Kuzuka kwa Dk Salmin Kwazusha Mjadala

Written by  //  08/07/2010  //  Kitaifa  //  17 Comments

Salma Said,

SIKU moja baada ya kuibuka kwa rais mstaafu wa Zanzibar Dk Salmin Amour Juma katika harakati za kumtafuta mrithi wa rais Amani Abeid Karume kumeibuka hisia tofauti za kibaguzi juu ya kujitokeza kwake.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ni miongoni mwa waliotoa maoni yao yanayokosoa kujitokeza kwa ghafla Dk Salmin ambaye kwa miaka kadhaa hajaonekana katika ulingo wa kisiasa.

Kauli kubwa ambao imetolewa na baadhi ya wanachama wa CCM Zanzibar hasa wenye msimamo wa maridhiano wa maridhiano ni kwamba Dk Salmin maarufu Komandoo ana lengo la kurejesha nyuma juhudi zinazoendelea za kuwaunganisha ambazo zimefikiwa na viongozi wakuu wa vyama vya CCM na CUF.

Said Soud Mwenyekiti wa chama cha wakulima (AFP) amesema kwamba kuibuka kwa Dk Salmin ni dalili za kukataa maridhiano ambayo kwa kiasi kikubwa yamepiga hatua ya kuondosha chuki na ubaguzi kati ya wapemba na waunguja.

“Kuibuka kwa Salmin ni jumla ya kambi inayokataa maridhiano ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ni jambo la kusikitisha sana na kuhuzunisha kwani siasa za chuki zinaendelezwa na ndio maana likaibuka suala la kuwa Shein sio mzanzibari ati amezaliwa bagamoyo na Aboud kuwa hajasoma hizi zote ni chuki dhidi ya wapemba tu … wanataka kuturejesha nyuma tulipotoka” amesema Soud.

Soud aliitahadharisha CCM kuwa makini na watu kama kina Salmin ambao waliiacha Zanzibar ikiwa katika dimbwi la ubaguzi, chuki na fitna za kisiasa za wenyewe kwa wenyewe.

Kauli ya Soud iliungwa mkono na Katibu Mkuu wa TADEA, Juma Ali Khatib ambaye amesema Salimin anataka kuwarejesha wazanzibari pale alipowaacha yeye ambapo chuki majungu na fitina zilitawala na hadi baadhi ya wafanyakazi kufukuzwa kutokana na fitna za kisiasa.

“Wasiwasi wetu ni kuwa huyu Dk Salmin kuibuka kwake anataka kuturudisha nyuma, wakati anajua kuwa hakuna chuki za kisiasa zile za upemba na uunguja hivi sasa tokea kuazishwa kwa maridhiano mwaka jana. Tunawaomba CCM wawe makini sana kumuangalia mtu huyu ambaye siasa zake ni za kizamani na hazipaswi kuendelezwa kwa sababu wakati wa utawala wake wazanzibari wengi waliathirika chini ya uongozi wake” alimalizia kusema Khatib.

Aidha Ali Omar wa NCCR- Mageuzi alisema kwamba mtu yeyote mwneye mtizamo wa kukumbatia ubaguzi wa unguja na pemba au za kisiasa kama Dk Salmin asipewe nafasi katika siasa za maridhiano ambazo zinahitaji zaidi umoja na mshikamano wa wananchi wote.

“Sisi tunapozungumza hatuingilii utaratibu wa CCM lakini tunajali sana utaifa na kuendelea kwa amani na utulivu nchini na watu kama Salmin wenye mawazo ya mgando wasiotaka mabadiliko hawatufai kwa sasa ni vyema wakatupisha tukasonga mbele” alisema Omar.

Kauli za kuhoji kuibuka kwa Dk Salmin pia zimejitokeza kwa baadhi ya wana CCM Zanzibar wenye kutaka mageuzi ya kisiasa na kuendeleza maridhiano huku wakikitaka chama chao kuwa na busara katika kumteuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama hicho.

“Sisi tunafuatilia kwa makini na tumefurahi zaidi Salmin kwenda Dodoma tukijua kuwa kuwepo kwake watatuletea mgombea anayekubalika unguja na pemba lakini kama ana ajenda ya kumuunga mkono mgombea Shamsi hilo litakuwa ni kurejesha nyuma maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar ambayo tunamaini wazanzibari wengi wanaunga mkono” alisema kiongozi mmoja wa CCM ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Hata hivyo Kada maarufu wa CCM, Baraka Mohammed Shamte amesema kuwepo kwa Dk Salmini Dodoma ni jambo la kawaida kwa kuwa ana haki ya kushiriki vikao vya chama chake katika maamuzi mazito kama ya kumteuwa mgombea wa urais wa nchi yake.

“Sio tatizo Salmin kuja Dodoma kwa sababu yeye ni kiongozi na mjumbe wa NEC na alikuwa haonekani kwa sababu alikuwa mgojwa lakini sasa amepona ana haki zote za kuja kwenye vikao, na kama kumuunga mkono Dk Bilal sio vibaya kwa sababu hata Karume anamuunga mkono Dk Shein” alisema Shamte.

Wajumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu ya CCM leo watakuwa na kazi nzito ya kuwachuja wagombea na hatimae kumpigia kura mgombea mmoja ambaye atasimamishwa kwa tiketi ya chama hicho kuwania urais wa Zanzibar pamoja na wagombea kutoka vyama vyengine kikiwemo chama kikuu cha upinzani cha CUF.

17 Comments on "Kuzuka kwa Dk Salmin Kwazusha Mjadala"

  1. mrfroasty 08/07/2010 kwa 11:11 um ·

    Kumbe Shamsi haungi mkono maridhiano, basi si angesema tuu kwenye mahojiano na hotuba zake anajizungusha bila ya kutupa jibu tukamfahamu.

    Anyways, Shukurani Bi.Salma kwa makala hii.

  2. Abuu Said 08/07/2010 kwa 11:28 um ·

    @Bi Salma
    Sifikirie kamwe kama hata Bilali kuja kua Mgombea wa uraisi Zanzibar atayarejesha ya nyuma au mwengineo wa ccm, atakua kiongozi wa ajabu kweli.
    Nnachoshangazwa kwa jama zangu wa pemba haweshi kulalamika kwa mfano wa Mohammed Aboud Dumla lile limekwenda wapi shule, yeye ni sawa na seif na masharubu tu.. Ama kwa Dr. Shein sio jambo la busara kusema si Mzanzibar hayo majungu mengine ni kijinga, kwani ni msomi na mstarabu ila kwa upande wabgu nnaona kama si vyema kwake kuingia katika msururu huu kwani ukiangalia ni sawa tu na kiongozoi aliokuwa Raisi ikisha akarudishwa nyuma kua mkuu wa mkoa…
    AHSANTENI wAUNGWANA..

  3. ommykiss 08/07/2010 kwa 11:34 um ·

    Mimi sijaona tatizo lolote kwa Dr, Salmin kwenda dodoma kwani yeye ana haki kama wajumbe wengine walivyo na haki ya kuhudhuria vikao vya chama chao, na hawa viongozi wa vyama vya upinza waliotoa ni maoni yao waliyoyahisi kwenye vichwa vyao na kwa upande wangu mimi siyapi uzito wowote.

    kwa nini kila siku tunakua na mawazo negative tu? tujaribu kufikiri positive kwa baadhi ya mambo na wakati

  4. Jiti mjaka 09/07/2010 kwa 12:06 mu ·

    Jamani Salmin ni sawa sawa na shabiki wa mpira yeye kenda kutizama hata kama ata chagua kingozi ata chaguwa kwa kura yake m1 nawengine nao pia watapiga izo kura au labda ange pewa kazi ya kuchaguwa kiongozi wa ccm peke yake apo kidogo tungelala mika.

    Ila atakama Dodoma akimchaguwa kiongozi si bado kuna kura ya October ambayo sie tulo kuwepo Zanzibar tunapiga kura tatizo liko wapi wao tuwa ache kama kuku ma kienyeji tu subiri jioni wataingia wenyewe bandani wasi tumize vichwa bureee!!

  5. mkarafuu 09/07/2010 kwa 12:07 mu ·

    Salam,

    @Abuu said ni kweli sisi wapemba tunalalamika ila hilo tulilalamikialo sio kweli?

    Malalamiko yetu ni hayo masikitiko yako ya kua Zanzibar imefanywa kua mkoa,na hii kumwambia DR, Shen si Mzanzibari sio ubaguzi ninini? au mpemba hafai kua Raisi?
    na hapo uanthibitisha kwakusema:.” Ama kwa Dr. Shein sio jambo la busara kusema si Mzanzibar hayo majungu mengine ni kijinga, kwani ni msomi na mstarabu ila kwa upande wabgu nnaona kama si vyema kwake kuingia katika msururu huu kwani ukiangalia ni sawa tu na kiongozoi aliokuwa Raisi ikisha akarudishwa nyuma kua mkuu wa mkoa… ”

    Hata hivyo unapaswa kujiuliza nani aloifikisha hapo Zanzibar?.
    Nikifika hapo ndio nashindwa kuwaelewa hawa CCM wa Zanzibar sio kua hamjui kua nchi mumeiuza na sio kua hamuumizwi na hilo,lakini munashindwa kua na uwamuzi na huo ndio udhaifu wenu ndio tukawaita MABUNJU,hamujui liwaumizalo wala liwafurahishalo,mupo tuuuuu.

  6. mohamed ngwali 09/07/2010 kwa 1:11 mu ·

    mimi najaribu kosoma article za watu mbali mbali lakini nashindwa kupata conclusion ya mambo yanayozungumziwa.hasa kuhusu serikali ya mseto. watu naona kama wanajikanganya ku, ltimatumhusu serikali ya mseto ‘utasikia fulani haungi mkono.kwa ufahamu wangu najuwa serikali ya mseto ni sheria ikiwa itapata ridhaa ya wananchi.maadam imepitishwa kwenye baraza la wakilishi.hakuna kiongozi mwenye uwezo wa kubadilisha sheria hii jambo la muhimu ni kuwaelimisha wapiga kura uzuri wake au ubaya wake.kuliko kutaka kujuwa kwenye mgombewa nani anapinga,, tumieni muda huu muhimu kuelimisha jamii. kwa sababu hao walokwenda dodoma wanakutegemeeni nyiye kuwapigia kura za uraisi . wache wafanye usanii wao huko dodoma, ultimatum watakuja kwenu kuomba kura.kuelimisha jamii ni bora kuliko kutaka kujuwa wangapi wako kuli a na wangapi kushoto

  7. depsis 09/07/2010 kwa 2:24 mu ·

    Lazima kuna kijambo kwa Salmini kujitoa pangoni kwa kujisotora akaelekea Dodoma. Na kijambo hicho si chengine ila ni kuhakikisha chaguo lake Bilal linapita ili aje aendeleze chuki na hasama ambazo kipindi kirefu zimezima tangu Salimini aondoke madarakani.

    Eti siku za nyuma alikuwa anaumwa ndio maana hakuhdhuria vikao lakini sasa amepona. Hayo maradhi yake yanapona kwa kikao cha Dodoma tu. Mbona kikao cha juzi siku chache hakutokea.

    Ameona mambo ni mazito kwa mgombea wake ndio maana akajitoa huko mafichoni roho yake haikumpa kukaa ndani kwani ile sadakat-al-jaria ya chuki aliyoiacha imezimwa. Lakini inshaallah kama wana nia ya kutufarakanisha Mola hatowapa nafasi mwaka huu.

  8. misali 09/07/2010 kwa 3:58 mu ·

    haaloooo haaloo comando waudongo mbona kachaka hangari jee sikuhizi hasingwi na mama salma jamani hili dude halina faida kwa wazanzibar aliyoyafanya thidi ya wanyonge MUUGU anamlipa lilikuwa na kiburi sasa limekuwa kama anti RASHIDA ndugu zanguni mpemba wawi ccm na akiwa ccm basi simpemba huyo ni mwan— ccm ni adui wa mzanzibar ikiwa sheni bilali nahoza shamhuna haruni ni maaduwi vibaraka wa watanganyika MUUGU atawafethehi mmoja baada ya mwengine wagelikuwa na uchungu wageikomboa kwenye mikono ya mwabwana zao wa kitanganyika

  9. ucha 09/07/2010 kwa 2:02 um ·

    a.a
    jamani nauliza huyu COMANDOO anaona sasa?

  10. muunguja 09/07/2010 kwa 2:13 um ·

    samini kenda kupiga kura kwenda kutimiza haki yake kikatiba.yeye hana shida anakula bure ni raisi mstaafu. kwanini wapemba mnamuogopa commando?

  11. muunguja 09/07/2010 kwa 2:20 um ·

    @mrfroasty
    wewe kweli umelala tena hata kushinda pono.cuf mshapigwa bao ccm mseto hawautaki si shamsi peke yake majority ya viongozi na wanachama wa ccm hawautaki ,karume peke yake ndio anaeunga mkono.wafuasi wa ccm wengi wao wanataka pure wali sio mseto hio ndio reality ndugu yangu.fanya reserch

  12. mkarafuu 09/07/2010 kwa 2:22 um ·

    MUUNGUJA; sisi wapemba tunamuogopa komando kwa kua ni muuwaji, na mbaguzi na tunamuogopa mtu yoyote mwenye sifa hizo akiwamo DR Bilal.

    Asante.

  13. ali mohammed 09/07/2010 kwa 3:48 um ·

    Loh ! sizia tamu kuliko lala !

    Commando hoyee ! kuonekana tu ,khofu imetanda kwa wanyonge ,yarabi yarabi huyo kankua aanza zake balaa .

    Tuelewe, kila zama zina watu wake, huyo commando wala hasikilizwi tena amedata ,hiyo ndani ndani izirusha akili.

    Ubavu wa kulazimisha CCM -Zanzibar wazi haupo.Tukalie yarabi falaq ,tungojea azaliwe akiwa mtoto vyema ,akiwa taahira vyema mradi tuwe tayari.

    Hahahaaa!

  14. kibakora jaz 09/07/2010 kwa 4:05 um ·

    A/Aaikum

    @MUUNGUJA,ABUU SAID.

    Hivi nyinyi mnaishi ktk dunia ipi?naona mnaongea utumbo kiasi kwamba mnanipa wasi wasi kama nyinyi kweli ni waislam,ndugu zangu ubaguzi wa aina yeyote ile hauna nafasi ktk uislam

    unajuwa ABUU JEHEL alikuwa anajuwa kwamba mtume MUHAMMAD ni mtume wa haki lakini alimpinga kwa nguvu zake zote mpaka akaingia kaburini,na kabla ya kifo chake M/MUNGU aliteremsha aya kwa ajili yake lakini hakubadilika mpaka akaingia kaburini

    Hivi leo ktk znzibar yetu iliotoka ktk wakati mgumu wa kisiasa na kwa kipindi kifupi kila mmoja si cuf wala ccm tulikuwa hatuongei sasa tunaongea,tulikuwa hatuzikani sasa tunazikana,sasa tuulizana,tunakaa pamoja ,tunahurumiana yote haya hayakutokea tuu bali imepita jitihada kubwa ya pande hizi mbili kuelewana .

    Ni jitihada kubwa zilizofanywa na viongozi wetu hawa na sasa nchi inaelekea katika amani,lakini la ajabu kumbe kuna watu wanasikia raha kuona mauaji,dhuluma,ubaguzi,ukandamizaji,ushenzi nakwa bahati mbaya watu hawa wanasema wao ni waisilam.

    mwisho nakusihini nyote mnaoshabikia mambo haya ya kijinga,mnaoshabikia comandoo bilal kuwa raisi kwamba amani hii tulionayo sasa hivi ina thamani kubwa sana, ni wajibu wetu kuienzi na kuiendeleza vinginevyo,vinginevyo?.

  15. muunguja 09/07/2010 kwa 4:22 um ·

    kibakora jaz
    kwanini unachanganya siasa na dini.nyinyi macuf kweli mmechanganyikiwa siasa mnaitia na aya za quran

  16. mrfroasty 09/07/2010 kwa 8:51 um ·

    @Muunguja,

    Mio sio kama nilikuwa sijuwi kuwa wana CCM hawautaki umoja wa kitaifa.Nilichokisema ni kuwa mbona hajatwambia kwenye mahojiano yake na hotuba yake.

    Maana msimamo wa chama cha mapinduzi ni kura ya NDIO, sasa hao wanaopinga wanafuata chama gani?Na hapo ndio anapoonekana mnafiki na msaka tonge.Maana suala la umoja wa kitaifa lina maslahi na Zanzibar,lakini halina maslahi binafsi kwa nafasi yake ya urais.

    Hivyo anapinga kwa kupigania tonge…tumechoshwa na wasaka tonge!

  17. muunguja 09/07/2010 kwa 9:11 um ·

    habari yangu ya matokeo ya kura ya urais ccm kwanini umeifuta .hizo habari ni genuine sheni kapata kura 117.bilal 54 na shamsi 33

Comments are now closed for this article.