Wazanzibari kula vyakula vibovu!

Written by  //  06/09/2010  //  Kitaifa  //  7 Comments

  • Bodi ya chakula na vipodozi inafanya kazi gani hadi vyakula vibovu vinaingia nchini ?

Na Salma Said,

WANANCHI wametakiwa kuwa makini na bidhaa zinazoingizwa nchini ambazo nyingi zimemaliza muda wake hasa katika kipindi hiki cha kukaribia sikukuu baada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.

Tahadari hiyo imetolewa na wataalamu wa afya baada ya kugundulika kuwa bidhaa nyingi zisizofaa kutumika kwa matumizi ya binaadamu kuingizwa nchini na kutumiwa na wananchi mbali mbali mjini na vijijini.

Hivi karibuni Bodi ya chakula dawa na vipodozi ya Zanzibar imekamata tani 245 za mtama na tani 193 za mchele kutoka nje ya nchi vikiwa vimeharibika na havifai kwa matumizi ya binadamu huku vikianza kutoa harufu ya kuharibika.

Kukamatwa kwa bidhaa hizo kumekuja huku bidhaa hizo zikitumika sana katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani ambapo bidhaa nyengine kama hizo zilizoharibika zilirudishwa zilikotoka kama siku za hivi karibuni.

Aidha hali hiyo imekuja zikiwa zimepita siku chache tangu kumalizika mkutano wa wadau wa nchi za Afrika mashariki na kati uliofanyika Zanzibar ambao ulibaini kuwepo kwa bidhaa nyingi zikiwemo dawa bandia katika ukanda huu.

Mrajis wa bodi ya chakula, dawa na vipodozi, Dk Burhani Othman Simai alisema mtama huo katika ujazo wa mifuko ya kilo 50 haina nembo yeyote uliingizwa Zanzibar kwa meli ya M/V RYU GONG kutoka Korea ya Kaskazini.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya bodi namba 2 ya mwaka 2006 mmiliki wa mtama huo Khatib Shamtana atapaswa kugharamia uangamizaji wake ambapo shilingi milioni 3 zitahitajika katika uteketezaji wa mali hiyo.

“Mtama tumepita katika maabara na umebainika haufai kutumiwa na hauna tarehe ya mwisho wa matumizi na tuliukamata ukiwa unataka kuingizwa katika soko hapa Zanzibar ”Alisema Dk Simai.

Mbali na mtama pia mchele aina ya Rose Brand Rici uliingizwa Zanzibar kutoka Pakistan ambapo pamoja na muda wa matumizi ulionyesha Mei 2012 umebainika haufai kutumiwa kwa matumizi ya binadamu.

Dk Simai alimtaja milki wa mchele huo kuwa ni mwanamke aitwaye Sabahi Said ambaye anamiliki duka la Teacher trading la Kijangwani huku akisema kwamba mchele huo unaendelea kushikiliwa na bodi ya chakula ukiwa ghalani hapo.

Kutokana na hali hio Dk Simai aliwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa ya kununua bidhaa hasa kipindi hichi ambapo wafanyabiashara wengi hutumia fursa ya kuuza kwa bei nafuu bidhaa zilizoharibika.

“Baadhi yao huchukua biashaa mbovu zilizoharibika na kuzihamisha katika mifuko mipya ili kuonyesha kwamba bidhaa hizo ni mpya na kuanza kuuza kwa za seli huo ndio utaratibu unaotumika hivi sasa naona” Alisema Daktari huyo ambaye amekuwa akiendesha msako.

Aidha amewataka wananchi kutoa ripoti katika bodi yake tukio lolote la kubaini kuuzwa bidhaa wanaozitilia shaka ili kuokoa afya za watu na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Bodi hiyo hivi karibuni ilikamata na kurejesha Australia Kontena moja la pombe iliyopita miaka 6 muda wa matumizi, tani 28 za sukari iliyorudishwa Mombasa Kenya na kuangamiza tani moja ya tende iliyoharibika

Tatizo la uingizaji wa vyakula na dawa zisizokuwa na viwango linaithiri sana nchi maskini kutokana na kukabiliwa na changamoto mbali mbali hasa kutegemea kwa kiasi kikubwa uigizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.

Changamoto nyengine ni kuwepo idadi kubwa ya bandari bubu,rushwa kwa watendaji wanaowajibika kudhibiti bidhaa hizo, ukosefu wa vitendea kazi na umakini ambapo wananchi wengi hujali zaidi urahisi wa bihaa kuliko ubora wa bidhaa zenyewe ambazo hutumika katika maeneo mbali mbali ya mijini na vijijini.

7 Comments on "Wazanzibari kula vyakula vibovu!"

  1. Royal Zenj 06/09/2010 kwa 8:48 um ·

    Hongera Dr. Simai kwa kazi nzuri endelea hivi ndivyo inavyotakiwa usijali wafanyabiashara wasio waaminifu hao , na kama inawezekana wanyan’ganjwe leseni nadhani hilo litakua funzu zuri kwa wengine .

  2. chachandu 06/09/2010 kwa 10:08 um ·

    oh kwani ni akina nani hao wanaoagiza hivyo vyakula?huu ni mtaji mzuri kwa waagiziaji ambao ni sawa na waagingizaji wa madawa ya kulevya.naona mkono wa wakubwa upo.

  3. jamaleyl 07/09/2010 kwa 12:09 mu ·

    Hao wanaofanya matendo hayo ya kuleta vyakula vibovu na dawa zilokosa viwango wamekosa ubinadamu kwa tamaa zao za kidunia.Sasa ikiwa wao hawajali afya za binaadamu wenzao kwanini wao wawe wanahurumiwa kiasi hiki.Nadhani umefika wakati serikali ipitishe sheria kali za kuwafilisi pamoja na kifungo,badala ya kuwataka kulipa gharama za kuharibu hizo bidhaa zao.Lazima tufahamu kuwa hao walokamatwa ni sehemu ya wafanyabiashara wanaofanya biashara hiyo haramu.Sasa tujiulize wangapi ambao washapitisha bidhaa kama hizo ama kwa kutumia rushwa au kutumia migongo ya viongozi wa serikali.Athari za bidhaa hizo katika jamii yetu ni kubwa lakini kwasasa ni vigumu kuijua kwa kuwa hakuna tafiti ambazo zimefanyika katika kuangalia athari ya vyakula vibovu na dawa zilokosa viwango

  4. WANYUMBANI ZANZIBAR 07/09/2010 kwa 9:15 mu ·

    SMZ kuweni makini na Wafanyabiashara wasio waaminifu ni wakati sasa kuwaadhibu wote wanaoingiza vyakula bila kujali afya za watumiaji.

    Bodi ya vyakula, dawa na vipodozi iimarishwe zaidi kwa kujengewa uwezo kisheria wa kuwaadhibu wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuwafungia lesini zao na kuwash-taki iwapo watakiuka maadili ya kibiashara.

    Hongera sana DKT Burhan Othman Simai, M/mungu atakulipa ujira mwema na kukupa maisha marefu yenye kheri na wewe

  5. mtu kwao hasahau 07/09/2010 kwa 9:57 mu ·

    hongera dk Simai’ ila tahadhari na nchi zetu hizi unapotenda majukumu yako kwa kufuata taaluma yako kama hivyo waliokuzunguka hukuchimbiya shimo lakini aso mtu ana mungu.

  6. Utomvu 07/09/2010 kwa 1:20 um ·

    Mimi nashangazwa sana nahawa wafanya biashara,
    tusemi hii nitamaaa au ndo wametumwa kutumaliza wazanzibari
    na kiukweli haswa imeshakua tabia yao yakututia sumu mwilini
    doooo mungu walinde wanzibari nanchi yawazanzbari nauwaangamize mahasid namadhali wanafsi, hongera DK Simai,
    kaza buti mungu sw atakusaidia amini.

  7. Annur 07/09/2010 kwa 8:40 um ·

    Ninavyo elewa mimi nchi nyingi zinakuwa zinadhiti uingizaji wa vyakula kwa kuweka mwabwana afya katika sehemu zote za kuingiza bidhaa nchini. Serikali huweka utaratibu wake.
    A.Bidhaa za vyakula hufanyiwa taftish na mabwana afya kwa ajili ya usahihi wake nakutoa shahada kabla hazijaingia kwa walaji. Hii kwa bidhaa mpya.
    B.Maofisa wa afya ya manisipaa ya mji hufanya taftishi zake kwenye maduka ya reja reja kuangalia kuwa sheria ya usafia inatimizwa na vya kula vanavyouzwa havijapitiwa na wakati wake kwa bidhaa kongwe
    C.Kila mara hufnyiwa vile vile taftishi ghala zote za vyakula kwa usafi na zisije zikawa na bidhaa kongwe zilizo kwisaha muda wake wa kutumiwa.
    Sasa ukiangalia hapo juu kwenye maelezo, inaonyesha ni bidhaa mpya zinazo zungumziwa kwa ajili ya matumizi ya mwezi Ramadhani si bidhaa kongwe zilizo lala kweye maghala. Sasa makosa hasa yako wapi kwa wafanya biashara au kwa maofisa husika wa afya? Jambo la kusitisha ni kuwa mwezi mzima Ramadhani watu walikuwa wanalishwa vyakuala vivlvyo kwisha muda mpaka mabwana afya wame kuja kufichua hivi karibuni. Tujue wafanya biashara wa vyakula popote ulimwenguni huwa wanatafuta mwanya wa kufanya uaharibifu kama huu, si Zanzibar tu, hivo serikali ni lazima
    iwe macho kudhibiti uingizaji wa vyakula ..
    Soma hapa chini uangalie hata Carrefour hawaaminiki.

    “Abu Dhabi Food Control Authority (ADFCA) has shut down the meat sections of two major retail chains for selling expired meat products, a statement said on Monday….

    The meat stalls at Lulu Hypermarket in Al Wahda Mall and Carrefour in Marina Mall were also closed down for three days during the past two months for allegedly selling expired meat and other violations, according to the statement.” – Gulfnews.com, 03 August 2009
    http://www.arabianbusiness.com/591311-dubai-firm-sold-food-not-fit-for-human-consumption

Comments are now closed for this article.