M.Seif arudisha fomu

Written by  //  23/08/2010  //  Kitaifa  //  4 Comments

  • Maalim Seif ahimiza uchaguzi wa uwazi

Asema hatakuwa na sababu ya kukataa matoe

Na Mwanajuma Abdi

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha CUF, Seif Sharif Hamad amekuwa wa kwanza kurejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) hapo jana na kuihimiza tume hiyo kusimamia uchaguzi mkuu ujao mwizi Oktoba kwa uwazi.

Fomu hizo alizikabidhi jana kwa Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Salum Kassim Ali, majira ya saa 9 alasiri baada ya kukamilisha taratibu mbali mbali ikiwemo la kupata wadhamini katika mikoa mitano ya Zanzibar.

Mkurugenzi huyo alizikagua fomu hizo na baadae kumkabidhi risiti ya malipo ya shilingi 2,000,000 ikiwa ni dhamana ya mgombea anayewania nafasi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabishi fomu hizo, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alisema katika kinyang’anyiro cha uchaguzi lazima kuna mshindi na aliyeshindwa hivyo akishindwa atakubali matokeo kama ZEC itaendesha uchaguzi wa uhuru na haki.

Alishauri ZEC iendelee kuwa wazi kama ilivyofanya zoezi la kura ya maoni pamoja na kuwashirikisha wagombea watakaoshiriki katika nafasi mbali mbali ili kuondosha matatizo yasitokee.

Aliishauri Tume hiyo kutangaza matokeo mapema, hasa ya Urais mara baada ya uchaguzi na yasikae kwa siku mbili hadi tatu bila ya kutangazwa.

Alisema kufanya hivyo ni kuwapunguzia imani wananchi na wagombea kwa kuwatoa wasiwasi na shaka ya matokeo yanayotolewa.

Wagombea wengine waliochukua fomu kuwania nafasi hiyo ni Dk. Ali Mohammed Shein wa CCM, Juma Ali Khatib TADEA, Haji Ambar Khamis NCCR Mageuzi, Haji Mussa Kitole Sauti ya Umma na Jahazi Asilia

Chanzo:GAZETI LA ZANZIBAR LEO

Na Salma Said,

Maalim Seif wa Mwanzo Kurejesha Fomu

MGOMBEA wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amerudisha fomu za kuwania nafasi ya urais baada ya kukamilisha masharti ya kupata wadhamini.

Maalim Seif ni mgombea wa kwanza kurejesha fomu za kuwania urais wa Zanzibar kati ya wagombea sita wanaowania nafasi hiyo ambao wamechukua fomu kwa tume ya uchaguzi Zanzibar iliyopo Maisara Mjini Unguja.

Akipokea fomu hizo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)
Salim Kassim Ali alisema Maalim Seif amekamilisha utaratibu baada ya kufanyiwa ukaguzi wa awali ambapo amepata wadhamini wa mikoa mitano ya Zanzibar ikiwa pamoja na kukabidhisha shilingi millioni mbili taslim kwa tume hiyo.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukabidhisha fomu hizo Maalim Seif alisema matumaini yake makubwa kwamba uchaguzi unatarajiwa kufanyika octoba mwaka huu utakuwa huru na haki kama ilivyofanyika kura ya maoni mwezi uliopita.

“Napokea fomu za mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF hizi ni fomu za wadhamini kwa ajili ya kuomba nafasi ya urais tunazifanyia kazi zaidi kwa ajili ya kuzihakiki”alisema Kassim.

Maalim Seif allisema dalili za kufanyika kwa uchaguzi huru zimeanza kujionesha pale ZEC ilivyoweza kuonesha uadilifu katika uchaguzi wa kura ya maoni hivyo matumaini yake na chama chake kwamba uchaguzi wa kura za maoni iwe ni kigezo kizuri cha kuigwa katika uchaguzi mkuu.

“Mimi matumani yangu makubwa ni kuona kwamba uchaguzi mkuu wa Oktoba utakuwa huru na haki kwa sababu tumeshuhudia sote hapa kura ya maoni zoezi lake lisimamiwa vizuri na tume hii hii yetu ya uchaguzi ya Zanzibar kwa hivyo nadhani tukitaka tunaweza”alisema Maalim Seif wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za ZEC.

Katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa mzuri na kuweka mazingira mazuri ya kuaminiana Maalim Seif ameiomba tume kufanya kazi kwa uwazi bila ya kuficha ili kutoa fursa ya kuaminiwa katika utendaji wa kazi zake.

Alisema matokeo ya uchaguzi yakianzia katika vituo vya wilayani itaweza kurahishiwa kazi tume hiyo kwani inawezekana kurahisisha kwa kuwa wazi na kufanya akzi kwa wepesi iwapo kila kituo kitakusanya matokeo yake na kuyabandika huku idadi ya vituo vikiwa vingi kama ilivyokuwa katika kura ya maoni.

Alisema kitu ambacho kinapaswa kutizamwa zaidi na kujifunza ili siku za uchaguzi ujao kiweze kurekebishwa ni tume kutochelewa kutoa matokea haraka na kwa wakati.

“Nadhani hili la kuchelewa kutoa matokeo tulirekebishe ili kujenga uaminifu maana ZEC wakati wa kura ya maoni iliahidi kutanagza matokeo lakini walitangaza matokeo ya majimbo matano na baadae wakasita wakaja kutangaza siku ya pili” alisema.

Akizungumzia kadhia ya kupokea matokeo ya uchaguzi ujao Maalim alisema kwamba atakubali matokeo ya aina yoyote katika uchaguzi mkuu kama kushindwa au kushinda has kwa kuzingatia katika uchindani kuna kushindwa na kushinda.

“Mimi nasema nipo tayari kupokea aina yoyote ya matokeo ya uchaguzi najua katiak ushinda kuna kushinda na kushindwa lakini uchaguzi uwe huru na wa haki lakini matumaini yangu makubwa ni kushinda na sio kushindwa” alisisitiza.

Alisema pamoja na kuwa idadi kubwa ya wanachama wa CUF kuwa hawajaandikishwa lakini hao waliokwisha kuandikishwa kama kutafanyika uchaguzi wa haki na uhuru matarajio ni kushinda kwa chama chake.

Alisema kwamba katika zoezi la usajili wa wapiga kura katika uchaguzi mkuu wapo wafuasi wengi wa chama hicho ambao walikataliwa kuorodheshwa katika daftari hilo na kivyo kukosa haki ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu.

“Tungependa wale wote waliokataliwa kuandikishwa waandikishwe ili washiriki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu lakini malalamiko yetu ni kuwa hawa wajaandikishwa na hilo tumekuwa tukilisema sana tu kutaka waandikishwe madhali wana haki zote za kuandikishwa na kushiriki uchaguzi” aliongeza.

Msururu wa magari na mahonda ulimshindikiza Maalim Seif huku idadi ya wanachama wa chama hicho ikiwa kubwa katika sherehe ya kurejesha fomu kwa tume ya uchaguzi Zanzibar.

4 Comments on "M.Seif arudisha fomu"

  1. seif 24/08/2010 kwa 3:34 mu ·

    As,alaikum,mimi namuomba yakarim atujaali uchaguzi wa huru na wa haki.

    Mungu ibariki Zanzibar

  2. Bosco 24/08/2010 kwa 9:26 mu ·

    Ndio maalim wewe ndie rais wetu kwa uwezo wa allah.
    Tunataka wale mapandikizi ktk daftari tusije tukawaona kupiga kura.

  3. zamko 24/08/2010 kwa 11:51 mu ·

    Hapa ilitakiwa iwepo ile kamati ya watu sita na hii ndio iliyopelekea kura ya Maoni ukipita. Ortherwise Wazanzibari wajitokeze kwa wingi in 31.oct. Na wote wanatakiwa wawe walinzi na kujaribu kuwafichua watu wasiohusika kupiga kura.

    Bila ya hayo ZEC ina mushkel. na mimi si-iyamini. Lakini watakapo litotesha . Nawao wata-tota na Watanganyika watazidi kumwagika Visiwani, makanisa yatazidi kutiwa kongrit. Na baadae kuanza kudhibiti mashamba ya minazi na Mikarafuu.

  4. kassim 24/08/2010 kwa 9:55 um ·

    Zamko, inaonekana kama hujaridhika na maridhiano. Bado upo kule kule kwenye majibizano. CUF wao wanaringa kuwa watashinda na hata kaa watashindwa kihalali, serikali ijayo ni ya pamoja. Sasa hii si hatua nzuri. Huwezi tu kuamka kesho ukawa kama Malaysia. Hata hao Malaysia na Singapore, waliaandaa watu nandio maana leo zikawa zinang’ara. Jaribuni kuelekeza maoni yenu juu ya serikali ya umoja wa kitaifa vipi munataka iwe na vipi inaweza kufanikiwa. Haya magovi yasiyo kusha hayasaidii kitu. Jana na juzi, Pakistan na India walikuwa maadui wawili, leo India anampa Pakistan $5,000,000.00Millions kama mchango wake. Pakistan imechukuwa masiku kukubali kuzipokea. Ujirani mwema ndio unao takiwa. Sasa na sisi kila siku tukiwa tunatukanana na kupeana majina mabaya, kesho tukifikwa na majanga, tusubiri msaada kutoka EU?

    Mambo mengi sababu ni sisi wenyewe hatuko tayari kujirekebisha. Kuanzia Mapinduzi, Muungano, kufa kwa ASP, kufukuzwa akina Maalim Seif, chanzo ni sisi wenyewe. Tulipo amua na kuachana na akina makamba, mbona maridhiano yamepatikana. Ramadhan ya mwaka huu tunaifunga kwa amani kabisa na furaha. Tunaingia kwenye uchaguzi hata watu hawajuwi kama kuna uchaguzi. Mh Jussa alisema kule kwenye mtandao wa facebook, kuwa Wazanzibari wengi waliopo tunapenda kuona sisi ndio tuko sahihi kuliko wao wanakula moto.

Comments are now closed for this article.