connected to the point and subject issue. Ila kwenye mzalendo unaonekana kidogo kuelekea zaidi katika discussing people more than issues wakati jamii upo vice versa.
Can you tell me why.
Punda yule yule lilobadilika ni soji endeleeni na furaha kibao kile kile ccm will never change
salamu wazanzibar, BILALI,eeeeeeeeeeee cmm hawakutaki tafuta jembe ukalime, au njoo cuf na wanachama wako, tutakupokea sisi hatuna matatizo muhimu upiganie haki, yaani haki kwa sote, na kama unataka kujiunga na jahazi asilia shauri yako jahazi yafata upepo ikikosa yatangatanga, lakini sisi cuf tunatumia speed jet boart kama unataka iwahi kabla boart haijaondoka, kama unataka jahazi asilia ujue tu jahazi lishatoboga linakwenda mrama.
alieshinda hasa ni Amani Karume…..na familia yake.. Mchezo umekwisha!
Na sisi wazanzibari tumerubunika kwa kutuletea maridhiano haliyakua tunajua fika kua angelitaka hili angelileta mapema 1- kaiba kwanza- 2- kafunga mlango halafu katupa wenyewe ufunguo. sisi tunafurahi tu kwasababu na sie tutakua washika funguo basi mwache aende na alichoiba… hamna neno!
wanaosema eti SALMIN< NA BILAL, MAKAMANDO WAMEKOSEA , COMANDO HASA AMANI KARUME KAMPINDUA BILAL, 2000,2005,2010 NA SASA KAMMALIZA KABISA ARUDI CHUO KIKU AKASOMESHE NDIO LILILOBAKIA
@ Junius,
habari yako, natumai umenielewa vyema hapo hako ka fatma karume atulie kweli saivi sababu wazanzibar wamechoka nae< sijui safari watampa tenda gani kama ya matofali au ya kushona uniform za janjawiri, junius kwa taarifa yako saivi wakina karume wanataka lile jumba la mayatima forodhani wauze ulevi basi, jee hii ni haki kweli, shein ajitayarishe kweli, mda wa karume umeisha lakini miradi yake bado, junius umeenda tunguu ukaona mahekali ya shadya karume? fanya uende, ujionee ardhi chache ya zanzibar inavyomilikiwa na wanamapinduzi wachache, yaani we acha tu.
@ MTUKWAO UNANIKOSHA
alieshinda ni karume sio sheni, sheni tayari alishajisabilia maisha yake bara na ndio maana hata kajiandikisha bara, sijui kapewa mabilioni mangapi na karume ili aje atuharibie shughuli yetu, sawa karume malizia hiyo ardhi iliyobaki baba, hongera.
@SARHAN SALIM,
kweli amani ndo komandoo
Kulikuwa na LIVE coverage hapo kwenye chapisho hilo, imekuwa moved kwenye section ya live coverage i.e
mzalendo.net/live au bonyeza button ya “LIVE” hapo juu kwenye navigation.
Maasalaam