Kwa nini wazanzibar wanaona fahari kuitwa hivyo
Written by Kipeto // 06/09/2010 // Mengineyo // 9 Comments
na watu wa upnde wa pili hawataki kuitwa watanganyika nimekaa na wazanzibar sehemu mbalimbali ya ulimwengu yeye huninasibisha na uzanzibar wake hata watoto wao walio wazaa nje ya nchi nao hupenda kuitwa wazanzibar kwa nini sisi watanganyika hatupendi kuitwa watanganyikahuona aibu kuitwa watanganyika na wakati huo sisi hujiita watanzania kwani kuna aibu gani na ikiwa tazanzania ni jina la muungano jee siku wazanzibar wakiukataa muungano tutatumia jina gani.
Nasikia hata hicho kiti cha umoja wa mataifa ni cha zanzibar jee wakikitaka wenyewe si itatufika aibu si nguo ya kuazima haistiri makalio jamani watanganyika tuamkeni na mapema leo zanzibar kila kukicha wanadai chao leo zanzibar ni jamhuri na ina mipaka yake kesho na keshokutwa watadai sarafu yao maana bendera tayari wimbo wao wa taifa wanao kimebaki nini sasa na kosa kubwa tumefanya kuwakubalia kufanya kura ya maoni hili ndio limetumaliza watakuja tumia tena kura ya maoni kuwataka wananchi wake kama wanapendelea muungano au laa ingawa tumejaribu kwa mlango wa nyuma kuharibu kura ya maoni kuwatumia watu wetu wenye asili ya bara kuwashawishi watu pia tumeshindwa ndugu zangu watanganyika tutafute tena njia nyengine kwa kuwatumia wazanzibara waliopo huku wafanya kazi ya ziada ikiwa leo maamuzi wanapelekewa wananchi si na suala hili pia watapelekewa la muungano udumu muungano wa tanganyika na zanzibar na zidumu fikra za muasisi wa muungano kwani kutengana ni udhaifu sisi sote ni ndugu




9 Comments on "Kwa nini wazanzibar wanaona fahari kuitwa hivyo"
HAHAHAHAAAAA!
NIMEGUNDUAA KUA:-
MTOA MAADA NI MZANZIBARI SIO MTANGANYIKA KAMA ALIVYOJINASIBU HAPO JUU!
TUSIPIGISHANE KELELE.
NAWASILISHA
Naungana na ndugu yangu KIMEWAKA kuwa huyu mtoa mada ni mzanzibari ila ‘anachokoza’ kuangalia response atayopata kutoka wazanzibari. Sio mbaya sana ila hupaswi kuwasemea hao ndugu zetu wa mrima.
Tuchukulie kweli mtoa mada ni mtanganyika, kwa ufupi hayo ndio makosa mliyoyafanya kulazimisha muungano kwa kutumia nguvu kuudumisha. Mlitawala viwiliwili vya wazanzibari na hamkuweza kuzitawala nyoyo zao, kwahiyo nanyi onjeni ladha hii ambayo mliwaonjesha wazanzibari kwa karibu nusu karne sasa, vipi ni tamu eeeeh!!
Napenda kukukumbusha tena ndugu yangu kuwa huu ni mwanzo tu,kuna mengi na ya msingi zaidi yatafuata kwahiyo ni muhimu kwenu kusubiri nini kitakuja baada ya kuundwa kwa serikali ya wazanzibari. Hilo jina la tanganyika litarudi na mtalitumia kama ilivyokuwa kabla ya muungano!!, nachelea kusema ila nahisi mtatafuta jina lengine lenye kupendeza zaidi masikioni…., punda ni yule yule lakini!!.
Ili kuelekea huko ndugu yangu nakuomba uanze kujiandaa kutafuta jina muafaka ili nchi yenu muipe jina zuri, huenda ukapata tunzo kwa kutoa jina zuri. Hili la TANZANIA alilitoa baba yenu Nyerere kwa ujanja wake tu.
Kila la heri, ndugu yangu mtanganyika
haahaa lazima nicheke kidogo!!!! maana huku niliko mimi kuna watanganyika wengi kuliko wazanzibari, wazanzibari tupo kama 30 hivi na watangayika wapo kama 300 kama sikosei.na sisi hutukwanwa matusi ya nguoni, wanadhani ni kejeli kutuita wazanzibari lakini kwetu ni fahari.Mara nyingi tukikutana sisi huwaita kwa majina yao kwa kuwaheshimu lakini waoa hutuita “wee mzanzibari hujambo? “kwa kejeli na indaa, lakini mimi huwaziba midomo kwa kujibu “sijambi mtanganyika HABALI YA LEO” hapo huja matawi ya chini na kuwanza kuniheshim. Mimi nadhani watanganyika hawana uwezo wa kututawala sisi WAZANZIBARI kiakili, ila wanachofanya ni kututawala kimaguvu, sasa walidhani akili inakufa kumbe nguvu ndio hufa lakini akili inakua kila siku ya mungu.Watanganyika mpoooo kumbukeni ” MCHIMBA KISIMA HUINGIA MWENYEWE”
Kila Binadamu anayo hisia na utashi juu ya kile anachokipenda, samahani sana Wasomaji wenzangu kwa mfano huu: mtu anaweza kujiita Ronaldo, anaweza kujiita Samuel Etto na majina mengine yasiyo na uhusiano na yeye, kwa baadhi ya wenzetu hujiita Mama fulani iwapo ni mke wa kiongozi (hapo unaweza kuchagua mfano lakini kichwani mwako). Sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuonesha jinsi anavyojisikia fahari kujiita hivyo na pia kuheshimu aidha mchango au hadhi ya hilo jina.
Kwa Wazanzibar kujiita Wazanzibar ni fahari kubwa kwetu kuliko kujiita Watanzania, Utanzania wa Wazanzibar umo katika Passport na nyaraka zote zinazotumiwa na Wazanzibar kwa kupata mahitajio yao tu lakini hata Utambulisho Wazanzibar wana vitambulisho ambavyo vinasomeka Kitambulisho hiki ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibr.
La ajabu ni kuwa miaka karibu 50 kasoro kidogo tu, hakuna kitambulisho cha Mtanzania lakini aahh…………… bora ninyamaze. Ukweli inatia kichefuchefu Taifa kubwa linalojuilikana duniani kote lakini halina utambulisho kwa watu wake.
Kwa sababu hizo ni lazima Wazanzibar tuone fahari kuitwa Wazanzibar kwani tunayo kila aina ya Utambulisho, Tunavyo vyeti vya kuzaliwa Vinasomeka hii ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na pia Vitambulisho navyo vinasomeka hivyo, Rais wa Zanzibar, nchi ya Zanzibar na Katiba pia Ya Zanzibar.
Ona hata kampeni tumeaghirisha kwa vile tunavyoheshimiana. Wazanzibar tuungane pamoja huu ni wakati wa mapambano juu ya kudai kilicho chetu, tunachosubiri sasa ni kuona jee hapo kabla hatukuwa na pesa/sarafu yetu kama tulikuwa nayo viongozi wetu fanyeni hima tuirudishe sarafu yetu. Kila kilicho chetu lazima tukidai hakuna kumuachia mtu hapa urafiki si kugawa mali bali ni kusaidiana tu.
A/alkm
mtoa mada mimi nakuomba usirudie tena mada km hizi kila mmoja anakujua km wewe ni mzanzibari, sisi wengine muda wetu ni mdogo na tuna mambo mengi ,tunapoamua kuingia kwenye mzalendo tunategemea kupata mamboya maana si utoto unaoufanya wewe, utaifanya mzalendo ionekane haina maana kwa mada kama hizi.
Ramadhan kareem
Nivizuri kutoa mada kama hizi ili wahusika wajuwe tunajisiaje wanapotuita Wazanzibari, kwani wao huzani kutuita Hivyo ni Kutuyarau kumbe ni fakhari kwetu. sisi WA Zanzibari wao WATanganyika
hamuogopi dhambi YA UBAGUZI mliotishwa na kambarage kwamba mkimaliza hapo itakuja sisi WAUNGUJA wao WAPEMBA? shauri zenu yule ndio baba wa taifa au mmesahau!!!
Hilo halina shaka ndugu zangu wazanzibar tulio hapa na walio nje,ufahari ulioje kuniita mzanzibar hata tukiwa bara tunajinasib kama ni wazanzibar na hatujifichi ,
lakini watanganyika nao wanajipandikiza kwa wazanzibar nje na hapa.
Nitakupeni mfano bila ya kumgusa mtu kwa jina,mmoja aliwasha mwenge mkamasini na kusema yeye ni mzanzibar,mwengine aliomba kura za wazanzibar kwa kupenda madaraka na akayapata kwa mgongo wa uzanzibar,mwengine alipata nyadhifa mbali mbali akiwa waziri wa elimu nk.lakini hakuna ambae alijipandikiza tanganyika akasema yeye ni mtanganyika ilhali ni mzanzibar.
Tanganyika(wildsail)watanganyika (wildsailer)Hawa hawakuwa na bandari au naweza kusema ufukwe wao ni watu pori,ufukwe wameupata baada ya mjarumani kuchukua kutoka utawala wa wazanzibar,sawa wamepata wao na ndio nyerere kitu cha kwanza akasema tuheshimu mipaka tuliorithi kwa wakoloni,kwa alijua fika kama iko siku wazanzibar watadai 20km costal area yao na wao watabaki muflis.
Hivyo Uzanzibar hautakufa na utazidi kuimarika duniani kote na tunauonea ufahari mkubwa kama watanganyika wanavyouonea ufahari uchogo wao.
Tunayo haki ya kujiita watanzania kwa sababu hizi–
TAN/ZAN/IA
TAN———-TANGANYIKA
ZAN———ZANZIBAR
IA—————-HAINA MAANA YOYOTE ILA KUTIA LAFDHI TU.
Lakini kwa nini niwache kuitwa kwa jina la baba yangu mzazi ,nikatumie jina la baba wa kambo? .