Matokeo zaidi ya kura ya maoni

Written by  //  31/07/2010  //  Habari  //  6 Comments

Wazalendo hapa kuna matokeo zaidi ya kura ya maoni ambayo tumeyapokea na bado hayajawa rasmi.

UNGUJA

Matokeo ya majimbo:

Bububu -   Ndio: 4978;    Hapana: 1622

M/Kwerekwe – Ndio: 3017;    Hapana: 2174

Kiembe Samaki -   Ndio: 1768;    Hapana: 1086

Dole -  Ndio: 2429;   Hapana: 2527

Kikwajuni -   Ndio: 3326;    Hapana: 2131

PEMBA

Sikupata matokeo na nambari kamili bali ni the nearest whole number. Pia ni matokeo ya vituo na sio majimbo.

Jadida (Wete) -   Ndio: 1800;     Hapana: 200

Utaani (Wete)  –    Ndio: 1200;   Hapana: 70

Chake Chake –   Ndio: 1000;   Hapana: 150

6 Comments on "Matokeo zaidi ya kura ya maoni"

  1. Bostoki 31/07/2010 kwa 11:26 um ·

    There seems to be a light at the end of the tunnel. Shukran kwa kutukata kiu japo matokeo hayajawa official, lakini tunapata kuona muelekeo wa matokeo yatakuwaje. Wengine kesho kazini na hivi sasa ni saa saba unusu usiku, lakini usingizi hauji.

    Mola ibariki na uirejeshee hadhi yake Zanzibar, na Uwaangamize maadui zake wasije juu daima – Aamin.

  2. chunaameirhaji 31/07/2010 kwa 11:54 um ·

    AMIN!

  3. showayb ali 01/08/2010 kwa 12:41 mu ·

    Ni haki yao, lakini Unguja bado hawajakuwa na nia safi ya Mabadiliko.
    Sijui kama kuna tofauti sana na matokeo ya kura zilizopita.
    Hapa TUME ya UCHAGUZI, UADILIFU na Wasimamizi kuwa makini.

    Salmini alisema nalitote.

    Jamani badilikeni Muiokoe nchi

  4. Administrator 01/08/2010 kwa 8:37 mu ·

    0830am:Latest:

    Unguja majimbo yaliosema HAPANA ni MAKUNDUCHI, CHWAKA, MUYUNI, KWAHANI, DOLE, CHAANI, UZI, DONGE kwa ujumla majimbo 8 tuu yamekataa na majimbo 42 yote ya Unguja na Pemba nzima yamesema NDIO.Matokeo rasmi kutolewa na Tume leo saa nne usiku.

    Zanzibar yasema NDIO, HONGERA WAZALENDO!


    Hio ndio latest kwenye chapisho la mwanzo, hivyo kwa ufupi wazanzibari wote wamesema NDIO.Tunaombwa tuache mjadala wa asili, mjadala wa asili na ukabila hauna afya tunaombwa tuache hususan kwa sasa hivi.Shukurani

    Maasalaam,

  5. zamko 01/08/2010 kwa 11:15 mu ·

    Salaam ndug wachangiaji na mada hii ya matokeo,
    Mimibado ninwasiwasi mkubwa na tue ya Uchaguzi, lakiniIshaallah ASW atatuletea kheri na faraja kwa Visiwa vyetu. Tujue huu ni mwanzo tu na sio mwiho, kinachonishangaza ni baadhi ya ndugu zetu wa majimbo ya Unguja. bado wanakasumba za CCM na hawataki kubadilika na ndio maana wakapiga kura ya hapana.

    Hawajui kwamba (ASW) kasema hawezi kukibadilisha kitu au nchi mpaka nafsi za wananchi zibadilike. Sasa kama hatujabadilisha nafsi zetu haknua kitakachobadilika. Mfano mdogo ni huuwa hayo majimboyaliotajwa kwamba hawataki mabadiliko a wanataka Zanzibar Imezwe na Tanganyika. Ndio maana wakasema HAPANA.

    Lakini Allah karim , Ishaallah tutapata uafaka wa Visiwa vytu na Wazanzibari wote walikua wamesema HAPANA watakuja nufaika. Kwani Neghema ikija humfikia kila mtu.

  6. seletochiy 01/08/2010 kwa 6:46 um ·

    kama unataka hutaki zanzibar leo imezaliwa upya.
    lakini tusile mseto tukasahu muhogo na ndizi zetu.
    ina mana tuwe macho na yanayofuatia.
    allah ndie pekee wa kushkuriwa.
    mungu ibariki ZANZIBAR.

Comments are now closed for this article.