‘Marekebisho Katiba Zanzibar yana walakini’
Written by mwamba // 08/09/2010 // Habari // 4 Comments
Stella Nyemenohi
Habari Zaidi:
Chadema: Wananchi wataamua
Chenge ana kesi ya kujibu
‘Marekebisho Katiba Zanzibar yana walakini’
Wagombea ubunge Moshi kulindwa
Chadema yapuuza madai kuhusu Josephine
CUF, NLD wasoma upepo Bunda
Mgombea afagilia serikali kwa wilaya mpya
Ratiba ya mgombea wa CCM Kilimanjaro yatolewa
Kahangwa wa Chadema achomoa pingamizi
Pangani wajipanga kumlaki JK
Mgeni aliyechana noti adakwa
Mramba na wenzake kortini tena leo
Tunduru yajizatiti katika pembejeo
Tume yatatua migogoro 23,000 kazini
Tanesco wabaini kuibiwa kwenye mashine za Luku
Misitu Olmotonyi kupanuliwa
TFDA yachukua hadhari kuzuia mtama mbovu
Waathirika wa mafuriko Kilosa wapewa bati
Raia wa Kenya ashikiliwa kwa mauaji Tarime
Tendwa akataa pingamizi la Chadema
Habari zinazosomwa zaidi:
Balaa lingine kwa Chenge
Salama: Jasiri aliyetangaza kuishi na virusi vya Ukimwi
Dina Marius, mrithi wa Amina Chifupa
‘Housigeli’ anataka kuniharibia ndoa
Vatican yamvua jimbo Askofu
Kikwete achekecha wakuu wa wilaya
Waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano waongezeka kwa 22%
Interpol yatumika kusaka wenye zeutamu
Orijino Komedi, Jay Dee waitwa Iringa
JK apigilia msumari wa mwisho Dowans
MAREKEBISHO ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika hivi karibuni yametiliwa shaka na watu wa kada mbalimbali wakiwamo wasomi.
Imeelezwa kuwa marekebisho hayo yanapingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano na mkataba ulioanzisha Muungano na hivyo kuashiria hatari ya kusambaratika kwa nchi.
Wadau wa Katiba, sheria, masuala ya jamii na utawala bora na wasomi hususan kutoka Tanzania Bara, wameonesha hofu juu ya marekebisho hayo kupitia mkutano maalumu ulioitishwa jana Dar es Salaam na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).
Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. Sengondo Mvungi, ni miongoni mwa watu waliopinga wazi baadhi ya vifungu katika marekebisho hayo kwa kusema vina harufu ya kusambaratisha Taifa.
“Ina maana gani kusema Zanzibar ni nchi? Neno nchi maana yake ni ardhi? Mwaka 1964 Tanganyika na Zanzibar zote zilikuwa nchi, zikaingia mkataba wa Muungano, kwamba zitaungana katika Dola moja huru … hapo ndipo nasema mabadiliko yako nje ya Mkataba wa Muungano na Katiba.
Haya ni mabadiliko makubwa na hili ni jambo la hatari,” alisema Dk. Mvungi. Msomi huyo aliyebobea katika mambo ya sheria na Katiba, alisema Taifa linapaswa kutii Katiba yake.
Alisema marekebisho yalipaswa kufanyika kwa kushirikiana na Jamhuri ya Muungano, ili kuepusha Dola kukosa uwezo wake kama ilivyojitokeza katika baadhi ya nchi zikiwamo Somalia na Sudan.
Alionya, “sisi si miungu na wala si maalumu tusioweza kufikwa na hayo (kama ya Somalia). Tujihadhari.” Alisisitiza kwamba ilipaswa wahusishwe Bara ili waombe Bunge la Muungano lijadili mabadiliko hayo tofauti na kulipa nguvu Baraza la Wawakilishi kupitisha kwamba Zanzibar ni nchi.
Katika alichokielezea kuwa ni kulala usingizi kwa upande wa Bara, msomi huyo alisema ili kukubali yaishe, inabidi kubadilisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano iendane na mabadiliko hayo.
Hata hivyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Ali Uki aliyekuwa miongoni mwa watoa mada katika mkutano huo, alipinga akisema kilichofanyika si kuitambua Zanzibar kuwa Dola.
Vile vile alisema Katiba ya Zanzibar ina nguvu zake na haiwezi kuingiliwa katika mambo yasiyohusu Muungano.
“Huwezi kuilinganisha Temeke na Zanzibar yenye mabalozi wadogo, Mahakama Kuu … Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano,” alisema Uki ambaye aliungwa mkono na Makamu wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS) Ibrahim Bendera.
Bendera alifafanua, kwamba mabadiliko hayakuifanya Zanzibar kuwa Dola. Alisema Katiba ya mwaka 1984 iliyofanyiwa mabadiliko, iliandikwa kwa Kiingereza kwa kuitaja Zanzibar kuwa ni ‘state’ ikimaanisha nchi na kwamba kwa kuwa marekebisho ya sasa yameandikwa kwa Kiswahili, neno hilo limetafsiriwa kama nchi lakini haimaanishi kuwa ni Dola.
Alitoa angalizo juu ya Zanzibar kuwa na vikosi vya majeshi kwa kusema, “Katiba ya Muungano hairuhusu Zanzibar kuwa na vikosi. Sisi kama wanaharakati tunalipeleka wapi hili suala?”
Hata hivyo, wachangiaji wengine, akiwamo Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, walipinga utetezi huo kwamba marekebisho hayo hayana kasoro katika Katiba ya Muungano.
Walisema marekebisho yanadhihirisha kwamba hawataki kutawaliwa na ndiyo hatua ya kujichomoa katika Muungano.
“Wazanzibari hawakufanya makosa kurekebisha Katiba yao, kwani hakuna kifungu katika Katiba kinachosema ni kosa kujitoa kwenye Muungano. Huu ni uhuru wao. Suala lililopo ni kuzungumza juu ya Watanganyika, waachane kubebeshwa nchi nyingine,” alisema Mtikila.
Marekebisho hayo yaliyokwishatiwa saini na Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, ni matokeo ya kura ya maoni ya Julai 31 iliyozaa mabadiliko katika muundo wa serikali baada ya uchaguzi mkuu





4 Comments on "‘Marekebisho Katiba Zanzibar yana walakini’"
wewe sengondo mvungi sawasawa na jina lako linamamvumbi mengi.nyinyi watanganyika mnaitakia nini zanzibar?mmetushika.mara tumevunja katiba.sasa tuoneshe hio serikali yako ya tanganyika tulioungana na zanzibar.sasa kwaufupi maneno yamekuwa mengi tusubiri uchaguzi umalizike.tuitishe kura ya maoni zanzibar kama muungano tunautaka au vp?nyinyi mloweka serikali2 hamkuvunja katiba?mbona mmetushika ndugu zangu wa kizanzibar hii mijitu tusiisikilize inatutia uchungu kila leo wanatia hasira wanatuhujumu halafu pia na sheria wanatupangia bora tuvunjeni muungano au serikali 3 tuazeni sasa ikiwezekana tuoneshe kwenye uchaguzi wa mwaka huu.tena hao hawakuaazia huko kila sehemu wanajifanya wao wanaakili nyingi
jamami hawo wacheni waporoje sisi nimoto kwenda mbele, siwanasheria wala siwanashauri inshaala kwa uweza wa muumba zanzibar itafika lengo.
WALIE WAOO TU ZUWARDE AKILIA BUNDI HUAMBIWA USHURO? WALIPO KAA WATANGANYIKA WAKAVUNJA MKATABA MAMA(ATCLE OF UNION) NA KUIUWA TANGANYIKA YENU JEE MULIWASHAURI WAZANZIBAR AU MULIONA MUTUMIE UBAVU TU. MULIHISI MUPIDISHE UJAMBAZI WENU ILI KUWAPIKU WAZANZIBAR YAGUJU. MUUNGANO SIO KITU CHA NGUVU NI HIARI TU NA TUKITAKA TUNAUVUNJA WAKATI WOWOTE.
E , Bwana we koti likikutia joto hunabudi na kulivua .