Waangalizi uchaguzi mkuu – 2010

Written by  //  06/09/2010  //  Kitaifa  //  5 Comments

Na Salma Said,

JUMLA ya waangalizi 7,210 wanatarajiwa kusimamia mwenendo wa uchaguzi mkuu katika maeneo yote ya Tanganyika na Zanzibar unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini.

Mratibu wa kamati ya kuangalia uchaguzi Tanzania (TEMCO) Dk Benson Banna aliwaambia waandishi wa habari wakati akizungumza juu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu katika ukumbi wa Sauti ya Zanzibar, Rahaleo Mjini Unguja.

Alisema TEMCO itatuma waangalizi 210 ambao ni waangalizi wa muda mrefu na waangalizi 7,000 wakiwa ni wangalizi wa muda mfupi kwenda kuangalia mwenendo wa uchaguzi ambao watapelekwa katika vituo vya kupigia kura vyote nchini.

Mratibu huyo alisema jumla ya vituo 6,650 kwa upande wa tanznaia bara na vituo 700 kwa upande wa Zanzibar vitakuwa vikitembelezwa na kukaguliwa na waangalizi hao ambao yatari wameshafanya matayarisho na kuomba kibali cha kufanyia kazi hiyo.

Lengo la TEMCO alisema ni kuwepo kwa uchaguzi huru na haki kwani hiyo ndio nguzo ya demokaraia na zoezi hilo la kuangalia na kufuatilia mwenendo wa uchaguzi litajieleza kwenye kutathimini uwazi, uhuru, na haki katika mchakato wa uchaguzi mzima.

Alisema waangalizi wote wale wa muda mrefu na wa muda mfupi wote wamepatikana kwa kutumia mfumo stahili kwa kutafuta vigezo, sifa, na uzoefu mkubwa walionao waangalizi hao katika chaguzi zilizopita.

“Waangalizi wetu hawa wote wamepewa mafunzo kuhusu stadi za uangalizi wa uchaguzi, ikiwa pamoja na maelekezo ya mambo ambayo waangalizi wanatakiwa kuyafanya na yale ambayo hawatakiwi kuyafanya kama walivyoelekezwa na tume zote mbili za uchaguzi” alisema Mratibu huyo ambaye alifuatana na Makamu mweyekiti wake Maryam Abubakar.

Dk Alisema waangalizi hao yatari wameshaeleweshwa kuhusu taratibu za kisheria na kitaasisi zinazotumiwa katika uchaguzi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na wa Zanzibar.

Mambo ambayo yataangaliwa zaidi ni na waangalizi hao ni masuala ya kisheria, ufanisi wa vyombo vinavyosimamia uchaguzi na utekelezaji wa sheria ya gharama za uchaguzi.

Akiyataja mambo mengine Dk Banna ni uteuzi wa wagombea, kampeni za vyama vya siasa, uwiano wa kijinsia, katika siku ya upigaji kura na mwenendo wa upigaji kura, kuhesabu, ujumlishaji wa kura zenyewe utangazaji wa matokeo na matukio yote yatakayofuatia baada ya kutangazwa kwa matokeo.

Aidha alisema suala la rufaa na namna amabvyo rufaa na malalamiko yatakavyoshughulikiwa ni miongoni mwa mambo ambayo yatafuatiliwa na waangalizi wa kamati yake.

Dk Banna alisema kabla ya zoezi hilo timu ya TEMCO ilitumwa Zanzibar kuangalia uandikishaji wa wapiga kura na uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia Octoba 10, 2009 hadi Juni 2010 huku wataalamu wake kuhudhuria mikutano mikuu malumu ya vyama vya siasa kwa lengo la kuangalia uteuzi wa wagombea urais na wagombea wenza.

Alisema Agosti 2010 TEMCO ilipeleka wangalizi wa ndani 62 katika majimbo yaliyoteuliwa kama mfano kuangalia uteuzi wa ndani ya vyama ambapo ulilenga kuvipatia vyama wagombea wa nafasi ya ubunge, uwakilishi na udiwani nchi nzima.

TEMCO inaundwa na asasi za kiraia (AZAKI) zipatazo 152 ikiwa ni pamoja na asasi za kidini, kamati ya TEMCO imekuwa ikiangalia mwenendo wa uchaguzi tokea mwaka 1995 kwa upande wa Zanzibar TEMCO ilianza kuangalia uchaguzi mwaka 2000 na kufuatia chaguzi ndogo za Pemba za mwaka 2003 na uchaguzi mkuu wa 2005.

Taasisi kiongozi ya TEMCO ni Mpango wa utafiti na Elimu ya Domokrasia Tanzania (REDET) ambayo iko chini ya Idara ya Sayansi ya siasa na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam idara yenyewe imekuwa ikiangalia na kufuatilia mwenendo wa chaguzi za Tanzania tokea mwaka 1965.

5 Comments on "Waangalizi uchaguzi mkuu – 2010"

  1. kitahanani 06/09/2010 kwa 9:48 um ·

    Mbona waangalizi ni wengi kuliko wapiga kura maana wako milioni saba!!!
    Mnaopandisha hizi makala huwa mnazipitia jamani? Vitu vidogo kama hivi vinaweza kufanyiwa marekebisho kabla ya kupandishwa.

    • Administrator 06/09/2010 kwa 9:55 um ·

      @Shukurani Kitahanani,

      Nimeichapa lakini hio nambari kwa kweli sina uhakika nayo, inawezekana ubinadaamu umepita hapo.Nimepiga mstari bila ya kuirekebisha.

  2. ashakh 06/09/2010 kwa 11:28 um ·

    Shukran Da Salma, mwache huyo KITAHANANI ahanike na hizo figure wakati zimeshapigwa mstari kuonyesha kuwa zimekatwa.

    Nilichokipenda Da Salma ni hii paragraph yako ya kwanza, uliposema:
    “..katika maeneo yote ya Tanganyika na Zanzibar unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini.”

    Hivi ndio tunavyotakiwa kusema, kuandika, kutangaza, nk kwa mambo yote yanayohusu ndani. Kwa yale mambo ya nje tunaweza kusema hiyo Tanzania. Ndio wenzetu watakapotambua au tuwambulishe hilotaifa lao japo kuwa hawalitaki, tuwalazimishe mpaka watalitaka.

    Mambo ya Zanzibar kwa wasaaa yatajwe Kizanzibar na yale Ya Tanganyika pia yatajwe kwa UTANGANYIKA. Tuone jee jirani zetu watafanya nini.

  3. Elbattawi. 07/09/2010 kwa 1:44 mu ·

    Naungana na Ashakh kwa kuzidi kumpongeza mwandishi wa habari hii kwa kufafanua na kuweka wazi jina la Tanganyika, wala sidhani kuwa hilo ni kosa, labda hao wenye Tanganyika yao wasiridhike na jina hilo. Nadhani kwa uono wao mdogo na hasa wale waliozaliwa kabla ya Aprli 26, 1964 wanaweza kuona hilo jina limepitwa na wakati.

    Kwa upande wa pili mshangao utakuja kwa wale waliyozaliwa baada ya Aprili 26, 1964.
    Hawa hatuwezi kuwaangushia lawama sana kuhusu jina la asili la nchi yao kwani, tangu wazaliwe wanasikia Tanzania bila ya kupewa maelezo ya kutosha kuwa nchi yao jina lake hasa ni Tanganyika. Jina la Tanzania ni jina la Serikalia ya Muungano tu na si jina la nchi.

    Hapa utaona kuwa hawa vijana wa Kitanganyika waliyochini ya miaka 40 ndio tatizo kulikubali jina la Tanganyika kwa ukosefu wa kupatiwa au kusomeshwa historia ya kweli ya nchi yao. Hatuwezi kuwalaumu kwani ni kosa la wazee wao kina Nyerere, walioua kwa makusudi jina la Tanganyika kwa lengo la kuimeza Zanzibar.

    Kuna wakati katika utawala wa Nyerere katika bunge la Muungano, kuliibuka tifu kubwa la wabunge wa Muungano kwa upande wa Tanganyika akina Njelu Kasaka, kudai kuwapo kwa Serikali tatu, ili Tanganyika iwe na Serikali yake. Kundi hilo la wabunge wa Tanganyika lilijipa jina la G55 na lilipata baraka za waziri mkuu wa wakati huo, nadhani alikuwa ni John Maleccela.

    Ushauri wa Ashakh kwa mwandishi wa habari hii (Bi. Salma) kwamba kila yanapojitokeza maswali ya ndani ya nchi mbili hizi yaani Tanganyika na Zanzibar, litumike jina la Tanganyika, ili tuone “reaction”; yake yaani vipi wata-react!!..

    Maoni yangu kuhusu sisi tunaotoa maoni, tusiwe na tabia ya kulaumu ovyo ovyo kwa makosa ya kibinaadamu. Kwa mfano hata huyo Kitahanani anayekosoa na yeye pia amekosea. Angalia neno hili “Mnaopandisha”; hapa alikusudia kuandika “mnapoandika hizi makala”; angalia kosa jengine “Kupandishwa”, hapa alikusudia – kufanyiwa marekebisho kabla ya kuandikwa. Dada yangu (sasa ni marehemu)aliwahi kunambia siku moja kuwa ustaarabu mwingi ni ujinga. Utamwambia vipi mwenzako kuwa unanuka wakati wewe mwenyewe vundo tupu.

    Kabla ya kumkosoa mwinzio jitazame wewe uko uko ok?..

  4. ashakh 07/09/2010 kwa 8:56 mu ·

    Lakini Albattawi, sisi Wazanzibar tunaojinadi kuwa ni Wazanzibar na hatutaki tuitwe Watanzania, wengi wetu tumezaliwa baada ya huo Muungano. Zaidi tunaambiwa Wazanzibar tuwajinga, wenyewe kwa nguvu zetu tumeitafuta na tumeisoma historia nakuweza kuijuwa, alaa Zanzibar ni nchi.

    Nambieni katika miaka ya 70s na 80s Zanzibar ikiitwa Tanzania Visiwani. Mbona jina halikuendelea? Wazee wetu ilionekana, pamoja na kuwa hawakuridhika, wameshalikubali hili jina.

    Tatizo ninalo liona ni Hichi kizazi cha Kitanganyika na ujinga wao wenyewe. Binafsi nitawalaumu kwani ukweli upo, unaonekana, unajulikana. Hata ukiwambia haya ni maji wanakwambia huu ni moto.

    Hawa vijana wengi ndiowako mamtoni, lakini mawazo yao ni yaleyale ya KUJULIUS. Sitomlaumu baba yao bali wao wenyewe. Sijuwi niwafikiri vipi kwani au kile wanachokitaka ni nini. Kwa kweli nimshangao mkubwa kuliko hiyo alama yenyewe ya Kushangalia.

Comments are now closed for this article.