HabariMatangazo

KONGAMANO KUBWA LA MKATABA BWAWANI – TAREHE 25/05/2013

TANGAZO!

Haya haya wazanzibari! Kumekucha! La mgambo likilia kuna jambo! Kamati ya Maridhiano inawatangazia wapenzi wazanzibari wote, kike kwa kiume, wapenda nchi yao kwa jumla kuhudhuria kwa wingi katika kongamano kubwa la aina yake litakalofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25/05/2013 hapo katika ukumbi wa Salama hall, Bwawani.

Agenda kuu ni Zanzibar kurejesha Mamlaka yake kamili kupitia mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Hatumwi mtoto! Shime wazanzibari wote kuhudhuria kwa wingi bila ya kukosa!

TUNATAKA NCHI YETU SASA TUMECHOKA TAFRANI!
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA!!

Tagsslider
Share: