Habari

Matofali yaanza kuadimika Zanzibar

Baadhi ya vituo vya upigaji matofali vimeanza kufunga biashara zao kutokana na ukosefu wa saruji zilizo na viwango, serikali imepiga marufuku saruji kutoka nje, Zanzibar kwa miaka mingi imekuwa ikinunua bidhaa kutoka nje ya nchi.

Mambo sasa hivi yamebadilika kutoka na Bwana yule kupiga marufuku bidhaa za nje ili bidhaa za ndani ya tanganyika zinunuliwe.

Mfuko wa saruji sasa hivi 15,000 lakini kama unapigia matofali, muda wa siku 3 halijakauka,wapigaji matofali wameanza kupunguza uzalishaji, baadhi ya matofali kama ya kujengea horofa kuanza kuadimika, matofali haya yanahitaji kiwango kizuri zaidi.

Hii ndio Zanzibar, kila lisemwalo tanganyika Zanzibar nayo itekeleze.

Share: