Mamia Wamzika Mufti wa Zanzibar
Written by administrator // 31/08/2010 // Kitaifa // 11 Comments
Na Salma Said,
RAIS wa Zanzibar Amani Abeid Karume jana ameongoza umati mkubwa wa waumini wa kiislamu katika ibada ya sala ya mazishi ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Zanzibar Marehemu Sheikh Harith Bin Khelef Bin Khamis.
Ibada hiyo ilifanyika katika msikiti wa Al Mushawar uliopo Mwembeshauri mtaa wa Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi kabda ya kwenda kupelekwa kijijini kwao Muyuni mkoa wa kusini Unguja.
sala hiyo ilifanyika majira ya saa 3:00 asubuhi na kuhudhuriwa na waumini wengi wa dini ya kiislamu ambapo wananchi waliohudhuria mazishi hayo walimuelezea Mufti katika uhai wake alikuwa ni kiongozi asiyependa kujionesha khsa kutokana na tabia yake ya upole na asiyependa misukosuko katika maisha yake.
Waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali na makamo wa rais wa Jamhuri ya Muungano Dk Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, Naibu waziri kiongozi, Ali Juma Shamhuna na mawaziri wa serikali ya mapinduzi Zanzibar.
Awali maziko ya Marehemu Mufti yalikuwa yafanyika juzi lakini kutokana na sababu mbali mbali za kutokufika kwa wakati mwili wa marehemu ilishindikana kuzikwa kwa wakati ulipangwa.
Juzi mwili wa marehemu Mufti ulikwama nchini Doha kutokana na baadhi ya nyaraka za mwili huo kutokamilika na hivyo kushindwa kupakiwa katika ndege iliyopangiwa ambapo mwili huo ulipetwa kwa siku ya pili.
Watu aliokuwa karibu na marehemu Mufti wamemuelezea kwamba ni mtu aliyesoma na alikuwa akiheshimu sana elimu yake kwa vitendo ambapo moja ya sifa yake ilikuwa ni kutokupenda kujiingiza katika malumbano ya aina yoyote aidha iwe ya kidini au kisiasa.
Mufti mkuu wa Tanzania sheikh Shaaban bin Simba alimuelezea marehemu Mufti wa Zanzibar alisema ni kiongozi aliyekuwa na upeo mkubwa katika taalumu ya dini ya kiislamu na alikuwa ni mtekelezaji wa vitendo vyema ambapo busara na hekma alikuwa akiitumia sana katika kutatua mambo mengi katika jamii.
“Namfahamu sana alikuwa kiongozi anayeheshimika na kuaminiwa na waumini wa dini ya kiislamu lakini hata kwa wasiokuwa waislamu marehemu Mufti alikuwa akiwaheshimu sana na ni mtu ambaye ametumia elimu yake vizuri sana” alisisitiza Mufti mkuu wa Tanzania.
Sheikh Shaaban Bin Simba juzi aliongoza ujumbe wa viongozi wa dini kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakati ndege uliyokuja na maiti kuwasili aktika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kufanyiwa sala maalumu ya maombi.
Mbali na viongozi waliohudhuria wakiwemo masheikh na maimamu katika sala hiyo ya juzi waliongozwa na rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye ni miongoni mwa watu wanaomfahamu sana marehemu Mufti.
Marehemu Mufti wa Zanzibar alifariki dunia wiki iliyopita nchini India ambapo alipelekwa baada ya kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na tatizo la mkojo na figo, hadi mauti yanamfika marehemu alikuwa Mufti wa Zanzibar. Marehemu Mufti ameacha mjane mmoja.






11 Comments on "Mamia Wamzika Mufti wa Zanzibar"
Ndugu waandishi inafaa musome kabla ya kuandika kwenye magazeti au mitandao.
Doha si nchi ni mji mkuu wa qatar
Pia luandika ugonjwa wa mtu bila ya idhni yake ni kosa la jianai ,sijui nani kakupa idhni ya kuandika ugonjwa uliokuwa ukimsumbua marehemu.
Kuandika au kutaarifu kwamba alikua mgonjwa iantosha
@Jaluo,
Kama sikosei taarifa za sababu ya kifo cha Mufti ziliripotiwa kutolewa na wanafamilia yake na ofisi ya Mufti na mwandishi kama asingepata huko wala asingeandika,mengine ni makosa ya uhariri tu au uchapaji, hii huweza kumtokea yoyote.
Hata wewe ukisoma ulichoandika utakuta kuna makosa mengi tu mfano, “Qatar” wewe umeandika “qatar”, mstari wa tatu ulikusudia kusema “kuandika” wewe umeandika “luandika”, “jinai” wewe umeandika “jianai”, mstari wa mwisho ulikusudia “inatosha” wewe umeandika “iantosha”.
Kwa hiyo na wewe kabla ya kuchapa maoni yako uyahariri kwanza, kama umesahau basi unasameheka kwa kuwa kusahau ni dharura inayokubalika wakati fulani,hivyo ukubali kuwa na mwandishi au mhariri naye kasahau na siyo kama hajuwi kuwa Doha ni mji mkuu wa Qatar.
Huenda na mimi nimeandika makosa humu lakini na appreciate habari ya D’Salma kwa kuwa nimeifahamu na mapungufu kiduchu kama hayo yanasameheka.
J
Mimi nauliza kwani kulikua na ulazima gani wakuisafirisha hiya maiti mpaka ikabidi icheleweshwe kuzikwa namna hiyo?
Au ni sunna au ni faradhi mtu kuzikwa kwao? Jee kuichelewesha maiti si makosa?
NAOMBA MUNIJUVYE HIVI SHEIKH WETU ALIKUWA AKIENDESHA DARSA MIKITI UPI? HIVI SHEIKH WETU JEE ALIWAHI KUANDIKA KITABU AU KUSHEREHESHA KITABU AU KUTAFSIRI KITABU? JEE SHEIKH WETU AMETUACHIYA KITU GANI SISI WAISLAMU WA ZANZIBAR AMBACHO DAIMA HAKITOSAHAULIKA NDANI YA JAMII YA WAISLAM.
SHEIKH WENGI ZANZIBAR WAMEACHA ATHAR ZILIZO NZURI NA BADO ZINABAKIA NDANI YA MAISHA YETU. MFANO SHEIKH ABDALLAH S. ALFARSY, BIN SUMEIYT, AMIR TAJO, NA WENGI TU MCHANGO WAO BADO NI KUBWA.
NAWAOMBA WAISLAMU MUNIFAHAMISHE.
ALLAAHUMMA INNAKA A’FUWWUN TUHIBBU L-AFWAA FA-AFANNAA YAA KARIYM L-AFWA.
@Kwaomtu,
Alikuwa Mufti, mtu mpole,hakupenda misuguano na watu,kasoma sana hawa akijivuna..hayo na mengine mengi ni mazuri ya kuigwa, na yeyote akiiga hayo tu kihakki Lillahi basi atapata athari nzuri katika maisha yake. Au hizi haziwezi kuwa athari nzuri kwa maisha ya mtu?
J
Assalam alaykum!
Kusema kweli, ukiwa Mufti kwa nchi ya Tanzania, basi inakuwa kama umekwenda kujitia mashakani. Na wengi wa Mashekhe hukwepa kuchukuwa dhmana hiyo. Ndio maana sasa hivi unaweza kuona viongozi wa dini wengi ni watu wenye asili ya bara.
Sheikh Abdalla Bin farsy, alipo ona nchi inakwenda vibaya. Heshima imepotea, huyo akaondoka. Kufika Mombasa, tunaelezwa Muftsi wa Mombasa au tuseme wa Kenya nzima. Akamwambia Kenyata, mimi siwezi kuongoza Wa-Islamu wakati kuna A’Alimu mkubwa ndani ya nchi. Kenya akatowa baraka zake na Sheikh Abdillah Alfarsy akashika u-Mufti. Ametafsiri Qur-an ka Kiswahili tokea miaka ya 1950′s. Amenadika vitabu vingi na aliweza hata kuandkia mambo mengi juu ya Makadiani. Alikuwa mweledi wa kuzungumza na kuandika Kiarabu na English. Nisije kufahamika nasema Almaruhum Mufti wetu Harith, laa hasha sin ubavu huo. Ninacho sema kufanya kazi n SMZ, unakuwa hupo huru. Unaburuzwa tu. Ninavyo sikia Muft alikuwa mikoani Bara na huko ndiko alipo kuwa akifanya shughuli zake za dini, za kutowa Ma-darsa makubwa maubwa. Kuja kwake ni kwa ombi la aliyekuwa Rais wa Zanzibar Dr Salmin Amour.
-Nami tokea jana nilipo soma Maiti yake imesahauliwa na kupeleka ucheleweshaji wa mazishi yake. Nikahudhunishwa sana, kwamba maiti imekua haina thamani kiasi hichi. Na kitendo hicho kinafanyika ndani ya nchi ya Ki-Islam nahuyu ni kiongozi wa dini wa nchi. Ilikuwaje viongozi wa msafara ule washindwe kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa sawa. Nadhani ni Soraga huyu huyu aliye fanya uzembe, akapoteza pesa briefcase nzima ya madola ya pesa za msafara wa mahujaj.
-Jambo jengine, ukienda kwenye darsa, tunaambiwa maiti haicheleweshi kuzikwa. Na anatakiwa azikwe pale mahala alipo kufa. Haya hutendeka kwa watu wa kawaida, lakini akifa Sheikh mkubwa, hatuoni kutendeka. Kidogo hapa nashindwa kupata jibu, kwa hiyo kwa yule ambaye anaweza kutupa ufafanuzi, naomba atusaidiye.Suali langu jee hii inakubalika kwa kesi ya maiti ya A’alim kama Mufti wetu, au Masheikh kama vile Abdalla bakathir, kwani yeye ya kwake ililetwa Zanzibar kutoka India?
Haya ni mambo ya dini. Kama nimekosea pahala, basi naomba radhi, isije ikaanza kuleta mizozano na mambo ya kurekeshina tu. “Hapa kidogo Kassim umekosea, rekebisha kauli hii na hii” na mimi nitafahamu.
Maasalam
kassim
mie sio mtaalaam wa mambo ya dini lakini ninavyo fahamu dini inaelezea mtu anpokufa azikwe hapo hapo na bila kukawia au kucheleweshwa. mfano mzuri wa kuigwa ni ndugu zetu mashnashir huzika hata usiku wanapofikwa na msiba.
ahlan wasahlan akhwan assalaam allaykum natumai nyote wazima ndugu zangu wa kiislam.
@kwaomtu inshallah nitajaribu kukutafutia majibu ya maswali yako lakini kwa habari za juu juu nilizonazo kuwa mufti alikuwa ni mcha mungu aliyekuwa ana ilmu kubwa sana lakini hakuwa ni mtu mwenye kujulikana sana. nasikitika jana nilichelewa kuhudhuria katika mazishi kutokana na taarifa zilotolewa kabla lakini ningelipata mengi ambayo ningeweza kukupa faida pamoja na wanaukumbi wengine kwa ujumla.
ramadhan mubarak.
SH ELIMU NI MIONGONI MWA SADAKATIL JAARIYA IKIWA TU UMEWACHA WANAFUNZI WAKAENDELEZA ELIMU, UMEWACHA VITABU WATU WAKAFAIDIKA NA ELIMU ULIYOICHAPISHA, UMEWACHA ASASI AMBAZO MITAJI YAKE ITATOWA NAFASI NA KUENDELEZA ELIMU, AU UMEJENGA MAJENGO AMBAYO YANATUMIWA KWA MISINGI YA ELIMU.
KUFARIKI NA ELIMU UKAENDA NAYO KABURINI HILO SI JAMBO LA BUSARA. MIMI SIKATAI KUWA MUFTI ALIKUWA NA ELMU KUBWA, NA ALIKUWA NI MAJI MAKUBWA MASHAALLAH, ILA NAOMBA KUJUWA MIONGONI MWA FATWA ZAKE, VITABU VYAKE, NA DARSA ZAKE. SITATI NIFAHAMIKE YA KUWA NAMSEMA MAREHEMU KWA UBAYA, ILA NATAKA NASISI TUJUWE KUWA ELIMU TUNAYOJAALIWA JAPO NDOGO KIASI GANI BASI TUJITOLEE MUDA WETU KWA MASLAHI YA KUENDELEZA JAMII YETU KABLA YA KUFIKWA NA MAUTI TUKAANZA KUIFIANA MAKABURINI, WAKATI UKWELI UKO WAZI KWENYE JAMII ZETU.
ALLAH SUBHAANA WATAALA ANASEMA, NA TOWENI TULIVYO WARUZUKU KABLA MMOJA WENU HAYAJAMFIKIA MAUTI, ATI HAPO TENA NDIPO AKAJA AKASEMA LAITI NINGELIAKHIRISHIWA MUDA MDOGO TU.
PIA ALLAH SUBHAANA ANASEMA KWENYE AYA NYENGINE HAKIKA MAUTI YANAPOWADIA HAKUNA WAKUYACHELEWESHA SAA WALA DAKIKA.
ALLAHUMMA INNAKAA AFUWUN TUHIBBU L’AFWAA FA’AF-ANNAA YAA KARIIM L’AFWA.
Assalam aleykum
Nafikiri suala la Al Marhum Sheikh Harith bin Khelef limekwisha.Si busara sasa kumuangalia yeye wakati ameshatangulia mbele ya haki.Huu ni wakati wa kujiangalia sisi na safari yetu ya akhera
Unajuwa unaweza kuandika kitabu cha dini au ukawa ni mtu uliyetowa ftwa fulani, mashekhewengine au wanavyuoni wanaanza kukuanalia. Huyu aliyetowa Fatwa, amesoma kwanani na nani. ahaa amepita hapa na hapa, aksomeshwa na Al’liim huyu na huyu. Usifikiriye utakwenda Makka na Madina ukasema una Phd yako ya dini umechukuwa Wales au oxford university, ukasikilizwa.
Siku hizi tumekuwa wazito wa kutaka kujuwa mashekhe zetu. Kwenye gazeti la Dira kulikuwa na ukurasa, linazungumzia mashekhe zetu walio kusha kutangulia na mambo yao. Sijuwi akina Almarhum Ahmed, Bin Sumeit, Hassan Bin Ameir, sijuwi Aa’lim kutoka Dodoma… Kulikuwa kuna ordha ya Masheikhe wa Afrika mashariki nzima.
Kwa hiyo unapoulizia elimu ya mtu unapata kujuwaMarehemu wetu ametowa wanafunzi hawa na hawa, kwa hiyo kama hukubahatika kusoma kwake unaweza kupata kwa wanafunzi wake, kwa yule mwenye nia ya kweli ya kutaka kusoma. Hawa Masheikh zetu walijisomea si zaidi a afrika mashariki, lakini wana elimu na hikma kuliko vijana wa siku hizi wanaosoma Makka na Madina. Yote wakienda huko hufuata pesa na si elimu. Mtu akipata nafasi ya Sudan au Misri anaanza kuikwepa.