Habari

Magufuli acha maneno, fanya vitendo: naona huwezi kukata umeme Zanzibar

Taarifa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuitaka Tanesco kuikatia umeme Zanzibar zimeenea katika vyombo kadhaa vya habari. Magazeti, mitandao ya kijamii vimemkariri Magufuli akitoa amri hiyo mbele ya hadhara.

Wengi wa wananchi wanaona kwamba Magufuli hana maskhara katika kauli zake. Naweza kuwa peke yangu mwenye mawazo tofauti wa hayo.

Nilichokiaona nikuwa Magufuli hawezi na huthubutu kuikatia umeme Zanzibar kwa madai ya kudaiwa. Labda alikuwa akistarehesha barza au kutaka watu wacheke.

Licha ya kufanya baadhi ya kutumbua majipu, bado Magufuli hana ubavu wala mamlaka ya kuinyima umeme.

Kwanza ununuzi wa umeme ni mkataba wa kibiashara baina ya nchi mbili, Zanzibar (mnunuzi) na Tanganyika (mchuuzi). Hivyo lazima kuwe na heshma kwenye makubaliano baina yao.

Pili Zanzibar, imeanza kuwa na umeme kabla ya Tanganyika. Hivyo njia walizopitia hadi kumiliki zinajuilikana kiasi kwamba kwa kitisho cha kukatiwa hakiwezi kufuadafu.

Licha ya unyonge wake, Zanzibar inaouwezo na mbinu za kujitoshelesha kupata nishati mbadala.

Magufuli kama kweli asemalo ndio afanyalo tusubiri kesho tuone umeme umekatwa. Vyenginevyo wananchi wataamini na nitazidi kuamini kuwa ni yayo kwa yayo, maji ya futi na nyayo.

Langu jicho, Ngosha nasubiri ushahidi kamili

Share: