MALIM SEIF KWELI AKISHINDA ATAPEWA SERIKALI ?

Written by  //  25/08/2010  //  Habari  //  25 Comments

naomba wachangiaji wenzangu tulichangie swala hili . unajua kinachofanyika katika uchaguzi wa zanzibar ni hatua ya mwisho yani watu washapiga kura wanasubiri matokeo wakati wa matokeao ndio yanajitokeza mambo ya kiajabu ajabu unaweza ukenda tume ukakuta kufuli imefungwa yani hamna mtu mwenyekiti wa tume hajulikani alipo unakuja kusikia tu matangazo ya kiajabu yashatolewa . hebu naomba fikra zenu nyiyi wenzangu

25 Comments on "MALIM SEIF KWELI AKISHINDA ATAPEWA SERIKALI ?"

  1. Bosco 25/08/2010 kwa 1:48 um ·

    Mimi naona hayo mara hii hayatatokea na inshallah maalim seif atakua rais wa znz mara hii.

    Lkn tume wajue kua mara hii wakitufanyia mchezo basi wakwanza kuwashughulikia ni viongozi wa zec. Kwani huu upuuzi wa tume kuharibu matokeo halafu wao wakaendelea kudunda mitaani ndio unaowapa kiburi kuendelea kuharibu lkn kama mkuu wa tume japo mmoja ameuliwa heshima ingepatikana japo kidogo. Basi tusubiri mara hii tuwaone kama wataendelea kudunda wakishavuruga.

    Ni imani yangu kua mara hii mambo yatakwenda vizuri ili tujenge znz.

    ZANZIBAR DAIMA

  2. jazz 25/08/2010 kwa 3:23 um ·

    Cuf haiwezi kushinda mapaka Seif aachie ngazi

    Waunguja wanamkumbuka Seif alivyoleta siasa ya kibaguzi baina ya wapenba na waunguja
    alipokuwa waziri kiongozi Seif alifanya mambo mengi ya ajabu, alidhubutu kuwapa mikopo wapemba tu waunguja walionkea patupu

    Alipokuwa waziri wa elimu scholarship zote zilikuwa wanapewa wapemba…nk

    God bless Zanzibar

  3. Kamshuu 25/08/2010 kwa 4:38 um ·

    jazz.

    Kama huna lakusema nyamaza,kuwa msomaji ya wale watu wanayoyaandika

    utapata faida kubwa na kukuwa kwa maarifa yako,kuliko kuandika maneno

    uliokuwa huyafahamu.

    Sitaki kwenda huko unakokwenda wewe,kwa mawazo yangu wewe ni MSHABIKI unafuata ……….

    KAMSHUU.

  4. Mandi 25/08/2010 kwa 4:41 um ·

    @Jazz.ningependa kukuomba samahani kwanza.awali ya yote ninahitaji kujua unaumri wa miaka mingapi?na umefka darasa la ngapi la msingi?nimekuuliza maswali hayo mawili kwsabbu mwenye akili zake timamu na elimu yakuchambua mambo hasubutu kutamka utofauti wa uunguja na upemba.siwezi kukatalia unachokisema bali ningeomba unijulishe swali hili.nikwamuda gani maalim seif amewahi kuwa waziri ya elimu?halafu umeongelea kuhusu wapemba kupewa scholarshp ni wapemba wangapi walowahi kupewa hizo nafasi?nasubutu kusema hayo ni maneno ya kulishwa sijui nani aliyekulisha.nahisi kwamba wewe ni mmoja ulompinga rais kwkupiga kura ya maoni hapana.wazalendo wenzangu tumemkamata huyu ni mmoja alokataa kura ya maoni.m.mungu tuepushe na watu hawa kwa kujarbu kuchafua upendo wetu.mungu ibariki zanzbar na watu wake na kila aliye na sera za kibguzi mdidimize asiweze kusimama amin

  5. mnyonge 25/08/2010 kwa 4:53 um ·

    Msijidanganye hakuna chama cha siasa chochote hapo Tanzania kitakachoshinda kikapewa Serikali sahauni kabisa Seif Ashinde mara ngapi tena ? CCM Kama ndio ilioshika mpini tume yao idara za ulizi na usalama wanamiliki wao serikali wanayo wao Bado mnategemea Seif kupiwa Serikali tu mara hii atashinda tena lakini hapewi wembe ndio ule ule unaoitwa TOPAZ Unageuzwa upande wa pili tu umnyowe tena,
    Hawakumpa CCM Mwenzao Dr Mohammed Khariib Bilal wakampa mtu kutoka upinzani, Jamani tupo M/Mungu atuweke hai na uzima tuje tuyaone lakini kwa tamaa ya Chama cha cuf au chochote cha upinzani kupewa Serikali na CCM Kukubali kushindwa hiyo Never kwa Siasa za kiafrica hakuna Democracy

  6. mumewetu 25/08/2010 kwa 4:58 um ·

    @ jazz
    mtu akikaa kimya hakuna atakaemlaumu kwa ukimya wake, bali anaweza kuulizwa tu “mbona KIMYA?”

    Hizi siasa za kibaguzi zimeshapitwa na wakati lakini inaonekana wewe jazz bado ziko kwenye damu yako. Nakuomba ufanye utafiti, tafuta na watu wanaujua mambo ya Zanzibar ili wakueleze nani aloleta siasa za kibaguzi kwa Wapemba na Waunguja, sio uje na jazba tu.

    Kwani kazuiwa mtu yeyote wa CUF wa Unguja kugombea Urais? kwanini wewe hukugombea au umetokea KISONGE?

    Kama huna cha maana chenye kuleta umoja na maendeleo kwa Wazanzibar, basi ukalie mkia wako.

    MUNGU IBARIKI ZANZIBAR, AMIN

  7. Ghalib 25/08/2010 kwa 5:51 um ·

    A.alikum
    Mimi ndugu zangu naweza kusema kuwa kushika kwa cuf madaraka ni vigumu,kivipi ? kutokana na mfumo ambao unatumika katika smz,na tume ya uchaguzi ZEC,ipo haja ya kufanya utafiti mapema kabla ya uchaguiz huu mwisho,ili kufanyike uchaguzi wa huru na haki.

    Japokuwa kumefanyika kura ya maoni naimeonyesha sura nziri ya znz napia rais kusisitiza kuwepo kwa amani na chaguzi huru,lakini naweza sema ipo haja ya sisi wananchi kukifanya kuonyesha kuwa upo msisitizo zaidi kwa rais kuchukua hatua ya haraka kwa tume ya uchaguzi.

    Ningeshauri wazanzibar wote sasa hivi kufanya maandamano juu ya kumsisitiza rais karume abadilishe mfumo wa zec kabla ya uchaguzi mkuu,au ahaidi wananchi wote wa znz kuwa atasimamia uchaguzi mkuu na utakuwa huru kama alivyosimamia kura ya maoni. Tusijiboteke tu tukasema kuwa tutashinda au uchaguzi utakuwa huru,ukimya wa sasa ni moto wa makumbi,uchaguzi mkuu ndio utakapouwona moto huo baada ya kutaja matokeo,tuamke.

    Nawatakia ramadhan nyema amin

  8. chachandu 25/08/2010 kwa 6:56 um ·

    hili suala ni gumu kivyake. kwanza kutokana na :muafaka” serikali haitakua ya chama kimoja bali ni umoja wa kitaifa ingawa sijuwi maana yake halisi.kutokana na hilo ni kwamba serikali ijayo sefu ashinde asishinde atakuwemo katika hao viongozi wa juu katika serikali,
    suala la wachangiaji wengine kuhusu ubaguzi wa kipemba na unguja hili nalo nionavyo mimi liko kwa kila upande kwa hiyo labda maridhiano yakikamilika huenda nalo likaondoka.ukweli ni kwamba katika miaka yote ya mapinduzi hapajakua na rais toka pemba na mwaka huu ndio tutapata viongozi wote wakuu toka pemba jambomambalo ni faraja kubwa kwa wapemba wote ,lakini pia ni kujiuliza wakati ule viongozi watendaji wote wakiwa wanatoka unguja jee wapemba walikua wakijihisi vipi?tukipata jibu la suala hili basi nafikiria mambo yatajua yamejieleza wenyewe kwani kama waislam wanavyosoma katika kitabu chao. tilka L ayyam nudawiluha baina nas. hakuna tendo jipya bali ni mzunguuko tu leo kwako na kesho kwa mwenzako,vitimbwi walivyofanya au kufanyiwa mtu leo kesho vitamzunguukia mwenyewe.tumuombe mola awape moyo wa ustahamilivu viongozi watarajiwa seif na shein na kama kutatokea vitimbwi vyovyote vile toka kwa wahafidhina wa kiunguja basi wachukulie kama ni utani wa kimila kati ya visiwa vyetu hivi kwani katika tawala zilopita ambazo zilikua zikiongozwa na waunguja nako pia kulitokea vitimbwi toka upande mwengine wa visiwa vyetu.

  9. cali 25/08/2010 kwa 7:32 um ·

    salam aleikum

    mm nazani kwa kweli maalim ni mtu wa kuzulumiwa tu na sizani kua atapewa

    na fikra zangu atazulumiwa mpaka kiama

  10. ahmed mohd 25/08/2010 kwa 7:56 um ·

    assalam alykum. safar hii kama hapewa ndo hapewi tena huoo urais mwaka wake huu seif.

  11. mtu kwao hasahau 25/08/2010 kwa 10:00 um ·

    binafsi naamini seif atashinda lakini kupewa serikali ni kitu kingine na pia tusisahau uso umembwa na haya na hii ndio yaweza wasukuma wale waliozoweya dhulumu wakashindwa fanya hilo tena kwa kuona haya na hata masalan tuchukuwe hakupewa au kashindwa basi na pia si mwanzo mbaya ukilinganisha natulikotoka kwani katiba tayari imeshaonesha hata asipopewa MAALIM atakuwa ni mmoja kati viongozi wa juu [MAKAMU WA RAIS] wa nchi na hilo ni faraja kwa wazanzibar kwa angalau ule mwanga japo kidogo wamaendeleo umesogea mbele au upo pale ambapo hatukutegemea kuwepo, na pia tusiwe wenye kutawaliwa na woga katika mambo anayoyaendesha ALLAH kwani hili linaonesha wazi kwamba lina nguvu ya ALLAH zaidi kuliko binaadam, nasema hivi kwa maana kila mzanzibar hawezi elezea ni jinsi gani ghafla hii tupo hapa? na ukijiuliza hili wazi utapata jibu kwamba hii ni ilham kutoka kwa ALLAH [S.W.T]…

  12. Mtu-wakale 26/08/2010 kwa 1:03 mu ·

    Mandi amemuliza Jazz, maswali mawili mazuri sana.

    Pamoja na maswali hayo namuomba Jazz, apunguze chuki dhidi ya maalim Seif, sababu chuki hazijengi. Kweli kila binaadamu anaupungufu wake. Mkamilifu ni Allah, peke yake.

    Jazz, nakupa jina la mtu tena maarufu sana ili umulize kwenda kusoma nchi za nje sababu ni nani.

    Said bakari Jecha, kama unamjuwa muuliza ilikuwaje akenda Uingereza kusoma, sababu hasa ni nani.

    Wakati Maalim Seif, alipokuwa waziri kiongozi Said Bakar Jecha, alikuwa waziri katika ofisi ya waziri kiongozi. Maalim Seif, alimshauri akamwambia kuwa bora aache uwaziri asome. Hapa Maalim Seif, alizingatia kuwa cheo kinaondoka lakini, elimu ikishakaa kichwani hakuna wa kuiondosha.
    jazz, kama unasema Maalim Seif ni mbaguzi, nakupa baadhi ya watu waliyoletwa katika madaraka na yeye maalim Seif, wakati akiwa waziri kingozi.

    Mhe. Mohamed Mzale Mhe. Mohamed Hijja (usalama wa taifa) Mhe. Omar Ramadhani Mapuri, Mhe. Juma Duni na wengine ni Marehemu akina Fessal Mbamba na wengi wengine ambao hao wote hawakuhusu Pemba, ndewe wala shikio.

    Jazz, zaidi nakupa mji, fanya utafiti zaidi kwa hayo yako na haya yangu sio unasukumwa na chuki na dhana. Usitumie dhana na chuki kuhukumu, fanya utafiti kwanza ndio uhukumu.

    Kuongezea hapo kwa upande wa maendeleo, maduka na biashara za aina zote pamoja na usafiri wa daladala kwa miji yote Unguja na Pemba chanzo ni Maalim Seif, ndie aliyekuwa mpiga debe mkubwa kwa Wazanzibari, kuwahimiza kuanzisha biashara.

    Jazz, nasikitika sina time sana leo, kesho kazini mapema, Maalim Seif, ndio chanzo cha Gulf Air, kutua Unguja. Na hii ilisabaishwa na vitu viwili.

    Kwanza Shirika la ndege la Tanzania (ATC) lilikuwa safari zake hata za ndani zilikuwa hazina dhamana (haziaminiki) ” any time cancel” na kwa upande wa Zanzibar, hali hiyo ilizidi. Maudhi yakawa yemezidi, Wazanzibari wakaitaka Serikali kuingilia kati.

    Hilo moja, lakini lapili ambalo nalo lilikuwa ni aibu na halivumiliki, ni pale abiria wa Zanzibar, wanapokuja kutoka nje na kushukia Dar Es Salaam, wakifika Dar Airport, mizigo yao inafunguliwa vitu vyao vinaibiwa na jeuri zaidi wanatiliwa mawe katika masanduku yao.

    Maalim alifanya mkutano Hotel ya Bwawani na wafanyakazi wa ATC wakiwamo viongozi wa ngazi za juu wa ATC. Mimi nafsi yangu nilikuwapo nilishuhudia.

    Maalim Seif, aliwataka wafanyakazi wa ATC, kurekebisha hali hiyo haraka lakini pia aliwambia kuwa wameanza kuzungumza na Gulf Air na kuahidi kuratibu safari zake kwa nchi za Ghuba na Dar es Salaam kupitia Zanzibar. Hicho ndio kilikuwa chanzo cha Gulf Air kuja zanzibar, sababu ni Maalim Seif.

    Jazz, nakuuliza mtu mbaguzi anafanya hayo? Nakuuliza Pemba na Unguja wapi hasa kuna maendeleo? Jazz, Karume (Dr.Aman Karume) alisema hadharani kuwa hakuwachaguwa mawaziri kutoka Pemba kwa sababu Wa-Pemba, hawakumchagua. Pima hiyo kauli ya kiongozi wa nchi.

    Kwa kauli ile ya Karume, ingekuwa baraza la wawakilishi ni(strong) makini na mahakama zetu zinauwezo zinajiendesha na kujitegemea kisheria basi, lazima Karume engepanda mahakamani tayari, alikuwa na kosa la ubaguzi. Kosa la jinai.

    Marehmu Maalim Idris, haifai kumsema yuko mbele ya haki, lakini alikuwa hatari. Iko siku naweza kusema ikibidi. Dk. Salmini, yeye funika kombe.. maana hata makaburu south Africa, basi baadhi ya mambo ya kibaguzi aliwashinda. Iko siku ya kumzungumzia jinsi alivyoendesha utawala wake kibaguzi.

    Jazz, Maalim Seif, ni mbaguzi au unamuonea tu, nakuuliza tena?..

  13. seif 26/08/2010 kwa 4:01 um ·

    As,alaikum wasomaji wa mzalendo, mimi naamini kwamba maalim mwaka huu ni mwaka wake wa kua raia wa Zanzibar.Kwa wale ambao wanasema hatapewa serekali mwaka haiwezekani, nasema hivi kwa kujiamini kabisa.Hata wazee wa kisonge wanasema kwamba bora mwaka huu apewe huyo seif ili tumuangalia atafanya nini sababu wanajua kwamba yeye ndie atakae kua rais.Kwa hivyo wewe Jazz ukileta tofauti zako ni bure kubwa jamii itakuangalia tofauti. Mungu ibariki Zanzibar na watu wake, amin.

  14. hokani 27/08/2010 kwa 1:59 mu ·

    KWA MAZINGIRA YALIYOPO HAPEWI SERIKALI.
    HAYAPENDEZI MASIKIONI LAKINI NDIYO HALI HALISI.

  15. jazz 30/08/2010 kwa 11:16 um ·

    Jamani mbona mnashindwa kufahamu kuwa Seif Sharif Hamadi ni mwanasiasa kwa upande wangu wanasiasa wato waongo..

    Napenda kuuliza kwani Seif Sharifu alikuwa wapi Zanzibar ilipokuwa ikizama,Je yeye alikuwa hayaoni yaliyokuwa yanaendelea wakati yumu kwanye siasa ya zanzibar kwanini alinyamaza kimya?

    Mtu-wakale,
    History inaonyesha kuwa Seif Sharifu Hamadi sio mbaguzi bali ni mbinafsi kama walivyo wengi wapemba kwa hali hiyo sio mtu mzuri kuwa raisi wa nchi kama Zanzibar ambayo watu wake wamechanganyika kila kabila

  16. Mandi 31/08/2010 kwa 6:42 mu ·

    @jazz unapoongea lazima uwe na ushahidi umesema kua seif si mbaguzi bali ni mbinafsi kama wapemba walivyo tunachoshangaa hukutoa ushahdi wa jambo hilo.kw mfano mm naweza kusema kua leo ww hukufunga,lap2 wapemba ktk serikali zilopta ilikua hawaajiriwi nk.ninaweza kupata madhambi kwani sina ushahdi wa hayo kwa iyo unaloongea kua makini sana huongei na watu wa maskani hapa bali niwasomi.takecare

  17. ashakh 31/08/2010 kwa 10:01 mu ·

    Simtetei Maalim Seif, atajitetea mwenyewe. Kwani mja kunena, Muungwana ni vitendo.

    Lakini Jazz, naomba uangalie maana ya “ubinafsi” kwenye kamusi. Ila ninavyofahamu Maalim Seif sifa hiyo kwake sijaiyona. Kwa sababu mpaka leo sijamuona kuishi kwenye kasri alilojenga, zaidi ya nyumba ya shirika la umeme. Hivyo tunasema hakujilimbikizia mali. Hizi mali ndio chanzo cha ubinafsi.

    Pili, katika awamu zake zote za uwongozi, ukichungulia muundo (hata huko kwenye makundi) basi inakuwa wa umoja wa kitaifa. Hebu uliza hilo kundi la FRONT LINE ni kina nani walio kuwemo. Bila ya shaka ni WAUNGUJA na WAPEMBA.

    Tatu, hata kwenye CUF alikuwa na uwezo wa kuwa mwenyekiti, lakini kwanini kashikilia kwenye ukatibu mkuu tu. Sababu hizo za ubinafsi zinatokea wapi.

    Jazz siku zote nasema siasa huanzia nyumbani. Ikiwa wanasiasa wote ni waongo basi na wewe ni muongo vilevile. Naithamini sana kazi ya siasa kwani ndio inayopanga mustakbal wa maisha yangu.

    Jazz unasema kama walivyo wapemba wengi kuwa wabaguzi. Siwezi nikakataa, pia siwezi nikakubali. Kwani ndugu zetu wengi wa Unguja wanapokwenda Pemba kufanya kazi, haondoki ikiwa hana koo nyongani. Pia hao Wapemba wanapokuja Unguja kuuza dagaa, hawaondoki ikiwa hawajapakwa liwa.

    Sijuwi vizuri sana, lakini kwa mtazamo wangu nimeishi na watu wa pande hizi mbili miaka nenda rudi, tunashirikiana, tunapendana,tunatembeleana, tunasaidiana, kwa hali na mali.

    Point itabaki jee mazingira yaliyopo hivi sasa Maalim Seif atapewa urais pindi akishinda. Naomba pia ifahamike, ni lazima ashinde ndio apewe, sio isomeke vyenginevyo.

  18. sale 31/08/2010 kwa 10:10 mu ·

    Ndugu zangu
    Kama akishinda na asipewe serikali, inakuwa shida si kwa sefu bali kwa wale waliomtilia kura, itakuwa wamenyimwa haki yao, swali je wewe uliemchaguwa huyo kiongozi Seif na asipewe serikali utafanya nini? au ndio yale ya maoni ya watu hapa hapa kwenye mtandao walisema kuna mambo mtu huyapendi lakini huna budi ukubaliane nayo? si mtaji mtu huyu kwani namuheshimu na inawezekana labda alikosea,,

  19. sale 31/08/2010 kwa 10:17 mu ·

    @Jazz inaonyesha si muda mrefu tangu uhamie Zanzibar,unaposema>Napenda kuuliza kwani Seif Sharifu alikuwa wapi Zanzibar ilipokuwa ikizama,Je yeye alikuwa hayaoni yaliyokuwa yanaendelea wakati yumu kwanye siasa ya zanzibar kwanini alinyamaza kimya?….Jazz hujui kwamba Seifu alifukuzwa kwenye ccm kwa sababu aligundua njama zao na ccm kugundua njama zake? swali zanzibar ilikuwa inazama waulize kina Jumbe, Salmin Amour, na washabiki wake kama wewe,,,

  20. kassim 31/08/2010 kwa 2:33 um ·

    -Mimi nasimama na wale wote waliombea dua ya kheri nchi yetu ya Zanzibarkwa dua na sala kem kem. Kile kisimamo cha Maisara, kilikuwa si cha kawaida. Dalili ya mvua ni mawingu.

    -Mwaka huu Alhamudllah, mpaka sasa hivi sijasikia mtu kuwekwa ndani, sijasikia wale vijana wa janjaweed, ile melody piga piga Pemba nayo naona mazumari yake sijayasikia, ubakaji wa dada zetu nao mara hii haupo. Nakuna mengi mabaya ambayo siku za nyuma yalikuwa yakitendeka ikifika wakati kama huu, lakini mara hii hayajatendeka. Kwa hili tushukuruni na tuzidi komba dua.

    -Haya mambo ya kuchochea watu na kuleta migawanyiko ya ubaguzi ndio yaliyo ikwamisha Zanzibar kwa siku nyingi. Nakubaliana na walio mjibu ndugu Jazz, lakini mimi nahisi tusimpe mwanya kuyaendeleza haya. Lengo la maridhiano ni kufuta hizi chuki za kijinga jinga kwa mtu binafsi, tabaka fulani, dini fulani nk nk.

    -Tumo kwenye kumi la mwisho, na likimaliza hili, ndio Rmadhani imekusha. Ni matarajio yetu kuwa tutakuwa ni wenye kufuzu amali zetu tulizo tenda ndani ya Mwezi huu mtukufu; kwa maana ya kuwa tuko wasafi kwa kiasi gani. Tuna miezi kamili kuingia kwenye uchaguzi. Yote tisa, kumi tuombe dua, uchaguzi uende salama, aliyeshinda na apewe, na zaidi ya yote MwenyeziMungu ajaaliye Serikali yetu tarajiwa ya umoja w akitaifa isimame na ifikiyemalengo yake.

    -Kwa wale ndugi zetu walio jenga bongo zao, wenyema-degree yao ya kila fani, huu ndio wakati wa kwenda nyumbani kujenga nchi, akina Mzee ramsi, mrfroasty, mzenji na wengine wengu.

    Maasalama

  21. jazz 08/09/2010 kwa 6:19 um ·

    @sale sijui unazungumza nini, Nashangaa kuwa hujui kama Seif ndie aliyemfanya Jumbe afukuzwe kwenye madaraka.

    Baada ya Jumbe kushtukia ujanja wa Watanganyika aliwaita lawyers kutoka Nigeria ili Zanzibar ijitoe kwenye muungano wa serikali moja.

    je unajua Seif Sharif Hamadi alifanya nini?

    Alimchonge Aboud Jumbe Mwinyi kwa Nyerere hiyo ndio Sababu ya Jumbe kufukuzwa kazi

    Kama Seif ana uchungu wa Zanzibar kwanini akafanya hivyo.

    Kwa upande wangu Seif ni mcgu wa madaraka na ndio maana kila siku anagmbea nafasi ya urais wa Zanzibar

    Je unataka kuniambia kuwa hakua mwangine anaefaa kuwa mgombea urais wa Zanzibar kupitia nafasi CUF??

  22. mrfroasty 08/09/2010 kwa 9:34 um ·

    Nimefuatilia mjadala huu kwa makini kidogo na kutizama wachangiaji na maoni wanayotoa.Roughly, nimeseme ukweli mimi si mwanasiasa ila ni mtu mmoja ambae natizama vitu kwa kuweka kwenye mizani na kuchanganua kadiri ninavyoweza au uwezo niliopewa na Mola.

    Watoaji maoni au mtoa maada ni typical Zanzibari kama wengi watakavyo expect.M.Seif ni mwanasiasa na wazanzibari watakaomchagua au kumpigia kura wana haki ya kufanya hivyo.Kiilivyo, suala si kuwa atapewa bali umma utamueka kiongozi unaemtaka ?

    Kusema atapewa ni nadharia ya kivivu, woga na udhaifu.Ikiwa wazanzibari wameamua huyo ndie kiongozi mwenye maslahi nao, basi wasisite hapo wasimamie haki itendeke na wapate kiongozi wanaemtaka.Hili sio suala la kuomba na kupewa.

    Unaposema atapewa…mimi sifahamu atapewa na nani ? Tanganyika ? Wanamapinduzi ? Makomredi ?Tuache kuwa wavivu na dhaifu na badala yake tusimamie haki.

    @jazz
    Watu kama Jazz ni watu wa kupuuzwa tuu na si watu wa kujadiliwa.Nimesoma maoni sioni jipya ni yale kwa yale ambayo nishayasikia tokea kuzaliwa …Jumbe weee!Jumbeeee….Wapemba weee!…So what ?

    Kwanza nikufahamishe hapa MZALENDO tuko watu wa aina tofauti, huo upuuzi wako wa kibaguzi wa kipemba na kiunguja unavuka mipaka na unavunja tamaduni mijadala ya mtandao huu.Hapa MZALENDO tunajadili uzanzibari tuu, Seif tunamjadili kama mzanzibari.

    Suala la kuanza kumfikiria ni mpemba ni offtopic na halina tija.Tutakuwa ni watu tulioshiwa na hoja kama tutakuwa tunajadili ukabila saa zote.

    Tunachotakiwa kujadili ili jamii ifaidike ni kuonesha njia, kiongozi gani yuko katika nafasi nzuri ya kurekebisha matatizo ya Zanzibar.Matatizo ya Zanzibar yanajulikana na yako wazi kwa mwenye macho na mwenye kutaka kuona.

    1.Matatizo ya kichumi, tunahitaji uchumi ulio huru na unaomilikiwa na SMZ katika sekta takriban zote
    2.Matatizo ya ushirikiano wa kimataifa.
    3.Matatizo ya kisheria na katiba

    Haya yote kama sikosei yanarudi kuwa Zanzibar tunahitaji mtu alieko nje ya CCM ili ajadili bila kuoneana haya.Shein ametokea CCM….he is the green devil!.Hio nafasi ya kugombea urais amebebwa…who knows amepewa nafasi hio kwa niaba gani –>Mafuta ? –>Serekali moja ?

  23. hilal 18/09/2010 kwa 5:15 mu ·

    kumebakia mwezi mmoja tuu tuangalie nani atakua mshindi ila ninalofaham wazanzibari wanataka mabadiliko katika nchi yaoo ili wapate kuishi maisha mazuri

  24. khalef 18/09/2010 kwa 2:51 um ·

    @JAZZ
    kua uyaone..!!!!????

  25. hilal 20/09/2010 kwa 4:51 mu ·

    NDUGU KASSIM SHUKRAN SANA KWA MAELEZO YAKO MAZURI AMBAYO YANAFAHAMIKA MAELEZO KAMA HAYO AMBAYO HAYANA JAZBA KWA VIONGOZI WALA WANANCHI MUNGU AKUBARK

Comments are now closed for this article.