Habari

MAALIM NA USALITI KWA UAMSHO

Kwanza assalamu alaykum wanamzalendo!Ama baada ya salamu kwa wingi wa majonzi na huzuni nawasilisha lawama zangu kwa Makamu wa kwanza wa Raisi Mh Maalim Seif Sharifu Hamad!

Wengi mtashangaa kwa nini nimlaumu maalim kwa kuwasaliti masheikh na maimamu wetu wapendwa kuwataja wachache Sheikh Farid na Sheikh Mselem.

Namlaumu maalim kwa sababu anauwezo wa kuwatoa kwenye madhila haya yanayowasibu,vilevile anao uwezo wa kukemea waliopo chini yake juu ya huu udhalimu wanaofanyiwa masheikh wetu,hasa ukitilia maanani mahakama ipo chini ya Waziri wa CUF.Lakini maalim kimya kabisa yaani haumii wala haoni uchungu!

Masheikh walikuwa watetezi wakubwa wa maalim mtake msitake,vilevile walikuwa wana msimamo mmoja na CUF wa kuwa na Zanzibar huru!Kuwafunga ni kuwapunguzia nguvu wapigania uhuru wa Zanzibar!Tumeona bara Lipumba akikemea Kukamatwa hovyo kwa Masheikh lakini huku Zanzibar CUF na Maalim wote wapo kimya,au kwa sababu na yeye ni sehemu ya serikali?Kwa hiyo na yeye ni sehemu ya uovu,anaogopa kuisema serikali atakuwa anajisema mwenyewe.

Nimalizie kwa kumuomba maalim seif aingilie kati masheikh wetu waachiwe mabona Karume alisema waziwazi bila woga?Yeye anaogopa nini?au anaogopa Shein atamtimua?Haya ni madaraka ya kidunia tu,hayana maslahi yeyote kwetu,Maalim baba funguka!HAKI SAWA KWA WOTE………………………………………………………………………..

Tagsmakala
Share: