RISALA FUPI YA MAREHEMU UMEME ZNZ

Written by  //  22/12/2009  //  Mengineyo  //  1 Comment

Marehemu alizaliwa 1976 huko kidatu TZ BARA,Katika uhai wake aliwatumikia wazanzibar kadri ya uwezo wake,marehemu alisumbuliwa na maradhi mbali mbali kama vile kukatika mara kwa mara na mgao.
Wakati wa Salmin aliwahi kaufleti kwa kipindi cha ramadhani hadi siku kuu na serikali kuamua kuongeza sikukuu ya tano,mnamo mwaka 2008 Aliwahi kufleti kwa muda wa sk 28,na kufanikiwa kurudia hali yake ya kawaida kwa msaada wa madaktari kutoka NORWAY.
Mnamo tar 10/12/2009 Marehemu alikua katika matibabu na madaktari kutoka south afrika lakini hawakufanikiwa na kupoteza maisha Katika kijiji cha Fumba ZNZ.
Katika uhai wake marehemu alifanya mengi ikiwemo kumurika watu na mali zao pamoja na kukuza uchumi.marehemu ameacha watoto wawili,GIZA na JOTO,WAKE 2,TABU YA MAJI na HARAMA ZA NAULI KUPANDA,na HAWARA 2 Mapacha,DIESEL na PETROL.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI.
AMIN

One Comment on "RISALA FUPI YA MAREHEMU UMEME ZNZ"

  1. kijini 23/12/2009 kwa 3:27 um ·

    aka yaani inalilahi waanailiihi rajiun wengine sisi farahi all kifaya mkono wa rambi2 kwa A/K kwani ndiye iliye mkitikiya kamba

Comments are now closed for this article.