Watano warudisha fomu
Written by Mrfroasty (Ufundi) // 28/06/2010 // Kitaifa // 6 Comments
Salma Said,
JUMLA ya wagombea watano wanaomba kuteuliwa kugombea nafasi ya urais wa Zanzibar kupitia CCM jana walirejesha fomu zao baada ya kukamlisha kazi ya kutafuta wadhamini, Unguja na Pemba .
Dk Ali Mohammed Shein, alikuwa ni miongoni mwa waliyorejesha fomu katika ofisi kuu ya chama hicho Kisiwandui mjini hapa na kufuatiwa na waombaji wengine.
Katibu wa Idara ya Oganazesheni ya Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar, Bi Asha Abdallah Juma alifanya kazi ya kupokea fomu hizo na kuzikaguwa kama zimejazwa kabla fomu hizo kuwasilishwa katika mkutano wa kamati maalum ya wajumbe 80 wa NEC Zanzibar siku ya jumamosi kuwajadili na kutoa mapendekezo yao .
Dk. Shein alirejesha fomu Makao Makuu ya CCM Kisiwandui saa 8:00 mchana baada ya Bw Hamad Bakarii Mshindo na kufuatiwa na Bw Ali Karume, Mohamed Aboud Mohamed, na wa mwisho alikuwa Bw Shamsi Vuai Nahodha.
Mgombea wa kwanza kurejesha fomu alikuwa ni Waziri Kiongozi Mstaafu Dk. Mohammed Gharib Bilal, ambae alirejesha fomu yake jumamosi iliyopita na baadae kupokewa na umati wa wanachama wa CCM kutoka Mikoa mitano ya Zanzibar, katika viwanja vya Mwembe Kisonge mjini Zanzibar.
Dk. Shein aliwashukuru wananchi waliojitokeza kumdhamini na kuahidi atakutana nao tena kutoa shukrani iwapo atashinda au kushindwa katika mchakato huo unaofikia tamati Julai 9 mjini Dodoma .
“Nawashukuru wanachama wote waliojitokeza kunidhamini na nitarudi tena kuwashukuru katika Mikoa yote ya Zanzibar ”, alisema Makamo huyo wa Rais.
Alisema kwamba vyovyote itakavyokuwa katika kumtafuta mgombea wa rais wa Zanzibar atahakikisha anarudi tena kwa wananchi kuwashukuru yawe matokeo mabaya au mazuri.
Dk. Shein alisindikizwa wakati wa kurejesha fomu na mkewe pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Meja Mstaafu Kassim Tindwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Issa Ahmed Othman.
Mshindo aliwashukuru wananchi waliojitokeza kumdhamini kwa vile hatua hiyo ndio imewezesha kurejesha fomu zake katika muda muafaka na kuongeza kwamba hakupata shida yoyote ya kuwatafuta wadhamini wake.
Balozi Ali Karume, alisema kwamba alikuwa akilazimika kufanyakazi hadi usiku kwa kusajili watu waliojitokeza kumdhamini kutokana na wingi wa watu.
Bw Aboud alisema kazi ya kusajili wadhamini haikuwa ndogo kutokana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kumdhamini.
Aboud alisema anamategemeo makubwa ya kufikia malengo ya ksiasa katika mchakato huo na kuwashukuru wanachama wote waliojitokeza kumdhamini Unguja na Pemba .
Aidha Bw Shamsi alisema anamatumaini makubwa ya kupitishwa na chama lakini ataheshimu matokeo yoyote kutoka Dodoma Julai 9.
Wagombea ambao bado hawajarejesha fomu zao ni Mfanyabiashara Mohammed Raza Dharamshi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri Kiongozi Ali Juma Shamuhuna, aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Omar Sheha, Raza na Mwanadiplomasia Mstaafu Muhammad Yussuf Mshamba.
Wakati huo huo RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume ametoa wito kwa Wazanzibari wote kwenda vituoni mwao kwa ajili ya kuchukua Shahada zao za kuandikishwa kwani ni haki yao ya msingi.
Rais Karume aliyasema hayo leo mara baada ya kuchukua shahada yake ya kuandikishwa mpiga kura katika kituo cha skuli ya msingi ya Kiembesamaki mjini Unguja.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua shahada yake, Rais Karume alisema kuwa utaratibu uliopo ni mzuri na unatoa nafasi kwa kila mwenye haki ya kupiga kura kupata fursa hiyo,hivyo alitoa wito kwa wananchi kuitumia fursa hiyo.
Rais Karume ambaye alifuatana na Mama Shadya Karume, alisema kuwa hatua hiyo inaonesha mwanzo mzuri ambao unaepuka malalamiko na kuondoa mzizi wa fitna.
Mwisho.
[nggallery id=20]






6 Comments on "Watano warudisha fomu"
Wagombea wote wamesema wao haswa watahakikisha wanasimamia sera za chama cha Mapinduzi, na hususan ile ya kuleta umoja na mshikamano kwa kuweka serekali moja.
Wagombea wote wansema muda umekuwa mrefu, ni takriban miaka 50 Chama Cha Mapinduzi kinasubiri uitekelezaji wa ilani yake ilioasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kutumia serekali mbili.Hivyo wakipewa nafasi ya urais, watatekeleza kwa haraka sera hii ya Serekali Moja kuhakikisha muungano wetu unadumu kama chuma!
Mbali na hayo wagombea wamesema ili kupata ufumbuzi wa kero zote za muungano, hakuna budi Zanzibar isarenda kila kitu chake kwa Tanganyika.
Hio ndio habari kwa ufupi,
Nawasilisha
mrfroasty
wewe mfloasty iyo itakuwa bola yaani, tuwe na selekali moja tu kwasababu wazanzibali wenyewe hawataki kuwa na selekali yao na sisi tuwe na yetu. mimi nataka muwe na yenu rakini naona hamutaki mumekuwa mdobwedo hahahaha
tanganyika oyeeeeeeeee zanzibali oyaaaaaaaaaaaaaa
@Kirinjiko
Usije kujisahau tuu, MZALENDO.net ni mtandao specifically kwa ajili ya wazanzibari na NA SIO WATANZANIA….Tunakumbushia tuu, usije dhani upo JF hapa.
Hivyo ni vyema ukafahamu kuwa kuwa kati-kati ya umma wa kizanzibari, jokes za kudhalilisha wazanzibari hazitafumbiwa macho!
Asalam alaik mimi nafkiri wote ambao wamechukua fomu kwa upande wa ccm znz sio kwa ajili ya ukombozi wa znz ila ni kuendelea kutumaliza na kufuta taifa la znz kwa hiyo napenda kuwaambia kwa wale wote ambao wanipenda znz tusiwe na ushabik mara hii kwa kupoteza kura zetu kwa watu ambao hawaitakii mema nchi yetu zaidi ya kuangalia matumbo yao na maslahi ya mabwana zao bara .tuangalie mfano mmoja kia mooja anasema atatekeleza ilani ya ccm ambayo ni kutuchimbia kaburi na kutuletea ubaguzi uasikini hakuna hata mmoja ambae anasema anataka mariziano ya wazanzibar kwa maslahi ya taifa la znz na watu wake
Mbona hawa wagombea wamenenepeana kiasi hichi? Hakuna hata mmoja aliye mwembamba. Shemsi alikuwa ujiti miaka 10 iliyopita. Leo kavimba huyu utafikiri ametiwa hamira.
Sasa njoo upande wa wananchi uone jinsi tulivyo dhofu -el-hali. Kweli madaraka matamu. Kiasi akina Shemsi waseme wanataka wapandishwe cheo kutoka kondakta kwenda udereva kamili. Jee Shemsi umeshapita kwa SILVA au ndio umegaiwa leseni?
nawapongeza wote walorejesha fomu na mungu atawajalia mchakto mwema na atawapa uwezo walobakia kurejesha fomu salama na tutampata mgombea wa CCM-ZANZIBAR kwa amani na utulivu ili awenze kutuongoza znz kwa misingi mizuri
ahsante